#COVID19 Ofisi nyingi hazitaruhusu watu kuingia bila kuwa na chanjo

#COVID19 Ofisi nyingi hazitaruhusu watu kuingia bila kuwa na chanjo

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari, lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya Serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo.

Kwa namna moja au nyingine itatulazimu na sisi tusiotaka kuchanjwa tuchanje bila kupenda maana hatutakuwa na jinsi.

Kwa kifupi huyu mama ametuharibia sana nchi ndani ya kipindi kifupi sana.

Hili suala la korona tulikuwa tumeshalisahau kitambo, watu wachache wenye maslahi yao binafsi wamemshika masikio matokeo yake anaturudisha kule kule tulipotoka.
 
Baadhi ya waajiri katika nchi mbali mbali duniani tayari ni lazima kwa waajiri kupata chanjo ili kuwalinda Wafanyakazi wao kwa maambukizi na vifo. Hutaki chanjo basi ajira inaota manyasi.
Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari ,lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo....
 
Ukiwa vitani unakusanya SILAHA ZOTE....

#ShimeTujiandaeNaChanjo
#KaziInaendelea
 
Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari, lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya Serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo...
Mbona hata kiongozi wako Mbowe, Tundu lisu wanasisitiza chanjo!

chanjo yaani hayati Magufuli pamoja na mapungufu yake lakini kuhusu corona tutamkumbukaa!
 
Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari, lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya Serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo..
Kwan wewe hujawahi kuchanjwa? Kuchanjwa ni kujikinga na magonjwa, ishu ni je imehakikiwa? Hivi unadhaninwakati wa jiwe ndio nchi hii tulikuwa salama?

No never Akili ndg kweli kweli itawaangamiza watanzaniakwa kiingereza inaitwa vaccine, kwa taarifa wazungu wanachanja sana .sindano si chini ya 5 wanapokuja Africa. Nahisi hadi ukimwi Wanafanya vaccination.
 
Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari, lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya Serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo...
Hakuna nchi duniani imefanya hivi, na haitatokea kamwe. Ukiwaza kitu, fikiri kwa mapana kabla ya kuandika tu, hujui kufanya uchambuzi vema wa mambo unaonekana
 
Kweli wazungu wakiamua jambo lao lazima liwe. Hiyo Cororna inavyopaishwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari unaweza sema hali ni tete sana mtaani, lakini ki uhalisia mtaani wananchi wameamua kuishi nayo tu na maisha yanaendelea kama kawaida. Serikali aiche kuhadaa wananchi
 
Back
Top Bottom