BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mgogoro huo ulikuwa ukifukuta kimyakimya lakini kwa sasa umepamba moto kutokana na nyumba za wakazi wa eneo hilo kuwekewa alama ya X na kuelezwa kuwa kufikia Alhamisi wiki ijayo (Juni 13, 2024) nyumba zitakuwa zimebomolewa.
Nimefuatilia masuala kadhaa kwa ukaribu sakata hili baadhi ya Wananchi wanaeleza kwamba waliuziwa viwanja hivyo kwa utaratibu kupitia mamlaka za Kiserikali kwa kuwa viwanja hivyo vilikuwa ndani ya Manispaa.
Baadhi ya Wakazi wanadai kwamba walipeleka maombi ya kuweka zuio Mahakamani lakini ombi hilo limetupiliwa licha ya kesi hiyo kuendelea kuwepo Mahakama.
Wanasema kumekuwepo na mchakato wa maridhiano baina ya MMM (anayedaiwa kushinda kesi) na Wananchi, ambao ulianzishwa kwa lengo la kuleta suluhu nje ya utaratibu wa Kimahakama baada ya uwepo wa taharuki baada ya uamuzi.
Wananchi wanadai kwamba Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliwaahidi kufanya mazungumzo na MMM kutafuta suluhu lakini wanadai matumaini yao yameisha baada dalali wa Mahakama pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na kuweka nyumba zote zilizopo kwenye eneo hilo kuweka alama ya X tukio ambalo linaleta taharuki kubwa kwa Wakazi.
Sijapata nafasi ya kusikiliza upande wa MMM lakini ukisikiliza upande wa Wananchi unaona kuna uwalakini, Wananchi wanadai kuwa kuna mazingira ya kugushi nyaraka pamoja na Rushwa.
Kwa namna nilivyofuatilia suala hili nimuombe Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa pamoja na TAKUKURU wamulike suala hili kubaini mazingira halisi yaliyopo, maana imekuwa ikishuhudiwa manung'uniko mengi kwenye jambo kama hili.
Mwenyekiti wa Juma Hashim Kipita, Tungutungu amesema:
Huyo anayedai ni mmiliki alikuja na nyaraka akasema alinunua eneo hilo Mwaka 1995, jina la mtu anayemtaja alinunua kwake alikuwa babu yangu, moja ya majina anayotaja ni tofauti na uhalisia wa majina ya babu yangu.
Ninavyofahamu hapa kuna raia wa India alikuwa anamiliki baadaye akaondoka eneo likabaki wazi, wenyeji waliokuwepo wakaanz kuchukua maeneo na baadaye kuanza kuyauza.
Hivyo, huyu alipojuna na nyaraka za Mahakama, tunatakiwa kumuwekeza zuio lakini kwa kuwa hakuna nyaraka muhimu za umiliki inakuwa ngumu kuweka zuio, pia tunajiuliza tangu Mwaka 1995 kama anavyodai, alikuwa wapi siku zote?
Hata hiyo kesi anayosema ameshinda siyo dhidi ya watu waliopo hapa bali ni watu ambao walishi hapa miaka ya nyuma na kwa sasa hawapo.
Pia soma ~ Waziri wa Ardhi azuia mchakato wa kutaka kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga