Nywele bandia: Je ni mvuto, au kudharau uafrika?


Tena afadhali ya hawa wa nywelebandia kuliko wale wanaojichubua ili wawe wazungu...
 
Tena afadhali ya hawa wa nywelebandia kuliko wale wanaojichubua ili wawe wazungu...

Haaa haaa sawa , Mkuu.
Sasa hawa wa nywele tuwasaidieje ili wabadilike aisee?, kisha tutakuja kwa hao wa kujichubua
 
Haaa haaa sawa , Mkuu.
Sasa hawa wa nywele tuwasaidieje ili wabadilike aisee?, kisha tutakuja kwa hao wa kujichubua

serikali ipige marufuku uingiziaji wa nywele bandia, na pia ipige marufuku madawa au kemikali zote za kujichubua...kwani yote hayo ni ukiukaji wa haki za binadamu
 
serikali ipige marufuku uingiziaji wa nywele bandia, na pia ipige marufuku madawa au kemikali
zote za kujichubua...kwani yote hayo ni ukiukaji wa haki za binadamu

Mkuu, nimekuelewa., Naamini wanaona hayo maoni yako. Asante.
 
Wazungu wenyewe wanasgonea weaving. Nilishangaa sana

Binti, ni kweli kabisaa ila wao wanasongeana hizo weaving za kufanana na nywele zao , na siyo kusongeana weaving za kiafrika kwa mfano. ana nywele zake anaweka bandiko lenye muonekano wa kizungu.
Yeye hawezi kusongea bandiko la kiafrika .

Sasa kwa nini sisi tuweke bandiko nywele ya kizungu, mfano, mtu ni mweusi anaweka nywele zina rangi ya dhahabu/ kreamu na rangi nyinigezo hadi leo naona rangi ziko za blue, kijani, nyekundu, njano,nyeupe peeee kama tui la nazi duuuh!
je hatuwezi kuweka ya kiafrika zaidi badala ya kuiga hadi rangi za kizungu na nywele ndefu sana yaani hapa unashindwa kujua ni kichwa cha mzungu mwili wa mwaafrika au macho yangu hayaoni vizuri jamani?

Je ni sawa kufanya hivyo? na kama siyo je tuwasaidieje wanaoweka bandiko nywele hizo?
 
hilo nalo neno....tena zito kwelii!🙂
 
Nachukia sana haya madubwana yaitwayo mawigi, mwanamke akilivaa wigi huwa namshusha thamani yake kbs hata kama atakuwa mjanja kiasi gani
 
Urembo wowote bandia ni mvuto tu na ni njia ya wanawake kuboresha uzuri wao. Nywele bandia zinazikamilishia mvuto zile zako za asili na si udhaifu au kutokujiamini. Mwanamke ni pambo na zaidi ya yote mwanamke anatakiwa ajisikie vizuri na mrembo wakati wote hivyo kama kuweka nywele bandia kunampa furaha na hisia nzuri, si tatizo akiweka.
 
Ni kweli hili la Nywele za dukani limeshakuwa janga la Afrika sambamba na hiyo mikorogo mikali ya kisasa hasa kwetu sisi wanawake na Tatizo kubwa ni ulimbukeni na kuiga kumetawala, lakini pia ninyi wanaume mnachangia uwepo wa uozo huu:iweje mkeo ajiharibu uasili wake na we unampenda na uko nae umeridhika tu na hali hiyo?? We ndo mtoa hela ya wigi ya mkorogo na unamuona daily anayatumia kujiharibu unamuacha tu. Badilikeni wanaume na hili janga litapungua kama sio kuisha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…