O.J.: Made in America

O.J.: Made in America

If it does not fit you must acquit.
 
Kwa uzoefu wako, unahisi kwanini mablack celebs wengi huwa wanaishia kufanya maamuzi ya ajabu na kubomoa mafanikio yao waliyoyapata kwa kipindi kirefu?

Sijawahi kuona takwimu zozote zile zinazoonyesha kuwa watu weusi wengi walio maarufu huishia kufanya maamuzi ya ajabu na kubomoa mafanikio yao waliyoyapata kwa kipindi kirefu kulinganisha na watu maarufu wengine wa rangi zingine. Hivyo siwezi kuwa na maoni juu ya hilo.

Ni kweli hizi stori tunazoambiwa kuwa wazungu wako inclined kuhakikisha waafrika wenye mafanikio wanashuka chini au ni imani potofu tu?

Binafsi nadhani ni dhana potofu tu na ni kisingizio cha kukwepa kuwajibika kwa matendo yako mwenyewe. Kuwajibika kwa matendo yako mwenyewe si kazi rahisi. Ila kunyooshea wengine vidole na kusema wao ndo sababu ya madhila yako ni kazi rahisi mno.

Ni kweli kuwa idadi kubwa ya black celebs and athletes waliopata mafanikio huishia kufilisika au kufanyiwa mizengwe kufilisika au ni sisi ndiyo tunaoverestimate hiyo idadi?

Bila takwimu ni vigumu sana kuwa na mtazamo wowote juu ya hayo.
 
USA BABY,
nasikia jamaa is a father to one of the kardashians,Ngabu taarifa plz
 
USA BABY,
nasikia jamaa is a father to one of the kardashians,Ngabu taarifa plz

Yeah hata mi nishasikia hiyo.

Baba yao na akina Kim, marehemu Robert Kardashian, alikuwa ni mshikaji wa O.J.

Sasa labda alimzunguka mshikaji wake na kuchepuka na mke wake.
 
Yeah hata mi nishasikia hiyo.

Baba yao na akina Kim, marehemu Robert Kardashian, alikuwa ni mshikaji wa O.J.

Sasa labda alimzunguka mshikaji wake na kuchepuka na mke wake.
haha hahahaa miafrika ndivyo tulivyo
 
Sijawahi kuona takwimu zozote zile zinazoonyesha kuwa watu weusi wengi walio maarufu huishia kufanya maamuzi ya ajabu na kubomoa mafanikio yao waliyoyapata kwa kipindi kirefu kulinganisha na watu maarufu wengine wa rangi zingine. Hivyo siwezi kuwa na maoni juu ya hilo.

Binafsi nadhani ni dhana potofu tu na ni kisingizio cha kukwepa kuwajibika kwa matendo yako mwenyewe. Kuwajibika kwa matendo yako mwenyewe si kazi rahisi. Ila kunyooshea wengine vidole na kusema wao ndo sababu ya madhila yako ni kazi rahisi mno.

Bila takwimu ni vigumu sana kuwa na mtazamo wowote juu ya hayo.
Je ukilinganisha wazungu na wamarekani weusi unahisi kwanini wazungu wana mafanikio sana kuliko wamarekani weusi ingawa wanaishi nchi moja?

Unazungumziaje uchaguzi wa mwaka huu na tabia ya Donald Trump katika kampeni zake. Unahisi ana nafasi yoyote ya kufanikiwa kushinda pamoja na kauli zake tata kama kupiga marufuku waislam kuingia Marekani n.k.

Kama ukiambiwa uelezee kitu kimoja ambacho Obama amefanikiwa kufanya katika urais wake, utataja kitu gani?

Kumekuwa na wimbi kubwa la waafrika huku Afrika waliojenga imani kuwa kuishi Marekani ni guarantee ya mafanikio. Je kuna ukweli katika hilo au ni imani potofu tu?

Juzi tulipata taarifa kuwa kuna mtu ameingia kwenye club ya mashoga huko Orlando na kuua watu 49. Ni nini maoni yako juu ya ushoga?

Je ikitokea umekuwa Rais wa Tanzania, ni kitu gani kitakuwa kipaumbele chako?
 
Je ukilinganisha wazungu na wamarekani weusi unahisi kwanini wazungu wana mafanikio sana kuliko wamarekani weusi ingawa wanaishi nchi moja?

Sababu zipo kadhaa na chache zikiwemo za kihistoria, kimfumo, kitakwimu, na kijamii. Kihistoria - watu weusi walikandamizwa kutokana na hali yao ya kitumwa ambapo hawakuhesabiwa kama binadamu bali walihesabiwa kama mali. Kimfumo - sheria za kibaguzi kama za Jim Crow ambazo ziliwakandamiza watu weusi kwa kuwanyima elimu na mambo mengine ya msingi. Kitakwimu - idadi ya watu weusi wachache sana kulinganisha na watu weupe. Kijamii - watu weusi nao wao kwa wao wana matatizo yao. Kwa mfano, mtoto mweusi anayefanya vizuri darasani huwa anaonekana eti 'ana act white' kisa tu yuko makini katika elimu. Labels kama hizo huvunja mioyo ya watu wengi na hivyo kufanya jamii kwa ujumla wake kukosa mafanikio.

