Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,380
Nimeyaona mengi Sana, Dkt. Slaa alijengewa nyumba na CHADEMA alipohama Chama hicho wakachukua nyumba yao huku walimpa bure, Tuntemeke Sanga wa Njombe alijengewa nyumba na Mwl. Nyerere alipoanza kumpinga akafukuzwa kwenye nyumba hiyo, mwaka 2004 nikiwa Dar es Salaam nilishuhudia Mkuu wa idara ya MAHAKAMA akifukuzwa kwenye nyumba aliyojengewa na Serikali baada ya kufuta mashitaka ya mtuhumiwa ambaye Serikali walitaka afungwe.
Nyumba za kujengewa huwa ni za mazingaombwe ni bora ukapewa Pesa/Hundi Mbele ya Wanahabari na ukajenga mwenyewe. Pia ni bora ujenge nyumba wewe mwenyewe kwa ramani unayotaka mwenyewe kulingana na uhitaji wako.
Mimi DJ. Don Nalimison sitapokea nyumba yoyote hata Kama NDugu watumike kuijenga. Natafuta Pesa zangu mwenyewe na nitajenga mwenyewe.
Regards
DJ. DON NALIMISON