Doppelganger
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,858
- 757
Picha ya mtuhumiwa aliyejifanya Afisa usalama.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.
Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.
Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.
Tanzania Daima
Huyo sio feki ndugu kwani kuna maafisa usalama hadi vichaa tunao mitaani hapo Kova amebugi meen ua kuna siri imejificha nyuma ya pazia. Isije ikawa ni mbinu ambapo huyu anaweza kutimika kuwadhuru mahabusu wa kisiasa hususani CDM watakapowekwa rumande na lengo lao la kuwauwa liwe limetimia kabla ya 2015
Mimi najua kuliko unavyojua wewe na nafikiri umejibu haya kwa kuwa mnachokifanya mnafikiri watanzania wa Leo ndio wale wa miaka ya 1947 endelea na upuuzi wako ndugu,Wewe akili yako haiko sawa! Unaandika tu upuuzi humu! Serikali itauaje mahabusu? Na hao TISS machizi labda ni wewe mwenyewe nadhani kichwani hauko timamu. Mnaleta story za vijiweni humu JF wakati huna unalolijua kuhusu TISS. Shame on you!
Chanzo cha yote Haya inasemekana ni mgogoro wa kiwanja Huku Ukonga ambao ulipelekea kuibua Songombingo hatimae likatinga polisi na kuibua yote Haya tunayoyasikia sasa
Haki ya mungu i know the guy na hata mimi nilidhani ni usalama wa taifa. Huyo jamaa huwa yuko sana bandarini kuna jamaa anaitwa Alnuur mkurugenzi wa Spedarg maagent wa kuleta clinker twiga cement atakuwa amelizwa sana. Hata wakina Godfrey Nyange watakuwa wamelizwa sana. Nitafungua uzi kuwaelezea kiundani. Kweli dunia hadaa. Ukimwona anavyoulamba huwezi amini. Hadi madiwani wa temeke anakunywa nao pale PR STADIUM au zamani IMASCO
Mimi najua kuliko unavyojua wewe na nafikiri umejibu haya kwa kuwa mnachokifanya mnafikiri watanzania wa Leo ndio wale wa miaka ya 1947 endelea na upuuzi wako ndugu,
mabwaku......
Tabia hii mbaya tuiache ,tutafungwa na kuishia jela.
Vijana msiingie kwenye biashara hii mbaya ya utapeli.
Kova ni msanii sana zaidi ya makamanda wote waliokwisha pita hapa dar nilipewa taarifa na kamanda mmoja akaniambia jamaa huwa anachukua bastola na risasi anaziweka mezani na kuita media na kuanza kuwabambikizia watu makesi hayo ya kukutwa na bunduki...kama huyo jamaa uwenda amebambikizwa hana lolote kova alafu swala la usalama wa taifa fake ni la kawaida hapa dar hawa hawa usalama wataifa wanashirikiana na matapeli kupiga dili mjini na wako wengi sana na hiyo nikutokana na kiongozi wa usalama wa taifa ni fisadi sasa watoto nao awawezi kuwa mafisadi
Huyo ni fake angekuwa TISS original asingebuluzwa na kupigwa picha hadharani.
Kanasa, na hayo Makabulasha ni fake pia.
Wewe akili yako haiko sawa! Unaandika tu upuuzi humu! Serikali itauaje mahabusu? Na hao TISS machizi labda ni wewe mwenyewe nadhani kichwani hauko timamu. Mnaleta story za vijiweni humu JF wakati huna unalolijua kuhusu TISS. Shame on you!
Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa! Sawa bana wewe ni insider wa TISS UNAJUA ZAIDI. HEBU TUJUZE BASI, ULIWAONA WAPI VICHAA WA TISS?????? MANAKE UMESEMA TISS KUNA VICHAAA. NA HUO MPANGO WA KUUA MAHABUSU UMEUPATA WAPI??? HEBU THIBITISHA HAPA, KISHA TOA TAARIFA POLISI ILI WAHUSIKA WAKAMATWE!
Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa! Sawa bana wewe ni insider wa TISS UNAJUA ZAIDI. HEBU TUJUZE BASI, ULIWAONA WAPI VICHAA WA TISS?????? MANAKE UMESEMA TISS KUNA VICHAAA. NA HUO MPANGO WA KUUA MAHABUSU UMEUPATA WAPI??? HEBU THIBITISHA HAPA, KISHA TOA TAARIFA POLISI ILI WAHUSIKA WAKAMATWE!