Unazungumziaje uchaguzi wa mwaka huu na tabia ya Donald Trump katika kampeni zake. Unahisi ana nafasi yoyote ya kufanikiwa kushinda pamoja na kauli zake tata kama kupiga marufuku waislam kuingia Marekani n.k.

Uchaguzi wa mwaka huu uko tofauti sana na chaguzi za miaka ilopita. Hilo ni kwa sababu mgombea mdhaniwa wa chama kimoja, cha Republican, siyo mwanasiasa.

Donald Trump anaweza kabisa kushinda [ingawa binafsi sidhani kama atashinda]. Itakuwa ni jambo la kipumbavu kabisa kumpuuza. Toka alipotangaza nia wale wote waliompuuza imewatokea puani.

Kuhusu kauli zake tata hususan hiyo unayosema ya "kupiga marufuku waislam kuingia Marekani", kwanza, si sahihi. Trump hajasema anataka kupiga marufuku Waislam kuingia Marekani. Alichosema ni kwamba, wasitishe kwa muda kuruhusu wahamiaji na wakimbizi wanaotoka kwenye nchi za Kiislamu hadi hapo watakapokuja na njia iliyo bora zaidi ya kuwachunguza hao wahamiaji na wakimbizi.

Sasa kusitisha jambo kwa muda si sawa na kulipiga marufuku kabisa. Au wewe unaona ni kitu kilekile tu?

Pili, kuhusu kauli zake zingine za utata hususan kuhusu Afrika na Waafrika, hizo hazina ukweli wowote kwa maana ya kwamba hajawahi kuzitoa. Ni uzushi tu.

Kama ukiambiwa uelezee kitu kimoja ambacho Obama amefanikiwa kufanya katika urais wake, utataja kitu gani?

Labda kusimamia kuurudisha uchumi katika mstari baada ya mtikisiko wa 2008.

Kumekuwa na wimbi kubwa la waafrika huku Afrika waliojenga imani kuwa kuishi Marekani ni guarantee ya mafanikio. Je kuna ukweli katika hilo au ni imani potofu tu?

Ni imani potofu tu. Mafanikio hayaji tu hivi hivi. Mafanikio huwa ni matokeo ya fursa na uchapa kazi. Sasa, ukweli ni kwamba Marekani fursa zipo nyingi mno kulinganisha na Afrika. Lakini mtu usipochapa kazi huwezi kufanikiwa hata kidogo. Na uchapa kazi ni kanuni ambayo inatumika popote pale ulimwenguni.

Juzi tulipata taarifa kuwa kuna mtu ameingia kwenye club ya mashoga huko Orlando na kuua watu 49. Ni nini maoni yako juu ya ushoga?

Binafsi siupendi ushoga. Lakini pia naamini katika uhuru wa watu kufanya yale kitu roho inapenda ili mradi tu hawaingilii anga zangu. Hivyo, kama mtu ni shoga hayo ni mambo yake. Mimi hayanihusu. Kauli mbiu yangu ni 'fanya yako, ishi kivyako'. Mtu anajifanyia mambo yake kivyake, mimi inanihusu nini? Kwa nini nihemuke na mambo ya wengine? Tigo si zao? Sasa kama ni zao na wanapenda ziliwe, mimi inanihusu nini? Hainihusu.

Je ikitokea umekuwa Rais wa Tanzania, ni kitu gani kitakuwa kipaumbele chako?

Kwa jinsi changamoto zilivyo nyingi, sidhani kama nitakuwa na kipaumbele kimoja tu. Ila kilicho cha msingi zaidi ni utawala wa kisheria. Kwa hiyo nitaanza na hilo kwanza. Kuhakikisha nchi inatawaliwa kwa sheria na si vinginevyo.
 
OJ Simpson atakuwemo?
Naikumbuka hii kesi hasa namna ilivyovuta hisia za Weusi v/s Weupe. OJ alichomoka ila kuna Wachambuzi wanasema alishinda kwa sababu ya technicality ili isionekane Judges wamemuonea Mweusi kwa sababu aliyemuua ni Mzungu.

Mkuu hata mimi niliangalia kesi yake mwanzo mpaka mwisho, binafsi naona O.J ulihusika kwa mauuaji hayo ya kutisha, nawakili wake walijitahidi sana kumtetea hasa yule mswahili, kama Jaji hasingekuwa Mmarekani mwenye asili ya Japan kesi ile ingehamuliwa kivingine kabisa.
 
Lakini jaji hakuhusika na uamuzi wa hatia yake.

Kesi yake haikuwa bench trial.
 
Wanayoionyesha sasa ni marudio ya Part.1 iliyorushwa J'mosi iliyopita.

Part. 2 itakuja ikiisha hii encore presentation...9pm EST.
ESPN unacheki kupitia website au kingamuzi gan hapa bongo maana hii channel nilikuwa naingalia kupitia dstv wakaitoa
 
mimi nilisoma somewhere ili sikumbuki vizuri, hiyo movi sijaifuatilia

Niliona akifukuzana na Polisi kwenye Highway akiwa kwenye ki pickup chake, Polisi walimzingira wafakanikiwa kumtia mbaroni bila labsha - kama nakumbuka vizuri ali buruzwa mahakamani within a week!
 
Back
Top Bottom