Ofisa usalama 'feki' anaswa

Ofisa usalama 'feki' anaswa

Nchi yetu ya kijanjajanja sana...

yani kukiwa na jambo linalotikisa nchi kama la gas kusini,katiba mpya,madawa ya kulevya,ufisadi n.k basi serikali itawatafutia vijimambo vinginevyo na kuvikuza ili kuwapumbaza,kuwatoa katika msimamo na kuwasahaulisha yale madai muhimu.

Kina FEKI wako wengi maeneo mbalimbali ambapo waeza pata SAHIHI YA RAIS na mawaziri wake wote,cheti cha chuo chochote hadi kile cha Havard bongo unapata...

Serikali imeishiwa mbinu!!!
 
attachment.php

Picha ya mtuhumiwa aliyejifanya Afisa usalama.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.

Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.

Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.

Tanzania Daima

Watu kama hawa ni wengi sana, na baadhi yao huwa wanapeleka taarifa za uongo kwenye chama fulani hivi cha siasa, halafu viongozi wa chama hicho huitisha mkutano na waandishi wa habari na kuueleza uma kwamba wamepewa taarifa kutoka ndani ya TISS, hahahahahaaaaa! Shame. Wanaokoteza vitaarifa vya uongo halafu wana exaggerate ili kufanikisha lengo lao! Endeleeni kuwatumia matapeli wanaojifanya TISS. Kuvuja kwa pakacha.....
 
Huyo sio feki ndugu kwani kuna maafisa usalama hadi vichaa tunao mitaani hapo Kova amebugi meen ua kuna siri imejificha nyuma ya pazia. Isije ikawa ni mbinu ambapo huyu anaweza kutimika kuwadhuru mahabusu wa kisiasa hususani CDM watakapowekwa rumande na lengo lao la kuwauwa liwe limetimia kabla ya 2015

Wewe akili yako haiko sawa! Unaandika tu upuuzi humu! Serikali itauaje mahabusu? Na hao TISS machizi labda ni wewe mwenyewe nadhani kichwani hauko timamu. Mnaleta story za vijiweni humu JF wakati huna unalolijua kuhusu TISS. Shame on you!
 
Wanajamvi hivi mbona bado hakuna taarifa rasmi????

HIVI HUYU JAMAA NI AFISA USALAMA FEKI AU ORIJINO???

Je ni nini kinaendelea???

Amekamatwa au lah????
 
Wewe akili yako haiko sawa! Unaandika tu upuuzi humu! Serikali itauaje mahabusu? Na hao TISS machizi labda ni wewe mwenyewe nadhani kichwani hauko timamu. Mnaleta story za vijiweni humu JF wakati huna unalolijua kuhusu TISS. Shame on you!
Mimi najua kuliko unavyojua wewe na nafikiri umejibu haya kwa kuwa mnachokifanya mnafikiri watanzania wa Leo ndio wale wa miaka ya 1947 endelea na upuuzi wako ndugu,
 
Chanzo cha yote Haya inasemekana ni mgogoro wa kiwanja Huku Ukonga ambao ulipelekea kuibua Songombingo hatimae likatinga polisi na kuibua yote Haya tunayoyasikia sasa

hebu elezea vizuri mkuu ilikuwaje???
 
Haki ya mungu i know the guy na hata mimi nilidhani ni usalama wa taifa. Huyo jamaa huwa yuko sana bandarini kuna jamaa anaitwa Alnuur mkurugenzi wa Spedarg maagent wa kuleta clinker twiga cement atakuwa amelizwa sana. Hata wakina Godfrey Nyange watakuwa wamelizwa sana. Nitafungua uzi kuwaelezea kiundani. Kweli dunia hadaa. Ukimwona anavyoulamba huwezi amini. Hadi madiwani wa temeke anakunywa nao pale PR STADIUM au zamani IMASCO

he he he he he he he he mkuu fungua uzi utupie mambo tumfahamu vizuri sasa
 
Mimi najua kuliko unavyojua wewe na nafikiri umejibu haya kwa kuwa mnachokifanya mnafikiri watanzania wa Leo ndio wale wa miaka ya 1947 endelea na upuuzi wako ndugu,

Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa! Sawa bana wewe ni insider wa TISS UNAJUA ZAIDI. HEBU TUJUZE BASI, ULIWAONA WAPI VICHAA WA TISS?????? MANAKE UMESEMA TISS KUNA VICHAAA. NA HUO MPANGO WA KUUA MAHABUSU UMEUPATA WAPI??? HEBU THIBITISHA HAPA, KISHA TOA TAARIFA POLISI ILI WAHUSIKA WAKAMATWE!
 
Tunawahadaa ili ishu ya ponda tuseme ni askari feki haaha jiulizeni kwa nn haya yanatokea baada ya ponda kupigwa .....
 
Tabia hii mbaya tuiache ,tutafungwa na kuishia jela.
Vijana msiingie kwenye biashara hii mbaya ya utapeli.
 
Ingekuwa china...bastola hizo hizo zingetumia kutekeleza hukumu yake
 
Tabia hii mbaya tuiache ,tutafungwa na kuishia jela.
Vijana msiingie kwenye biashara hii mbaya ya utapeli.

