Odinga apinga matokeo, adai ni matokeo ya mashine sio Wakenya

Odinga apinga matokeo, adai ni matokeo ya mashine sio Wakenya

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo , mgombea huyo amepinga matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayoonyesha kuwa Kenyatta anaongoza wakiwa wametofautiana kwa kura zaidi ya milioni 1.3.

"Tunayakataa matokeo haya yaliyofikia sasa kwa kuwa siyo sahihi, ni mashine iliyopiga kura hizi na siyo wananchi wa Kenya", amesema Odinga.
--------------

More updates..

Raila Asema NASA imeshinda kwa kura 8.1m, Jubilee 7.2

Mgombea urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati.

Bwana Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.

Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.

Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.

Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu". Na kwa hesabu zao kutokana na fomu za 34A, NASA imeshinda kwa kura 8.1m dhidi ya 7.2m za Jubilee kwenye upande wa Urais.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu.

Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua.

Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea.

20638779_1548554241854655_8803509652641900114_n.jpg
 
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo , mgombea huyo amepinga matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayoonyesha kuwa Kenyatta anaongoza wakiwa wametofautiana kwa kura zaidi ya milioni 1.3.

"Tunayakataa matokeo haya yaliyofikia sasa kwa kuwa siyo sahihi, ni mashine iliyopiga kura hizi na siyo wananchi wa Kenya", amesema Odinga.
Angeongoza yeye angekubali akafee mbele uchwara mwingine
 
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo , mgombea huyo amepinga matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayoonyesha kuwa Kenyatta anaongoza wakiwa wametofautiana kwa kura zaidi ya milioni 1.3.

"Tunayakataa matokeo haya yaliyofikia sasa kwa kuwa siyo sahihi, ni mashine iliyopiga kura hizi na siyo wananchi wa Kenya", amesema Odinga.
Kutawaka moto kama ni ukweli wacha tuone
 
ni lini Odinga aligombea Uraisi akakumbali kushindwa..yeye lazima alete chokochoko....najiuliza wao wamejuaje Jubilee wamehack IEBC...Raila s a dying horse
Yakitokea machafuko, watakaoumia ni wananchi wa kawaida wa Kenya huku wanasiasa wakikimbia nchi na kwenda kula bata huko ughaibuni.

Chonde chonde wananchi wa Kenya kuweni makini na wanasiasa. Anayeshindwa ni lazima akubali kushindwa. Kama hataki kukubali wananchi mlazimisheni akubali kwa kutumia njia yoyote ile hata kama ni kum_delete kabla maamuzi yake hayaja_delete wananchi wengi wasio na hatia.
 
Hii issue ilikuwa wazi, Odinga atashinda ila figisufigisu za IEBC na KERU wametengeneza genge lao la kuibia kura hadi wakamtoa roho Mr. Msando.

Any way, I am already packed everything to come in Kenya for a diplomatic mediation.
Don't worry guys you just fight.
 
toka auliwe yule mtaalamu wa hizo mashine itakuwa ni upuuzi kutokuwa na hofu!
 
Enda kwa wafuasi wa Nasa uwaambie hayo. Enda Kisumu uwaambie, sawa?

Kuanzia Kampeni mpaka uchaguzi uliendeshwa vizuri sana.Wapinzani walijimwaga na kutoa sera zao kwa uhuru kuliko nchi yoyote kusini mwa Jangwa la sahara ukitoa South Africa.
Hilo ni ushahidi tosha kwamba Uhuru ni mwanademokrasia na matokeo haya aliyastahili.
Odinga akubali matokeo ili aendeleze sifa nzuri ya Kenya kimataifa.
 
Siku hizi kupiga kura huwa haina shida. Kampeni kila mtu amefanya kwa Amani. lakini transmission of results ndio Muhimu. Form 34 A isipotoka sioni vile kutakalika sehemu kama Kisumu. Saa hii wanangoja Baba atoe order Kisha utanielewa
 
Akae pembeni,hawezi kushinda raila..!unazani wakenya ni mapunda kama watz!aende akatulie chato kwa swaiba wake.
 
Back
Top Bottom