OFFICIAL THREAD: UEFA™ Champions League Competition Analysis And Statistics

OFFICIAL THREAD: UEFA™ Champions League Competition Analysis And Statistics

* HISTORIA FUPI YA MICHUANO HII

View attachment 517694
Ni michuano ya soccer liyoanzishwa na mashirikisho ya mpira ya nchi wanachama barani ulaya(Union Of European Football Assocciations) miaka ya 1955 ikijulikana kama EUROPEAN COMPETITION CLUB'S CUP...hadi kufikia mwaka 1992 ambapo kombe lililokuwa likitolewa kwa mshindi wa michuano hiyo lilifanyiwa mabadiliko ya kimuundo(rebranded)...hii ilipelekea jina la michuano hiyo kubadilika na kuitwa UEFA CHAMPIONS LIGUE(LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA)...Hapo chini ni picha ya kombe ambalo lililokuwa likitolewa baada ya kufanyiwa mabadiliko anzia mwaka 1992 hadi Sasa...

View attachment 517706

*ZAWADI KWA WASHIRIKI
Katika michuano hii kila timu inayoshiriki hupata kitita cha pesa katika kila hatua ya ushiriki kama ilivyo hapo...
  • First qualifying round: €220,000
  • Second qualifying round: €320,000
  • Losers third qualifying round: €420,000
  • Losers play-off round: €3,000,000
  • Winners play-off round: €2,000,000
  • Base fee for group stage: €12,700,000
  • Group match victory: €1,500,000
  • Group match draw: €500,000
  • Round of 16: €6,000,000
  • Quarter-finals: €6,500,000
  • Semi-finals: €7,500,000
  • Losing finalist: €11,000,000
  • Winning the Final: €15,500,000
. Hiyo inamaana timu itakayoibuka kinara kwenye hatua zote hizo za michuano bila kupoteza itajinyakulia kitita cha €57,200,000.


* TIMU ZILIZOSHINDA TAJI HILO
Tokea kuanzishwa kwake michuano hiyo...Timu inayoongoza kutwaa taji hilo ni Real Madrid ikifuatiwa na nyingine kama ilivyo hapo...


FOOTBALL CLUBS THAT WON THE TITTLE

Real Madrid Imechukua Mara 11...Imepoteza Mara 3.
Milan Imechukua Mara 7...Imepoteza Mara 4
Bayern Munich Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 5
Barcelona Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 3
Liverpool Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 2
Ajax Imechukua Mara 4...Imepoteza Mara 2
Internazionale Imechukua mara 3...Imepoteza Mara 2
Manchester United Imechukua Mara 3...Imepoteza Mara 2
Juventus Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 6
Benfica Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 5
Nottingham Forest Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 0
Porto Imechukua mara 2...Imepoteza Mara 0


*WIMBO WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Bila ubishi huu ni wimbo unaokonga sana Nyoyo za mashabiki Wengi wa soccer duniani,ulitungwa na mwanamuziki Mwingereza mwenye taaluma hiyo ya muziki anaitwa TONY BRITTEN mwaka 1992...mara tu baada ya mabadiliko ya kombe hilo kufanyika, Wimbo huo umetungwa kwa kutumia luga Tatu tofauti kwa pamoja zinazotumiwa rasmi na shirikisho la soka barani ulaya(UEFA) ambazo ni Kijerumani, Kifaransa na Kiingereza na maana yake in English ni kama ilivyo hapo chini...

Original song...
Champions League Theme

Ce sont les meilleures équipes
Es sind die allerbesten Mannschaften
The main event

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions

Une grande réunion
Eine große sportliche Veranstaltung
The main event

Ils sont les meilleurs
Sie sind die Besten
These are the champions

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions


In English translation...
Champions league Anthem

They are the best teams
They are the best teams
The Main Event

The master
The best
Great teams
The Champions

A big meeting
A great sporting event
The Main Event

They are the best
They are the best
These are the champions

The master
The best
Great teams
The Champions

The master
The best
The Champions


#Mnaweza kuusikiliza Huo wimbo wote...Full version hapo...




*UPCOMING UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINAL On 3rd June Of 2017 in CARDIFF



Ni Fainali ya 59 ya michuano hiyo barani ulaya, Ikiwakutanisha JUVENTUS(Mabingwa Wa Serie-A 2016/2017) Vs REAL MADRID(Mabingwa Wa LaLiga-Santander 2016/2017) itakayofanyika CARDIFF...tarehe 3 june.

