Obama alikua na Juris Doctor (JD) sawa na PhD ila hakupenda kutumia Dr

Obama alikua na Juris Doctor (JD) sawa na PhD ila hakupenda kutumia Dr

Hazina tija hizo kuna watu huwezi kujua na tulikuqa tunakula nao mnel😀😀😀
Sifa za maskini kuitana itana.
Niliwahi fanya kazi na Jamaa mmoja from Ireland aisee
1.PhD in Neurosciences
2.Masters in Comp.Sciences(Cyber)
3.Masters in pyschology(Human)

Yule Bwana mtulivu sana,anajua vitu sijawahi ona😀😀😀
 
Tanganyika mnapambana na Udocta wa kupewa huku Obama hakutaka kabisa kuItwa Dr
In principle, nakubaliana na hoja yako, lakini siyo sahihi kusema JD ni sawa na PhD. JD ni American professional degree in law ambayo inahitajika na kila mtu anayetaka kujikita kwenye legal practice. Mawakili wote wa Marekani wana JD. Hata hivyo, JD haimpi mtu hadhi ya kuitwa Doctor so and so! Ukiwa kwenye academia unaweza kusoma LLM na PhD baada ya kupata JD.
 
Tanganyika mnapambana na Udocta wa kupewa huku Obama hakutaka kabisa kuItwa Dr
Obama hana shahada inayolingana na PhD.

Ana JD. Hiyo ni Juris Doctor. Ni professional degree.

Kila wakili Marekani ana JD. Hata mawakili wanajishighulisha na traffic offenses wana JD.

Shahada ya sheria ndivyo inavyoitwa hivyo huko Marekani.

PhD ni research degree. Kwa Marekani, shahada ya sheria yenye hadhi ya PhD ni JSD [Doctor of Juridical Science] au SJD [Doctor of Science of Law].

Obama hawezi kujiita wala kuitwa dokta [wa kitaaluma] maana hana shahada hiyo kitaaluma.

Acheni kupotosha. Obama hana PhD ya sheria. Ana shahada ya kawaida tu ya sheria kama walivyo mawakili wengine wote Marekani.
 
In principle, nakubaliana na hoja yako, lakini siyo sahihi kusema JD ni sawa na PhD. JD ni American professional degree in law ambayo inahitajika na kila mtu anayetaka kujikita kwenye legal practice. Mawakili wote wa Marekani wana JD. Hata hivyo, JD haimpi mtu hadhi ya kuitwa Doctor so and so! Ukiwa kwenye academia unaweza kusoma LLM na PhD baada ya kupata JD.
Equivalent ya PhD kwenye sheria [nchini Marekani] ni JSD.

Tatizo wabongo wakishaona neno doctor tu basi, wao wanahitimisha ni PhD.

Marekani kwa sasa kila wakili ana JD. Hata wale wanaojishughulisha na kesi za ajali za barabarani.
 
Back
Top Bottom