Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Naunga mkono hoja. Hata azimio la Arusha lilipijasikiwa kwa kina ktk vikao vya chama na serikali wapo baadhi ya viongozi wao chama na serikali walikuwa hawana sifa za kulinadi azimio na misingi yake, tayari walikuwa na mali na biashara ikiwemo nyumba za kupangisha kule Kariakoo n.k.mfano Kina Dosa Azizi, balozi Rupia na wengine.

Baada ya maazimio ya kulipitisha azimio kuafikiwa ikajadiliwa nani wenye sifa za kulinadi Azimio kwa umma wakati watanzania nchi nzima, sifa zikachambuliwa na watu wakatumia busara kukaa pembeni kwani hawana sifa na mwisho maamuzi ya vikao yakachora mstari mwekundu kwa kubainisha watu na makundi yenye sifa na yasiyo na sifa za kulipeleka azimio la Arusha kwa wanachi.

Vikao vikaamua kundi la VIJANA ndio waingie mstari wa mbele kujinadi azimio kwani hawakuwa na mawaa, hawakuwa wachafu kwa mujibu wake misingi ya Azimio......mwisho wakaipewa kazi ya kuhubiri Imani na misingi ya Azimio nchi nzima. Hakukua na maswali,mkanganyiko wala utata kama huu wa chanjo ya UVICO 19... ...
 
Zile nafasi 10 zilishajazwa na mwendazake!
DAA.... DUUU!!!! Hapa ndipo Paskali anasema jukwaa limevamiwa....kimbe haya mambo hata hatuyajui..Tujitahidi kuyafahamu haya mambo kabla ya kuchangia,kujua kutumia simu za kisasa hadi kujiunga kwenye makundi nyeti kama haya hakujufanyi uwe MJUVI wa kila jambo. Tujielimishe kwanza
 
Mama kateua watatu tu Mulamula Bashiru na naibu waziri mmoja nafasi zikawa zimeisha.

Naona una joto kali au ni chanjo!
 
Wanamchukulia poa mama, wanajua walifanyalo Gwajiboy anatafuta attention ili hali Gwajigirl anatafuta umaarufu.

Sasa ili kutuliza hali inategemea na iwezo wa baba mwenyenyumba mwenyewe
 
Serikali inatakiwa kummaliza huyo taperi kwa risasi nyingi za kichwa, haiwezekani hailetee dharau serikali,Ni wakati Sasa azimwe kabisa, ana chuki binafsi na Rais aliyepo Sasa, na ana ukabila wa Hali ya juu na udini pia
Wajameni,
Hivi mnataka kusema kuwa serikali YETU imeshindwa kumjibu na kumnyamazisha kwa HOJA? Hasha.
Kinyume chake mitazamo mbadala ya mwananchi/wananchi inapojitokeza yatakiwa kutazamwa kwa umakini kama changamoto. Maadam aliyewatia sumu wananchi dhidi ya chanjo ya corona na hata misingi/sababu zake vinajulikana, kinachohitajika kwanza ni kujisafisha.
Serikali yatakiwa ikubali kosa hilo na kufanya kampeni ya WAZI ili kulisafisha na ili kujenga imani kwa wananchi, panahitajika kutumia majibu yatokanayo na UTAALAMU/UTAFITI. Kama serikali itakwepa jukumu la KUELIMISHA na kuwa wakweli kwa wananchi wake, itakuwa inazidi kuingia kwenye la kutoaminika kama ilivyo sasa. AMEN
 
Huyo taperi ni wakati sasa serikali immalize mazima, Ni hatari kwa usalama wa Taifa

Ajibiwe kwa hoja,Wala isitumike hasira,Wala jazba...ajibiwe hoja zake,.ni haki yake kujibiwa,and not to be angry with him,

Anyone can be angry, that's very easy,but to be angry with the right person,to the right degree,at the right time for the right purpose,and in the right way that's intelligence...ajibiwe kwa hoja
 
No wonders the ongoing dramas are set to quit people from 'Tozo' Agenda.
We the people of this Republic we will remain firm to oppose the unjust, unfair Tozo.

About COVID-19. The National Position is 'Voluntary'. The needy to be vaccinated. And it is free as well to air out if your opinion. If goes against, the responsible will clear it will evidence...

Tozo must be Removed Now.
 
