Nyumbani ni nyumbani, karibuni Mafia

Siku mtakayopata boti ya mojakwamoja Mafia kuja Dar es Salaam basi mtagomboka kwelikweli, maana kiila mtanzania wa Dar es Salaam atataka apande boti aje kupaona kunafanania vipi, washazoea Zanzibar wengi Mafia hawajafika, usafiri wa uhakika toka Dar ukiwepo wengi watakuja, ila wahamiaji wataingezeka pia
 
Mkuu itabidii nikutafute niko interested sana na kufanya biashara ya vitunguu comoro ila sijuii ni anzie wapi na mtaji kama 1.5m hivi

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Twende wote pls
Hahaa! Ushawahi kutumia mashua lakini?! Mimi ninapoenda Mafia/Zanzibar napenda sana kutumia usafiri wa maji kuliko wa anga ambao sio adventurous kabisa.

Let's go on December
 
Hahhaaha.. Nilikaa huko miaka mitatu ajabu nyama ya ngombe nikawa siipendi tena....

Kwa jinsi walivyo fresh na varieties huwezi kinai aisee

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
Unajua mara ya mwisho kwenda Mafia, nilikaa kama mwaka mmoja hivi huku nikitoka kwa vipindi vifupi vifupi tu! Sasa wakati naandika hiyo post uliyoni-quote nilikuwa najaribu kuvuta kumbukumbu kama kwa muda wote huo niliwahi kununua nyama!

To be honest, sikumbuki kama niliwahi kununua nyama hata siku moja! Na kv kisela sela ni ngumu sana kula mboga ya majani, basi kuna uwezekano mkubwa within 1 year, sikutumia mboga yoyote zaidi ya samaki!

Kitu pekee ambacho ni tofauti kidogo ni kamba, pweza na ngisi ambao na wenyewe ni samaki!
 
Ndege hatutaenjoy ..twende na boat naskia Sasa hivi Kuna boat sijui meli.mie usafiri wa maji nimeshazoea siogopi. ...twende 28th oct
There you're!! For adventure, ndege haifai! Tena ukiweza, hata boti tupa kule, unapanda mashua ambayo hamkawi kujikuta mmetokezea nchi za ng'ambo angalau Comoros hapo!!

Unajua ukikutana na upepo mtamu mtamu, hizi boti uchwara zinapitwa na mashua kama zimesimama!! Na siku niliachana na mambo ya kupanda boti, ilikuwa tunatoka Mafia to Dar, and by the time, boti ambayo nilipanda ilikuwa one of the best boats kisiwani!

Sasa unaambiwa siku ya siku kulikuwa na winter baharini la kufa mtu, na tumetoka Mafia mapema zaidi huku tukiwa tumeiacha mashua pale wala dalili za kuondoka hawana!

Nadhani tulikuwa halfway of the route huku tukipigwa baridi na mvua juu! Huku na kule, tunaona tanga kwa mbaaaaali linatoa saluti but in no time, jamaa na mashua yao wakatuacha kama tumesimama!

Ile na sisi tunawasili Kisiju, tunaikuta ile mashua inakula land and sea breeze huku kukiwa hakuna wala dalili kwamba walipakia watu na mizigo... yaani raia washasepa zamani hizo!
 
Hahhaaha umenikumbusha unajua kule mboga za majani ni anasa kipind kile.. Ndio maana anemia ilikuwa juu Sanaa...

Yaani maisha kule ni wali samaki [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€! Umeandika nikaisoma kihisia fulani dahπŸ˜‹
 
Miaka ya 80 nilikuwa daktar wa mifugo hapo lakini hapakuwa na abbatoir yaani machinjio ,!
 


Mtu anayekula Sana samaki huwa Wana upeo mkubwa Sana wa akili! Naamini uko hivyo!..
 
Mtu anayekula Sana samaki huwa Wana upeo mkubwa Sana wa akili! Naamini uko hivyo!..
Maybe, twende basi December... tukifika, kuanzia breakfast hadi msosi wa usiku, full samaki hadi tunarudi! Maybe tutarudi tukiwa vi-genius fulani hivi!!!
 
Miaka ya 80 nilikuwa daktar wa mifugo hapo lakini hapakuwa na abbatoir yaani machinjio ,!
Ng'ombe walishavuka bahari kitambo! Tena naya-miss sana maziwa ya Mafia manake ilikuwa ni 100% guaranteed no water milk chini ya project iliyokuwa inaendeshwa na Mama Chole (if am not mistaken)!
 
Hahhaaha umenikumbusha unajua kule mboga za majani ni anasa kipind kile.. Ndio maana anemia ilikuwa juu Sanaa...

Yaani maisha kule ni wali samaki [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
Yah, ilikuwa ni anasa kweli kweli labda wabadilike na kuanza kulima mbogamboga kwa wingi kwa sababu inawezekana kabisa! Nilishawahi kwenda Kirongwe, kulikuwa na shamba la magereza... jamaa walikuwa wanatoa vitunguu vya maana hadi unaweza kushangaa kwamba vinalimwa Mafia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…