Kuna nyumba moja niliwahi kuishi nilikutana na maza mmoja mtata sana. Wakati nahamia mume wake alitaka kuweka uzio katikati maana zilikuwa nyumba mbili kwenye uzio mmoja lakini huyu maza alikataa. Ilikuwa nikipata mgeni ananiita kuniuliza anakaa hadi lini, kuna wakati aliniambia sasaivi shimo la maji taka limewahi kujaa inaonekana nawageni wengi wanaotumia choo na kuflash mara kwa mara.
Siku moja mapema alinipigia simu na kuniambia mkataba ukiisha nihame baada ya kumuona mdogo wangu anatoka kwangu asubuhi. Huyu dogo aliwahi kunitembelea maza akaniita kuniuliza nikamwambia amekuja kutembea tu ataondoka, dogo aliondoka baada ya wiki akarudi tena kwangu ndio asubuhi yake alipomuona maza akanipigia kunipa taarifa zile za kunitaka kuhama.
Nashukuru nyumba niliyopata sasaivi naishi peke yangu japokuwa kuna nyumba mbili lakini hii moja mwenye nyumba kaweka mlinzi tu yeye hana time yuko zake nje ya nchi, hapa nakaa kwa amani sana naimani sitahama hadi nahamia kwangu 😛