Kuna namna ya ukweli, lakini alitakiwa afute kila asiekuwa wake na aweke wake, kwa ujumla sio hao wawili tu Kuna wengi walitakiwa mpaka Sasa wawe wamepmzika Ila ndio hivyo hatujui lengo la kuwaacha hata Sasa[emoji3589]
Wasio wake? Ni wa nani?
 
Mkuu, kwenye mazungumzo kuna mambo muhimu ya kuihimili katika lugha mtumiayo. Hata lugha ya kiingereza ambayo kwa kwa sisi tusozaliwa huko duniani lugha hiyo huitwa "second language".

Baadhi ya mambo hayo huitwa "listening and hearing" na bila kusikiliza huwezi kuelewa undani wa jambo anolizungumza mtu.

Kusikiliza ni kipaji pia na husaidia watu wengine kuwa washauri wazuri kwenye migogoro au kutokuelewena.

Kushindwa kusikiliza kisawasawa hupelekea kutafsiri visivyo kile kinachozungumzwa na hupelekea kuzidisha migogoro au kutokuelewana.

Kusikiliza kunahusiana na kumbukumbu kwa kusadia kukumbusha matukio fulani yalotokea nyuma.

Mchungaji Gwajima jana katumia reference zote, mifano yote na watu zaidi ya 700k walikuwa hewani wakimfuatilia na kumsikiliza ndani ya nchi na nje ya nchi.

Je weye, ulipata muda wa kumsikiliza na kumwelewa kabla hujaandika hii?
 
Kiutaratibu, kama unataka kuwa huru na mawazo yako usijiunge na taasisi ambazo huwa zina taratibu zake, unapokubali kujiunga na hizo taasisi basi ni lazima ufuate sheria na taratibu utakazozikuta, na mojawapo ya taratibu hizo ni ile ya wengi wape, wachache wasikilizwe.

Sasa mkishakubaliana kwenye vikao vya chama jambo fulani, sharti mkitoka huko wote muwe kitu kimoja hata kama hukukubaliana na maamuzi ya wenzako, kinyume na hapo ukianza kelele kwenye public kupinga misimamo ya wenzako unageuka msumbufu na kuishushia heshima taasisi uliyopo.

Kama kila mmoja akiamua kupayuka kivyake kwenye public hapo inakuwa ni vurugu, hiyo sio demokrasia unayotaka kuaminisha watu, demokrasia ndio uhuru wa kutoa maoni ambapo wengi hupewa, kasoro kwenye chaguzi zetu ambapo tume huwapa wachache.
 
Sema hapo jina ulilo maliza kwa kuandika ndo limekaa kizalendo achana na pascal.
 
Kuna thread nilitaka kuianzisha kuhusu Gwajima na hao mawaziri wa afya, lakini kwa vile umeshaianzisha ngoja niweke hapa mawazo yangu japo yapo tofauti kidogo.

Katika hii vita ya Gwajima askofu na Gwajima waziri nikiri tu kwamba Gwajima askofu anaonekana kuwa na hoja nzito, za msingi, za muhimu ukiondolea mbali drama zake.

Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama mtu anayeusema siyo mwakilishi mzuri wa huo ukweli.

Ukiachilia mbali inconsistencies za mawaziri wa afya, kuna mambo kadhaa ya kufikirisha yaliyomo kwenye hoja za Gwajima.

1. Hivi kweli tumaini la suluhu ya corona na madhara yake Tanzania yapo kwenye kinga ya corona ya Johnson & Johnson iliyotolewa kwa msaada wa Marekani? Dozi milioni moja? Hebu tuwe serious, let us say kwamba kinga ya corona ya J&J does work, kwamba ukiipata huji kufa kwa corona. Kwa corona ambayo imekwisha sambaa miji yote Tanzania na vitongoji vyake, serikali inayotuhamasisha tujichanje kama tukiitikia wito wake, itatutosheleza? Huo ni usanii, ni kuwapa wananchi tumaini feki na kujitia kufanya mambo ambayo aidha serikali haiyajui na haiyawezi.

