OFFICIAL THREAD: UEFA™ Champions League Competition Analysis And Statistics

Bufon siyo katika penalty nadhani Navas nimzuri sana kwenye matuta Ila kwa kuwa watu wengi wanampa Juve nafasi naona kama Madrid anaweka Historia tena
 
Mkuu, unasema Madrid apige penetration pass? Barca alichemka hapo kwa hiyo style, tena Barca akiwa na manguli wa kudribble akina Messi na Neymar na hawakufua dafu.

Njia pekee ya kumuokoa Madrid ni Counter, PERIOD. Labda yatokee makosa madogo madogo ya hapa na pale yatakayofanywa na Juve ila sio kwa kupiga pass za kupenyeza. Hata hizo Counter sio mipira ya juu.

ACHANA NA VILE VIUMBE MKUU.

Juventus wangekuwa na mtu kama Lewandoski au Vidal hii Game wala tusingesubiri dakika 90 kujua nani anabeba kombe.

Sioni Madrid akipata goli kwa namna yoyote mbele ya Juventus, wale watu wanajua ni nini wanachokifanya uwanjani hususani linapokuja suala la kukaba.
 
Eti mjinga mjinga kama Benzema anaenda kukaa na akina Bonuchi, Chiellin, Barzaghi n.k Aiseee hakuna Striker nnayemdharau duniani kama Benzema.
 
Hiyo umesema wewe kuwa hajui kupiga pasi ....kama hajui kupiga pasi angekuwepo pale Madrid..??..... Ungeniambia ni mtu wa fouls sana ningekuelewa. [HASHTAG]#forzajuve[/HASHTAG]
Embu tuliza munkari kijana, Casemiro na mambo ya upigaji pasi wapi na wapi?

Yupo pale kwa kusudi moja tu, KUKABA, PERIOD. Na ni kweli jule jamaa anajua kukaba, anakaba kweli kweli ila tu usimpangie amkabe Messi maana utamkataa Casemiro.
 
Sijui ni mimi tu, lakini fainali hii ya mwaka huu imekuwa na msisimuko wa aina yake, naifananisha na ile ya mwaka 2008 Man Utd vs Chelsea.

All in all, atakayekuwa kuwa mjanja wa kumsoma mwenzake vizuri ndiye atakaye shinda.
Hakuna ambae mpaka sasa hajamsoma mwenzie, hivi Zidane haijui Juventus? Akina Khedira, Dani Alves, Buffon hawaijui Madrid?

Mimi naona Madrid anahitaji mbeleko kupata Goli mbele ya Juve, hii beki imenikumbusha Inter Millan ya Jose Mourinho ila hii imezidi sasa ya Juventus.
 
Naona watu wengi wanaona kama hii ni changamoto kubwa kwa Madrid, ni kweli madrid amekuwa mbovu kidogo kwenye defence lakini huwa sio kwa game kama hizi.....hata ukiangalia tu kwa mbali utaona kwamba game hii ina maana kubwa sana kwa Madrid kuliko Juve kwa sababu tu anataka kuandika Historia nyingi zaidi hasa kwa wachezaji binafsi, kocha hata team kwa ujumla. Hivyo basi tutegemee Madrid kucheza mpira wa kushambulia sana chini ya dakika 30 za kipindi cha mwanzo kitu kitakachowapelekea juve kujihami sana na hata kujikuta wakifungwa goli la mapema. Achana na yote mpira ni dakika 90 lolote laweza kutokea! Lakini karata yangu nimeilekezea kwa Madrid
 

Hata mie Naona kabisa...Ndoo lazima iende Spain pale bernabeu hiyo mkuu,Hamna namna...Kwamza kiushambuliaji Juve ni timu ya kawaida Sanaaa...wanachoringia ni ile defence yao tu,NA SIKUZOTE WATAALAM WANASEMA "THE BEST WAY TO DEFEND YOURSELF...IS TO DO ATTACK"....Kwa philosophy hiyo Juve anaweza poteza Huo Mchezo japo sio kirahisi rahisi.
 
Hii ngoma extra time ...

Yani ata mie naona hii ngoma itakuwa siyo ya kitoto...ulichokisema kinaweza kutokea...MAANA REAL AKICHARUKA KUSHAMBULIA JUVE HAPANDI KWENYE HALF YETU YULE LABDA AFUNGWE NDO ITAMLAZIMU KUFUNGUKA...LAKINI KAMA HATOFUNGWA ATAKAZA HADI Dakika 90 ZA MCHEZO ZIISHE.
 

Jamaa zako hawa mkuu...MABEKI HATARI DUNIANI YANI WANA ULE UKABAJI WAKUSINDIKIZA....HUWA WANAHAKIKISHA MPIRA HADI UMETOKA KABISA NA HAUPO ENEO LA GOLI LAO.

 
Eti mjinga mjinga kama Benzema anaenda kukaa na akina Bonuchi, Chiellin, Barzaghi n.k Aiseee hakuna Striker nnayemdharau duniani kama Benzema.

Huyo barzaghli ndo nuksi mkuu,yule kocha wao Juve Allegri alisema baada ya kufanya Sub ya barzaghli kuingia kipindi cha pili...kwenye match yao ya 2nd Leg against Barca...ALIJUA WAZI ATA WANGEINGIZWA WAKINA MESSI SITA KUTOKEA BENCHI WASINGESHINDA ILE MATCH...Nilichekaga sana, Dah!...yani Juve kwenye Defence sio wakisport sport kabisa asee.
 

Lakini hutoamini mkuu REAL Atabeba hili Taji lake la 12...Juve watafungika tu...mie nachowafahamu Madrid kwenye games kubwa kama hizi huwa hawanaga upuuzi hata punje, ILISEMEKANA JUVE NI MFUPA ULIOMSHINDA FISI(BARCELONA)...JE MBWA(MONACO) ANGEUWEZA???...Lakini Huo msemo yule Mbappe akaufutilia mbali na kumfunga Buffon goli dakika ya 69...Wakati watu wazima BARCA mlishindwa kupata goli ata la kusingiziwa kwa DAKIKA 180!
...Hivyo kwa kilichowakuta nyie BARCA Sidhani kama ndicho kitakachomkuta REAL...Me nachojua mpira hubadilika mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…