Mkuu chuki unajua bado tupo njia panda. Je ni kweli au si kweli kuwa jamaa ni TISS?????
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chuki unajua bado tupo njia panda. Je ni kweli au si kweli kuwa jamaa ni TISS?????

Huyo ni fake angekuwa TISS original asingebuluzwa na kupigwa picha hadharani.
Kanasa, na hayo Makabulasha ni fake pia.
 
Kova ni msanii sana zaidi ya makamanda wote waliokwisha pita hapa dar nilipewa taarifa na kamanda mmoja akaniambia jamaa huwa anachukua bastola na risasi anaziweka mezani na kuita media na kuanza kuwabambikizia watu makesi hayo ya kukutwa na bunduki...kama huyo jamaa uwenda amebambikizwa hana lolote kova alafu swala la usalama wa taifa fake ni la kawaida hapa dar hawa hawa usalama wataifa wanashirikiana na matapeli kupiga dili mjini na wako wengi sana na hiyo nikutokana na kiongozi wa usalama wa taifa ni fisadi sasa watoto nao awawezi kuwa mafisadi

Tunaomba uthibitisho wa TUHUMA HIZI NZITO. HAZITAPUUZWA. NI KWA VIPI KIONGOZI WA TISS NI FISADI ????????????? AMEFANYA AU KUSHIRIKI UFISADI UPI, WAPI, NA LINI?????????????????????? TUNASUBIRI MAJIBU YAKO.
 
Huyo ni fake angekuwa TISS original asingebuluzwa na kupigwa picha hadharani.
Kanasa, na hayo Makabulasha ni fake pia.

Hahahaaaa.... Hii serikali ni zaidi ya unavyoifikiria mkuu, subiri tuone ni hatua gani atachukuliwa!
 
huyu jamaa yuko nje kwa ile mikwara ya Kova na jamaa kuwa nje ndani ya muda mfupi inaacha maswali mengi
 
Wewe akili yako haiko sawa! Unaandika tu upuuzi humu! Serikali itauaje mahabusu? Na hao TISS machizi labda ni wewe mwenyewe nadhani kichwani hauko timamu. Mnaleta story za vijiweni humu JF wakati huna unalolijua kuhusu TISS. Shame on you!

Wewe uliyeko timamu kichwani hebu tuambie basi..tupe story za ndani ya TISS na si za vijiweni...!
 
Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa! Sawa bana wewe ni insider wa TISS UNAJUA ZAIDI. HEBU TUJUZE BASI, ULIWAONA WAPI VICHAA WA TISS?????? MANAKE UMESEMA TISS KUNA VICHAAA. NA HUO MPANGO WA KUUA MAHABUSU UMEUPATA WAPI??? HEBU THIBITISHA HAPA, KISHA TOA TAARIFA POLISI ILI WAHUSIKA WAKAMATWE!

Polisi amkamate afisa wa TISS,,,,,sio kwa tanzania hii . Wao ni zuga tu.
 
Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa! Sawa bana wewe ni insider wa TISS UNAJUA ZAIDI. HEBU TUJUZE BASI, ULIWAONA WAPI VICHAA WA TISS?????? MANAKE UMESEMA TISS KUNA VICHAAA. NA HUO MPANGO WA KUUA MAHABUSU UMEUPATA WAPI??? HEBU THIBITISHA HAPA, KISHA TOA TAARIFA POLISI ILI WAHUSIKA WAKAMATWE!

Ngoja tukusaidie ingawa ni nje ya thread,miaka ya 90 I mean 1990's hivi kulikuwa na tatizo sana na uwindaji wa ndovu kule tarangire/manyara!jamaa aliyekuwa anapiga biashara hii alikuwa mwarabu mmoja maeneo ya Galapo Babati,sasa kumpata nyendo zake na ushaidi ilikuwa kazi kweli!akatumwa TISS mmoja ambaye alipofika galapo akawa anajifanya ni kichaa,anabeba makopo mauchafu uchafu nk!yule mwarabu alikuwa na matrekta na mgahawa,basi jamaa akajijengea mazoea ya kwenda kuomba omba chakula pale,kwa sababu hakuwa akipiga mtu wala kuwa na neno na mtu ikawa rahisi kuzoeleka,taratibu jamaa akawa hata mwarabu akiwa na waarabu wenzie friends yeye anaenda na kuzunguka zunguka..hakuna aliyekuwa akimtiliia maanan as wote walijua ni kichaa!mshkaj alikusanya ushaid wa kutosha,audio as alikuwa akiwarecord,alipokuwa na uhakika na kujua huwa wanaficha wap pembe jamaa aka-organise police wakaja na defender,jamaa akamkamata mwarabu baada ya kumtolea na vitambulisho!watu wote hawakuamin kuwa yule kichaa ndo alikuwa TISS na kufanikiwa kumtia mikonon na ushahid juu wa uhakika mwarabu!to cut the story shot,go find anyone aliyetoka maeneo ya galapo huko babati ambaye ana miaka 30 plus/au alikuwa galapo miaka ya 90 hivi ,uulizie hii taarifa kama hujathibitishiwa.
 
Back
Top Bottom