Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Sijamaliza kusoma bandiko lako kwa kuwa pendekezo lako la kupumzishwa mawaziri wawili,ambao unajua kabisa hawana makosa,walikuwa/wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao kwa mkuu wa nchi. Wakati ule hawakufanya makosa yoyote kutii msimamo wa CinC kama ambavyo na sasa hawafanyi makosa yoyote kwa kutii msimamo wa CinC wa sasa.

Kinachokusumbua, Paskali,ni ukabila. Subconsciously uko upande wa askofu Gwajima kwa sababu ya ukabila, kama ambavyo,pamoja na kidhalilishwa hadharani na JPM kwa kuwa alikuwa msukuma mwenzio,uliamua kuwa mtetezi na mnazi wake!

Ushauri wako umekosa kabisa mantiki. Mawaziri wajihudhiru kwa sababu ya kelele za mbunge wa Chama chao anayepinga maamuzi ya serikali ya chama chake? Huo ni ushauri au mzaha?
 
Naona jiwe la Mayala limekupata!

Askofu Gwajima umetinga front kujitetea mwenyewe. Angalia usije kujeruhiwa au kuuawa. Frontline siyo mchezo!
 
Kwani msimamo wa chama ni lazima uwe sahihi kwa maslahi ya nchi kwa ujumla? Ina maana haiwezekani ukawa mbunge wa chama na ukatofautiana na chama chako kwa baadhi ya mambo?

Si ndiyo hicho tunachokililia siku zote, kwamba wabunge watangulize maslahi ya nchi kwanza kabla ya maslahi ya chama chao? Au kwamba yule mbunge wa Kigamboni (Ndugulile) aliyetofautiana na mwenyekiti wa chama chake kuhusu masuala ya kujifukiza si alikuwa anasikilizia utashi wake unamtumaje? Hatutaki mawaziri wasioelewa wanachokifanya, hawapo pale kuwa marobot. Nafasi ya uwaziri ni kuwa think tank siyo kuwa robot la kutekeleza amri tu.

Askofu Gwajima pamoja na kuwa hakubaliani na chanjo pia anaexpose unafiki na undumilakuwili wa wanaojifanya viongozi wa Tanzania.
 
In my opinion,
Rais alipaswa kuwaondoa hawa mawaziri wawili hata kabla ya kuunda ile kamati ya kuhusu CORONA.Kuwepo kwao tu mpaka sasa,kunawapa skeptics wa chanjo grounds kwenye arguments zao sababu hawa mawaziri wawili walishaaminika na wananchi kwa kupitia nafasi zao hasa ukizingatia asilimia kubwa ya jamii ya watanzania bado haikubahatika kupata elimu rasmi ambayo pengine ingewasaidia kupambanua mambo independently.
Issues za public health duniani zina changamoto zake nyingi hasa hasa consipiracy,-Na moja ya njia za kupambana na conspiracy theories ni kuhakikisha public inapata reliable and trusted information kutoka kwenye vyanzo vya vinavyoaminika hasa serikali pamoja na kuteua watu wanaoaminika na jamii kwa ujumla ikiwemo ku-inforce sheria dhidi ya watu wanaoeneza taarifa potofu zinazoweza kuhatarisha Afya ya jamii husika nk. Tukiangalia context ya Tanzania-Hawa viongozi wa wizara walishakosa credibility ya kiuongozi kwa jamii hasa kwenye hili swala la CORONA kupitia conspiracy theories ambayo ndiyo key pillar ya ku-defeat CORONA.

Uwepo wa hawa viongozi madarakani una implication nyingi sana ikiwemo,
-Mwamko mdogo kwenye uchomaji wa chanjo,sababu mabalozi wa njanjo yenyewe walisha waaminisha umma kwamba chanjo ni hatari therefore mabalozi walewale wanapokuja kuuaminisha tena umma kwamba chanjo ni salama wana-create more confusion than clarity.
-Uchomaji Mdogo wa chanjo unapelekea wastage of national resources,sababu chanjo inanunuliwa na serikali lakin demand hakuna hvyo kupelekea baadhi ya chanjo kuwa disposed. Hata ambazo pia zipo,inabd pia zikae kwenye refridgerators kwa muda mrefu huku ziki-consume power needlessly hvyo ku-raise cost ya storage na burden kwa tax payers.
-Kama Rais hatoingilia kati kwa makusudi na kwa wakati,atakuwa anaufanya uchumi kuendelea ku-suffocate bila reasonable grounds.Rapid recovery ya GDP za mataifa mbalimbali ikiwemo US zimekuwa linked na faster vaccination rates.Hivyo basi,Lower vaccination speed is very very harmful to our economy.
Public Trust ya wananchi kwa government ni jambo la muhimu sana,na kuendelewa kuwepo kwa hawa watu kunapelekea serikali na serikali zijazo kwenye very very dangerous path,path ambayo watu watakuwa wanaamin taarifa za mtaani kuliko serikali au viongozi wa serikali hvyo kufanya handling ya majanga mengine ku-suffer serious blows.
 