View attachment 517759
View attachment 517760
View attachment 517764
View attachment 517765


#Mambo muhimu kwenye fainali hii...ambayo inahitajika kuyajua.
-Juve amefika Fainali za UEFA Mara 8...ameshinda 2 na kupoteza 6(Mara nyingi zaidi ya Madrid).
-Real amefika fainali Mara 14...ameshinda 11...na kupoteza 3(Mara chache zaidi ya Juve).

-Real Madrid inahitaji kuandika historia mpya kwenye michuano hiyo...kuwa ndiyo timu pekee barani ulaya kuchukua Taji hilo mara mbili mfululizo kama bingwa mtetezi.
-Pia Real Madrid inataka kuandika historia ya kuchukua mataji mawili yani LaLiga na UEFA Katika msimu mmoja...baada ya miaka 59 tokea msimu wa 1957/1958.

-Goli kipa Wa Juve ameruhusu magoli matatu tu kuingia wavuni tokea waanze michuano hii ya UEFA msimu huu.​
-Juve wameweza kutoka na Clean sheet 9(Hajafungwa goli ata moja kwenye mechi tisa za UEFA) katika mechi 12 za UEFA walizocheza msimu huu.
-Zidane anataka kuweka record ya kuwa kocha pekee barani ulaya aliyeweza kutetea taji lake la UEFA Champions League.
-Juve wameruhusu magoli 27 tu kwenye mechi zote za ligi walizocheza huku Madrid wameruhusu Magoli 41 kwenye mechi zote za Ligi walizocheza.
-Gianluigi Buffon anaelekea kustaafu Mpira kutokana na Umri wake...hivyo hii ni nafasi adhimu sana kwake kuchukua taji hili muhimu akiwa na Juve.
-Dani Alves anahitaji kuandika historia ya kuchukua Taji la UEFA na Juve katika msimu wake Wa kwanza.
-Cristiano Ronaldo anahitaji ashinde taji hili ili afikie record ya Mpinzani wake Wa soka(Messi) Ya kutwaa mataji manne ya UCL.

*ANALYSIS

#JUVENTUS FC
Juventus wanatarajiwa kutumia mfumo wa "4-2-3-1" au "3-4-2-1"...Juve hawatacheza mchezo Wa kushambulia muda wote Bali watatumia mashambulizi ya Counter dhidi ya Madrid,kwa mfumo Huo wa "4-2-3-1" utakaotumia Juve utamruhusu Higuain pekee kucheza mbele kama Forward huku Dyabala na mandzukich wakipandisha mipira kwa kujiami na wengine wakibaki nyuma Kwa tension ya kuzuia, Juve anajua wazi Madrid atashambulia sana kutafuta goli la mapema ili aweze kuumiliki mchezo na kujihamini...hivyo kipindi cha kwanza Juve hatoshambulia sana atajitahidi kulinda goli lisiingie ila kipindi cha pili atajaribu kushambulia kiasi akiona Madrid kacharuka sana atarudi kucheza kama first-half....na itakuwa bora sana kwa Juve kwenda Hadi extra-time ikiwezekana ata penalties wakijua Kipa wakueleweka wanaye kuliko kuruhusu goli dakika 90 za mchezo...na ikitokea wamefungwa mapema itawalazimu wafunguke ili wasawazishe...na hapa kuna mawili wanaweza wakafanikiwa ama wakaongezwa magoli.

#REAL MADRID C.F
Madrid wanatarajiwa kutumia mfumo Wa "4-3-1-2" au "4-3-3"...Madrid wanafahamu vyema ubora Wa defence ya Juve hivyo basi watahitaji goli la mapema ili waweze kuutawala mchezo...ukizingatia watakuwa na Full-backs wao wote wakupandisha mipira(Marcelo & Carvajal) ila watategemea sana mipira ya kupenyeza(penetrations) ili kuitoboa ngome ya Juve.

