kifo kinauma, hakifurahiwi na yeyote kiwe cha mtu mzuri au mbaya. hata Yesu alipoletewa taarifa ya kifo cha rafiki yake Lazaro, alilia machozi. Mungu awape faraja wafiwa wote na yeyote aliyeguswa na msiba huo.
Bisides that, kufa ni kitu kizuri kama utakufa mikononi mwa Mungu, ila ukifa nje ya mikono ya Mungu hakika ni hasara kubwa, kwasababu maisha yote umeishi duniani utakuwa umeyapoteza, hayakuwa na faida yeyote, kwasababu mwisho wako utakuwa moto wa jehanum milele na milele.
UFUNUO 14:13 INASEMA: Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
ukifa leo hii, matendo yako ambayo haujayatubia yatakufuata, utaenda nayo, wala usidanganywe na wanaohubiri kwamba watakuombea ukiwa maiti na Mungu atakusamehe, hao waongo. baada ya kifo ni hukumu, tengeneza mambo yako na Mungu kabla haujafa.
KWA JINA LA YESU KRISTO, ninawaasa wote mnaosoma hapa, andaeni maisha yenu ya baadaye, baada ya kifo chenu, kifo kinachokuja ghafla au hat akama sio ghafla, no one knows the exactly date that you would die. WHERE WILL YOU SPEND YOUR ETERNITY? kuna maisha ya baadaye ambayo ni maisha ya milele, eidha milele motoni au milele uzimani, uamuzi ni wako sasa kumpa Yesu Kristo maisha yako sasa ukiwa hai, Mungu ameweka mbele yako uzima na mauti, uchaguzi ni wako. nakushauri chagua uzima kwa kuokoka leo, ama la, utadondokea kwenye mauti ya mielele.
hizi ni siku za mwisho. Biblia ilitabiri kwamba INJILI lazima ihubiriwe ulimwenguni kote hapo ndipo ule mwisho utakuja, wengi huwa wanasema mbona tangu enzi wanasema mwisho na hauji, ndugu, kama mwenye nyumba angeliijua saa mwizi angekuja, angelikesha. kwa sasa, hata wewe msomaji ni shahidi, mtu akitaja neno KUOKOKA hakuna asiyelijua hapa Tanzania, unaelewa kabisa nini maana ya kuokoka, ila unashupaza tu shingo yako. pia, dunia imekuwa kijiji, youtube, facebook, whatsapp, tittwer x etc vinafika kila mahali na humo injili imepenetrate, hivyo kwa kutumia internet injili imefika kila mahala, khata north korea wanakosema wamefungiwa ndani ya nchi, injili ipo, manake wanawaona watu wanaofungwa kwa kushika tu Biblia, na wanajua kushika Biblia ni kosa kwa sheria zao, kumbe wanajua Neno la Mungu lipo, hukumu ya Mungu itakapokuja hapatakuwa na mtu wa kujitetea kwamba hakusikia injili hizi hizi mnazozisikia na kuzidharau na kuzitukana na kutuita tumechanganyikiwa. Mungu akusaidie, amua leo, jiunge na wokovu na watu waliookoka, nawe utapata uzima wa milele. Mungu akusaidieni.