2. Kuonyesha hilo hapo juu jinsi serikali inavyofanya mambo bila kuyafikiria kwa kina hoja ya pili ya askofu Gwajima ni kuhusu namna serikali inavyoweza kupata taarifa za maendeleo ya watu waliokwisha chanja. Kutokana na kwamba hizi chanjo bado ni experimental, real time data ya waliochanjwa, maendeleo yao hasa ukilinganisha na wasiochanja ni muhimu sana. Huko kweingineko tunasoma kwamba watu wengi waliokwishachanja wameambukizwa mara ya pili, kuliko au sawa na wasiochanjwa. Kinachowapa moyo wa kuendelea kuzipigia debe chanjo ni kwamba wale walioambukizwa wakiwa wameshachanjwa pengine madhara yangekuwa makubwa (worst outcome) zaidi kama wasingekuwa wamechanjwa. Kinachokosekana kwenye narrative hii, ni ubora wa matibabu, inawezekana kabisa kwamba wale waliokwishachanjwa kinachowasaidia ni kwamba nchi hasa zilizoendelea tayari zimeshafahamu namna bora ya kudeal na ugonjwa wa corona, kuliko ilivyokuwa awali, na wala si chanjo. Je hilo linaapply kwetu? Sisi kwetu hapa mtu anakufa tu just kwa kukosa hata ventilator tu.

3. Nini hasa lengo kuu la chanjo kwenye kudili na corona? Wanavyotuambia ni kwamba ilibidi tulockdown kabla chanjo haijapatikana, tusiambikizane kizembe kabla chanjo haijapatikana, watu wasijekufa wengi sana kabla chanjo haijapatikana, ili tubuy time chanjo ikipatikana itusaidie kufikia herd immunity. Sasa Tanzania hatukufanya yote hayo. Kwa maana nyingine tuliambukizana sana, waliokufa walikufa na wasiokufa waliishi. Ila kama uliishi maana yake una natural immunity. Haiwezekani kwa nyomi ile ya Kariakoo, kwa watu tunavyolundikana kwenye madaladala, watoto mashuleni, mihadhara kanisani na misikitini eti hatukuambukizana. Je chanjo itakuwa bora zaidi ya natural immunity? Kuna scientific ground ya kusupport kwamba chanjo itakuwa bora kuliko natural immunity? (Na pia kama kitakuja kirusi kipya kitakachokwepa natural immunity iliyojengeka awali, sidhani kama kitashindwa kukwepa artificial immunity ya chanjo).

4. Mwisho, Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kufollow the agenda tu. Lazima tuwe nchi ya kuset the agenda. Ina maana tulipata uhuru kutoka kwa mkoloni ili tukae tusubiri afya zetu zitegemee kudra za wale waliotutawala? Na hapa ndipo Gwajima (askofu) anapopata credit fulani fulani za kisiasa. Ni kweli nchi ilikuwa haijajiandaa kukabiliana na corona, na hata yale mambo ya kujifukiza na kutengeneza traditional remedies ilikuwa ni kujaribu kudeal na issue kulingana na uwezo wetu. Kuna watu wanatumia huo ukienyeji kudiscredit approach ya Magufuli, lakini kuna wengine tunauona huo ukienyeji kama mwanzo wa kile alichotumia muda mwingi akikihubiri kwa watanzania, kwamba watanzania tujitambue, tujielewe, tusisubiri mjomba wala shangazi wa nje kudili na ishu zetu. Kwamba majanga kama hayo ni eye opener kuwa Tanzania iwe tayari na ijenge internal capacity ya kudeal na threat bila kusubiri kudra za mataifa mengine. Kitendo cha Magufuli kufa, na mara moja aliowaacha wanabadili gia angani na kuanza kuona kwamba yale yote tuliyokuwa tukiyafanya hayana maana tena, wanafikiri sisi watanzania ni maboya kiasi hicho?

I wouldn't like Gwajima awe president wangu, lakini I can see the man is intelligent anajua nini watanzania wanataka na kwa vile ni con artist he is saying all the right things, he is demonstrating all the right attitude leader wa nchi anapaswa kuwa kuhusu nchi yake na watu wake. Yangu macho na hapa nilipo nina pop corn zangu!
 
Umekosea sana kutaja jina wakati ulisema tusitaje jina la mtu wakati wa kuushambulia uzi. Sawa umeeleweka, na ndivyo ilivyo tuliisema mapema hii. Mguu alioanzia kuukanyaga Mama katika hii mambo ya covid na chanjo alimiss step, sijui ni kwanini ama hakutaka kuvuruga sana ilikua mapema.

Ingawa najua na nina amini kuwa reshuffle ipo tu tena ya maana ni vile Mama alitaka transition kipindi cha mpito kile ili asiamshe popo.

Ahsante.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…