Sidhani kama ulikuwa unamfahamu vyema Gaga. Anaweza asicheze hayo mazoezi ila akija kwenye mechi Kocha atamzingatia sana, na baadae kumpa namba kisha ataperfom vizuri pengine kuliko waliohudhuria mazoezi vyema.
Hata nikirejea kwenye suala la unywaji pombe ambao umekiri jamaa alikuwa anakunywa vilivyo. Kwa hali ya kawaida si tungetegemea Hamis Thobias Gagarino awe na kiwango cha hovyo? Ila haikuwa hivyo. Na hata alipokosa mazoezi haikuwa hivyo pia.
Mimi Gaga simfahanu juu juu, Gaga alikua mshikaji mkubwa wa Morgan(Mogela) wakati Mogela anatoka Tumbaku kwenda Simba yeye Morgan ndio alimvuta pale Msimbazi.
Wakati uo Gaga alikua na kesi Mbaya pale Moro, Wadau wa Simba wakapambana kumaliza Ile kesi akaenda Simba ila Dirisha la usajili hakuliwahi.
Simba wakamfanyia mipango akawa anacheza pale prisner Ligi Daraja la pili akisubiri msimu unao fuata asajiliwe Simba.
Msimu unao fuata Prisner ikawa imepanda Ligi Daraja la kwanza(Ligi kuu) Wakagoma kumwachia na Simba waka msainisha akafungiwa mwaka mmoja kwa Double Signing.
Msimu wa 1986/87 adhabu ikaisha aka sign Simba, kakipiga baadae akaondoka yeye Gaga, mshikaji wake Morgan, Lila Shomari na Kipa nimemsahau jina wakaenda Kenya
(Volkano).
Waka Zima Volkano baadae Gaga akarudi Bongo akawa anazima pale Ndovu ya Arusha.
Morgani alipotoka Kenya akarudi Simba, akamshawishi Gaga naye akarudi Simba akitokea Ndovu ya Arusha.
Baadae pale Simba ukatokea mgogoro wa ki uongozi wakaondoka Simba Gaga na Mogela(Morgan) wakaenda Yanga.
Walitwaa Ubingwa wa Afrika mashariki na kati mwaka 1993 wakiwa na Yanga.
Baadae Gaga alistaafu soka.
Gaga alikua anafanya sana Mazoezi shida yake ilikua Mitungi tu.
Gaga namfahamu vizuri japo Mimi si mshabiki wa Simba