figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo , mgombea huyo amepinga matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayoonyesha kuwa Kenyatta anaongoza wakiwa wametofautiana kwa kura zaidi ya milioni 1.3.
"Tunayakataa matokeo haya yaliyofikia sasa kwa kuwa siyo sahihi, ni mashine iliyopiga kura hizi na siyo wananchi wa Kenya", amesema Odinga.
--------------
More updates..
Raila Asema NASA imeshinda kwa kura 8.1m, Jubilee 7.2
Mgombea urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati.
Bwana Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.
Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.
Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu". Na kwa hesabu zao kutokana na fomu za 34A, NASA imeshinda kwa kura 8.1m dhidi ya 7.2m za Jubilee kwenye upande wa Urais.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu.
Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua.
Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea.