Official Video: Nagharamia - Pongezi kwa Ali Kiba

sumbai

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
19,955
Reaction score
45,207
Kwa wapenzi wa muziki, tukiweka figisu figisu pembeni.

Kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kumpa pongezi Ally Kiba kwani kwa kiasi fulani amajitahidi kujibu lawama kwa vitendo kwenye hii video.

Tofauti na matarajio ya wengi kwamba historia yake ingejirudia ya kutoa video ambazo kidogo zinakuwa hazipendwi saana, ila for this Kiba amejitahidi. Video kuendana na story, rangi nzuri, scene. Location, daah hongera Kiba.

Wengine huwa tunakuponda ili ujirekebishe na sio kukuangusha. We always need Kiba upige hatua kufikia uwezo wako.

 
Last edited by a moderator:
Hii nzuri unakuja kwa mbali na sisi ndo tunaka vitu kama hivyo good video
 
Atleast mkuuu,
Ila tunatofautiana..

Upo serious tufananishe hii video na video izi
Jux one more night
Ben pol ningefanyaje
Chegge sweety sweety
Ommy dimpoz achia body
Then hii video rangi yake mbaya bora chekeche cjui story ilikuwa haieleweki ila rangi ilikuwa amazing
 
Upo serious tufananishe hii video na video izi
Jux one more night
Ben pol ningefanyaje
Chegge sweety sweety
Ommy dimpoz achia body
Then hii video rangi yake mbaya bora chekeche cjui story ilikuwa haieleweki ila rangi ilikuwa amazing

Ni kweli rangi ya kwenye cheketua ilikuwa nzuri kuliko video zote. Ila alikosea ile location, wale queens, cheza yake na mavazi.

Ya leo kwenye rangi kidogo sio nzuri kama ile ya cheketua. Ila tofauti na mambo hayo mengineyo amejitahidi.

Nsingependa kuzifananisha na hizo ulizo zitaja.
 

Ha ha ha ha ha ha ha naona unakusanya kusanya vimchanga unabumba bumba unavichomekea na maua ili uite keki
 
Upo serious tufananishe hii video na video izi
Jux one more night
Ben pol ningefanyaje
Chegge sweety sweety
Ommy dimpoz achia body
Then hii video rangi yake mbaya bora chekeche cjui story ilikuwa haieleweki ila rangi ilikuwa amazing

team monds acheni chuki za kijinga, K 4 REAL hapa kamfunika mpaka huyo mpaka rangi wenu
 
Kuna tatizo la mapenzi na ukweli ila mwisho wa siku Kiba atajitahidi katika video wakati Dangote ashafanya. Diamond ni Messi wa muziki wa bongo
 
Hawakuheshimu mchezo wa golf, yaani wanacheza huku wanajibizana na kubrowse!

Tuacheni unafki, Diamond anajua kuigiza, hata humkubali kuna sehemu kwenye video yake itakufanya urudishe nyuma. 'My love boat' na Kcee video inafika mwishoni kuna namna anadance anachezesha mdomo kama anavibrate utapenda urudie. Video na inyaya "nakupenda" kuna sehemu anashake utaipenda.

"Utanipenda" kuna sehemu kakanyagiwa maji na Wolper alivyorespond utadhani ni kweli, Kwetu Mbagala bibi harusi anaolewa yeye anachugulia utadhani ni kweli.. Nana dem anaingia class macho ya Diamond yanagongana na ya dem halafu Diamond anaangalia chini yaani kitu ambacho kipo sana inatokea.....

Diamond nyimbo zake nzuri, video zinauhalisia anajua kuigiza utadhani kweli..

Alikiba ana sauti, ila video anazotoa hazina mvuto hata hii ya kawaida sana. Quality nzuri ila yanayoendelea mle hazina tofauti na video za zilipendwa
Hata kwa mtu asiyejua lugha akiangalia video za Diamond anajua kinachoendelea na story inahusu nini, inavutia.
 
Safi sana shemeji sumbai,ushabiki pembeni tunajadili issues namna hii.
Umenifurahisha kuliko tukuka,kudos.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikaucheki nije na maoni yangu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…