Ndugu mtoa hoja ni vizuri kutumia taarifa za ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) 2023-2024 kitaalam na si kwa mihemko. Hatua zilizochukuliwa na NHIF zimekuwa endelevu kwa muda sasa zenye kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu (sustainable) na wakati huo huo upatikanaji wa huduma bora za bima ya afya kwa wananchi.
NHIF imeendelea kupunguza matumizi katika nyanja mbalimbali ikiwemo uendeshaji
NHIF imekuwa ikichukua hatua kali za kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu. Hii imepunguza upotevu wa fedha
NHIF imeboresha mifumo yake katika usimamizi wa shughuli za Mfuko na uchakataji madai inayozuia mianya ya upotevu wa fedha
NHIF imehakikisha uwajibikaji kwa kwa watumishi wake kwa kuhakikisha madai yote yanalipwa si zaidi ya siku 60.
NHIF imesajili vituo 10,098 ambavyo ni Binafsi, Vya Kidini na Vya Serikali na vinalipwa kwa muda stahiki kwa hiyo si kweli kwamba vituo binafsi vyote vimejitoa.
Sasa nani anamihemko hapa. Umekuja kujibu hoja bila ya kuelewa Hoja. Uliyoyaongea yote ni nadharia na hayo ndio mnayowadanganyia viongozi kwa kuandika mareport kwa data za kupika.
Tukitaka kujua uzuri au ubaya wa NHIF tunapaswa kuwauliza vituo vya Afya na Hospital….. wao ndio watawasemea. Stop kuendelea kudanganya watu wee mzee
Hakuna Hosp ya maana inayotaka kufanya kazi na NHIF , wewe unajua MOi, MNH, KCMC , JKCI, BMC combined inawadai Bei gani ? That is rough sampling
Private ndio hawataki kusikia kitu NHIF ….. umesajili Ghost Hospitals za Private…… do you know namna wagonjwa wa NHIF wanavokuwa treated wakitaka huduma za provate….. kama NHIF ingekuwa ni worth it …… hakuna Hospital ya Private inge pull off.
Tambua hata gvt Hospitals , ni vile tu hao ni wateja wa lazima and they are mandated kufanya kazi na nyie kisheria ipo hivyo … otherwise msingekuwa na mteja
Hivi mnafanyaga hata opererational study kujua reputation yenu kwa Hospitals?
Bado NHIF is not perfoming, umetamka neno sustainability ……. You have wrong idea we mzeee….. sustainability while private Hosp zina pull off
Hamuwezi kuwa na profit , halafu watanzania wapate huduma bora. Kama mnaziada mana yake watanzania wanakufa kwa kukosa huduma
Listen , mmepika data na mmedanganya Umma na hiyo ni JINAI , mnahitaji Special audit kwenye maeneo 3
. Forensic Audit … kufanya deeper Investigation and Substantive test
2. Performance Audit… kuangalia complince yenu na vitu vya Afya
3. Operational Audit
4. Financial Audit ….. hapa tutaangalia curent ratio , quick ratio , asset na liabilities mlizolimbikiza kwa wateja
Mtuambie hiyo ziada mmetoa wapi
Njoo na data, usilete maneno ya kuandika kwenye report zenu za mchongo ; tumesajili vituo 10,000, tunaendelea lufanya sustainability bla-bla ….. hayo ndio maneno ya report za uzushi
Njoo na Data
Hosp ngapi zinawadai ? Jumla ya fedha zote
Njoo na data, mnachukua mda gani kuwalipa wateja
Njoo na data watz wangap wanakosa huduma hali ya kuwa wana kadi
Njoo na data za toto card
% covered out of 65 Mil
Mnaenda kuweka fedha za michango UTT huku watu wanakosa huduma, are you business entity or non profit organisation ?