Rais anademka tu anaunda tume kula posho tu, hakuna lolote la maana. Aendelee kupiga usingizi wa pono. ''Majuto mjukuu.''
 
Siku hizi sijui umekuaje!
Yaani unafikiri Gwajima anasikizwa na kutazamwa na watu wengi kwa vile anaongea akiwa Mbunge?
Kwa hiyo solution ni kumtemesha Ubunge?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Wakati anapambana na Makonda,Pengo,mahakama ya kadhi,alikuwa anasikilizwa na kufuatiliwa na watu wangapi?

Unafikiri Gwajima anatafuta umaarufu? Yeye tayari ni maarufu.
Labda unauchungu wa kukosa Ubunge Kawe.

Pole Mami.
 
naona kama

Nyumba yetu inazidi makelele, jee tumshinikize Mama aonyeshe uwepo wake, kwa kuonyesha uwezo wake kuwadhibiti na kuwatuliza hawa watoto wake wasio na adabu​

Mama ameonyesha uwepo wake!.

Mama, wengine wamefikia kukudharau wazi wazi, hata kama wewe ni mpole vipi, angalau anza kuonyesha uwepo wako na uwezo wako kuidhibiti nyumba yako, kwa kuwaadabisha watoto wako, wawe na adabu,​

Mama kaanza kuadabisha, sasa ni heshima na adabu kwa kwenda mbele!.

anza na wale marrionates wako wote wawili uliowakuta pale mahali, na ukawaacha na kuamua kuendelea nao, wapumzishe, au vinginevyo na wewe kama unapenda ze comedy, then tuendelee nao.​

Kwa vile Mama anakwenda kufumua the cabinet, ushauri huu bado uko very valid.

Mama Onyesha Uwepo Wako, Onyesha Uwezo, Pumzisha Baadhi ya Comedians Uliowakuta.

Mama hongera sana, umeisha onyesha uwepo, na umeonyesha uwezo wako, sasa imebaki kazi moja tuu, kupumzisha.

Mtu unaposhauri kitu, halafu ukaona kimetekelezwa, lazima urudi kupongeza.
Hongera sana
Kazi Iendelee!.
P
 


Kaka Paskali sidhani kati ya hao kuna asiyejua nguvu ya kiti cha urais/ufalme/umalkia/amiri jeshi mkuu.
Sidhani kama wanayoyafanya hawajui matokeo yake.
Sidhani kama walikua na ushauri na wakakosa au kushindwa kumshauri nje ya hadhara.

Tuendelee kuliombea taifa letu amani tukijua katika kila nchi kuna muwakilishi wa Mungu ambaye ni mtawala mkuu/ Mfalme/Rais wa nchi hiyo.

Kwakuwa taratibu za kumpata zilikua sahihi, na kwakuwa tumeamriwa na Mungu kuwa watii. Hatuna budi kuwa watii huku tukimuomba Mungu usiku na mchana kwaajili ya ustawi, amani na mafanikio ya Rais na taifa letu; huku tukipeleka haja zetu nyingine zisizokuwa na hila kwa Mungu tukiwa safi.

Kwa tunaamini chochote Rais anachokifanya kipo anachokijua na kukiamini; basi na sisi tuendelee kuomba ili Mungu amuongoze kwa maono na ndoto atufikishe pale tunapohitaji

Katika hili sakata wapo wanaotoa ushauri mzuri au pongezi nyingi kwa Rais lakini ni wenye hila ndani yao na muda utasema. Maadui unaowajua ni bora zaidi ya marafiki usiowajua na ukadhani ni marafiki kumbe wana jambo lao.

Wapo wanaoongea lugha mbovu/dharau/chuki/dhihaka dhidi ya Rais sababu wanaumia kwa yeye kuwa kwenye hicho kiti na wanaona hastahili. Hawana mpango kabisa wa kumsaidia Rais wanatamani watumie nguvu zao binafsi kuonyesha misimamo yao kwamba wako bora zaidi. Ila tuu wanajisahau kwamba hawana hiyo mamlaka.

Wapo wanaoongea na kukosoa kwa nguvu bila mipaka sababu wanaamini kwamba mambo yanayofanyika sio sahihi na hayawapendezi ila wanahisi hawana nafasi ya kusikilizwa. Lakini wanasahau SSH ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Busara ni bora kuliko nguvu, wangeangalia njia bora yenye maslahi ya taifa ingekua bora zaidi.

Watanzania tumuombee Rais. Tumuombee apate watu sahihi wa kutafsiri kile anachotaka kufanya, na apate wasaidizi wa kukifanya kwa usahihi uleule uliotafsiriwa. Mungu ni mwema sana kwetu na ataendelea kututendea mema kadri tunavyomuomba kadri ya nia zetu njema ukamilifu wetu mbele zake.

Yohana 16:23-24
"Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili."


Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…