Note: Ifahamike mbali na uchambuzi Huo...Mpira ni dakika 90,na kuna ushindi wa magoli ya faulo na penalty pia...hivyo lolote litaweza kutokea mchezoni.​


Update nyingine tutaendelea kupeana Wadau...tukiwa tunausubiri huu [HASHTAG]#MTANANGE[/HASHTAG]!​

Bufon siyo katika penalty nadhani Navas nimzuri sana kwenye matuta Ila kwa kuwa watu wengi wanampa Juve nafasi naona kama Madrid anaweka Historia tena
 
Mkuu, unasema Madrid apige penetration pass? Barca alichemka hapo kwa hiyo style, tena Barca akiwa na manguli wa kudribble akina Messi na Neymar na hawakufua dafu.

Njia pekee ya kumuokoa Madrid ni Counter, PERIOD. Labda yatokee makosa madogo madogo ya hapa na pale yatakayofanywa na Juve ila sio kwa kupiga pass za kupenyeza. Hata hizo Counter sio mipira ya juu.

ACHANA NA VILE VIUMBE MKUU.

Juventus wangekuwa na mtu kama Lewandoski au Vidal hii Game wala tusingesubiri dakika 90 kujua nani anabeba kombe.

Sioni Madrid akipata goli kwa namna yoyote mbele ya Juventus, wale watu wanajua ni nini wanachokifanya uwanjani hususani linapokuja suala la kukaba.
 
Eti mjinga mjinga kama Benzema anaenda kukaa na akina Bonuchi, Chiellin, Barzaghi n.k Aiseee hakuna Striker nnayemdharau duniani kama Benzema.
 
Hiyo umesema wewe kuwa hajui kupiga pasi ....kama hajui kupiga pasi angekuwepo pale Madrid..??..... Ungeniambia ni mtu wa fouls sana ningekuelewa. [HASHTAG]#forzajuve[/HASHTAG]
Embu tuliza munkari kijana, Casemiro na mambo ya upigaji pasi wapi na wapi?

Yupo pale kwa kusudi moja tu, KUKABA, PERIOD. Na ni kweli jule jamaa anajua kukaba, anakaba kweli kweli ila tu usimpangie amkabe Messi maana utamkataa Casemiro.
 
Sijui ni mimi tu, lakini fainali hii ya mwaka huu imekuwa na msisimuko wa aina yake, naifananisha na ile ya mwaka 2008 Man Utd vs Chelsea.

All in all, atakayekuwa kuwa mjanja wa kumsoma mwenzake vizuri ndiye atakaye shinda.
Hakuna ambae mpaka sasa hajamsoma mwenzie, hivi Zidane haijui Juventus? Akina Khedira, Dani Alves, Buffon hawaijui Madrid?

Mimi naona Madrid anahitaji mbeleko kupata Goli mbele ya Juve, hii beki imenikumbusha Inter Millan ya Jose Mourinho ila hii imezidi sasa ya Juventus.
 
Naona watu wengi wanaona kama hii ni changamoto kubwa kwa Madrid, ni kweli madrid amekuwa mbovu kidogo kwenye defence lakini huwa sio kwa game kama hizi.....hata ukiangalia tu kwa mbali utaona kwamba game hii ina maana kubwa sana kwa Madrid kuliko Juve kwa sababu tu anataka kuandika Historia nyingi zaidi hasa kwa wachezaji binafsi, kocha hata team kwa ujumla. Hivyo basi tutegemee Madrid kucheza mpira wa kushambulia sana chini ya dakika 30 za kipindi cha mwanzo kitu kitakachowapelekea juve kujihami sana na hata kujikuta wakifungwa goli la mapema. Achana na yote mpira ni dakika 90 lolote laweza kutokea! Lakini karata yangu nimeilekezea kwa Madrid
 
Naona watu wengi wanaona kama hii ni changamoto kubwa kwa Madrid, ni kweli madrid amekuwa mbovu kidogo kwenye defence lakini huwa sio kwa game kama hizi.....hata ukiangalia tu kwa mbali utaona kwamba game hii ina maana kubwa sana kwa Madrid kuliko Juve kwa sababu tu anataka kuandika Historia nyingi zaidi hasa kwa wachezaji binafsi, kocha hata team kwa ujumla. Hivyo basi tutegemee Madrid kucheza mpira wa kushambulia sana chini ya dakika 30 za kipindi cha mwanzo kitu kitakachowapelekea juve kujihami sana na hata kujikuta wakifungwa goli la mapema. Achana na yote mpira ni dakika 90 lolote laweza kutokea! Lakini karata yangu nimeilekezea kwa Madrid

Hata mie Naona kabisa...Ndoo lazima iende Spain pale bernabeu hiyo mkuu,Hamna namna...Kwamza kiushambuliaji Juve ni timu ya kawaida Sanaaa...wanachoringia ni ile defence yao tu,NA SIKUZOTE WATAALAM WANASEMA "THE BEST WAY TO DEFEND YOURSELF...IS TO DO ATTACK"....Kwa philosophy hiyo Juve anaweza poteza Huo Mchezo japo sio kirahisi rahisi.
 
Hii ngoma extra time ...

Yani ata mie naona hii ngoma itakuwa siyo ya kitoto...ulichokisema kinaweza kutokea...MAANA REAL AKICHARUKA KUSHAMBULIA JUVE HAPANDI KWENYE HALF YETU YULE LABDA AFUNGWE NDO ITAMLAZIMU KUFUNGUKA...LAKINI KAMA HATOFUNGWA ATAKAZA HADI Dakika 90 ZA MCHEZO ZIISHE.
 
Hakuna ambae mpaka sasa hajamsoma mwenzie, hivi Zidane haijui Juventus? Akina Khedira, Dani Alves, Buffon hawaijui Madrid?

Mimi naona Madrid anahitaji mbeleko kupata Goli mbele ya Juve, hii beki imenikumbusha Inter Millan ya Jose Mourinho ila hii imezidi sasa ya Juventus.

Jamaa zako hawa mkuu...MABEKI HATARI DUNIANI YANI WANA ULE UKABAJI WAKUSINDIKIZA....HUWA WANAHAKIKISHA MPIRA HADI UMETOKA KABISA NA HAUPO ENEO LA GOLI LAO.

skysports-juventus-giorgio-chiellini_3940925 (1).jpg
 
Eti mjinga mjinga kama Benzema anaenda kukaa na akina Bonuchi, Chiellin, Barzaghi n.k Aiseee hakuna Striker nnayemdharau duniani kama Benzema.

Huyo barzaghli ndo nuksi mkuu,yule kocha wao Juve Allegri alisema baada ya kufanya Sub ya barzaghli kuingia kipindi cha pili...kwenye match yao ya 2nd Leg against Barca...ALIJUA WAZI ATA WANGEINGIZWA WAKINA MESSI SITA KUTOKEA BENCHI WASINGESHINDA ILE MATCH...Nilichekaga sana, Dah!...yani Juve kwenye Defence sio wakisport sport kabisa asee.
 
Mkuu, unasema Madrid apige penetration pass? Barca alichemka hapo kwa hiyo style, tena Barca akiwa na manguli wa kudribble akina Messi na Neymar na hawakufua dafu.

Njia pekee ya kumuokoa Madrid ni Counter, PERIOD. Labda yatokee makosa madogo madogo ya hapa na pale yatakayofanywa na Juve ila sio kwa kupiga pass za kupenyeza. Hata hizo Counter sio mipira ya juu.

ACHANA NA VILE VIUMBE MKUU.

Juventus wangekuwa na mtu kama Lewandoski au Vidal hii Game wala tusingesubiri dakika 90 kujua nani anabeba kombe.

Sioni Madrid akipata goli kwa namna yoyote mbele ya Juventus, wale watu wanajua ni nini wanachokifanya uwanjani hususani linapokuja suala la kukaba.

Lakini hutoamini mkuu REAL Atabeba hili Taji lake la 12...Juve watafungika tu...mie nachowafahamu Madrid kwenye games kubwa kama hizi huwa hawanaga upuuzi hata punje, ILISEMEKANA JUVE NI MFUPA ULIOMSHINDA FISI(BARCELONA)...JE MBWA(MONACO) ANGEUWEZA???...Lakini Huo msemo yule Mbappe akaufutilia mbali na kumfunga Buffon goli dakika ya 69...Wakati watu wazima BARCA mlishindwa kupata goli ata la kusingiziwa kwa DAKIKA 180!
...Hivyo kwa kilichowakuta nyie BARCA Sidhani kama ndicho kitakachomkuta REAL...Me nachojua mpira hubadilika mkuu.
 
Back
Top Bottom