Ofisi ya Taifa ya usalama Serikalini

Ofisi ya Taifa ya usalama Serikalini

Nenda pale jirani na ofisi za TFNC jirani na Ocean Road Hospital ugonge pale uulizie majukumu yao!!! Nchi hii iko imara kila sekta
Iko Imara Kila sekta wapi wakati Kuna Ofisi ,za umma tunakuja kuzijulia Jamii Forum badala ya kukutana nazo Kazini..?? Huo ndo uikara,kikalia TU viti vya kuzunguka na kujipulizia hewa safi kutoka kwenye AC ?? Nina Miaka 28 Ila nilikuwa sijawahi Kusikia Wala kuona angalau hata Shughuli Moja ya hiyo Ofisi. Sasa huo ushauri wanapewa kina Nani au ni Special case..??
 
Mkuu hii ni tofauti na ya TISS. Hii ni taasisi nyingine kabisa nadhani iko chini ya wizara ya utumishi
Utumishi lakini kitengo chao Usalama. Mambo ni mengi MDA michache Ngoja tuishie hapo. Hata Ofisa wa TISS atakuambia niko utumishi ukiachilia wale ambao wako kwenye taasisi za umma na binafsi. Hawa ndiyo wasiojukikana haswa🤣🤣🤣
 
Mimi pia ni mtumishi wa umma ila zikuwahi kuwa na taarifa zao kabisa.
Kwa hiyo wewe hujafanyiwa vetting. Kisheria wewe siyo Mtumishi wa umma kama hujafanyiwa vetting. Kiboko hiyo!!!
 
Iko Imara Kila sekta wapi wakati Kuna Ofisi ,za umma tunakuja kuzijulia Jamii Forum badala ya kukutana nazo Kazini..?? Huo ndo uikara,kikalia TU viti vya kuzunguka na kujipulizia hewa safi kutoka kwenye AC ?? Nina Miaka 28 Ila nilikuwa sijawahi Kusikia Wala kuona angalau hata Shughuli Moja ya hiyo Ofisi. Sasa huo ushauri wanapewa kina Nani au ni Special case..??
Kwa taarifa yako tuu ofisi hii ina KAZI kubwa Sana na wako busy. Niishie hapo. Kifupi kama taasisi haikuhusu huwezi kuifahamu. GSO ndiyo yenyewe.
 
Hawa kazi yao kubwa ni Kufanyia Vetting watumishi wa Umma na kutoa mafunzo ya namna ya kudeal na nyara za Serikali. Katika mafunzo yao huwa wanapenda kusema Ukiwa mtumishi wa Serikali/Umma utafuatiliwa mpaka siku unaingia kaburini
Yap. Mambo ni mengi hapo mkuu. Tuishie hapo maana nazo ni mambo ya ndani kwa wasiohusika. Big up
 
Hii nchi kumbe ina ofisi nyingi namna hii na hamsemi leo ndo nimejua kama kuna hii ofisi ya usalama Serikalini ambayo wajibu wake ni kutoa elimu kuhusu kanuni za usalama Serikalini kwa watumishi wa ngazi zote. Hii ni tofauti na taasisi ya TISS ambayo iko chini ya ofisi ya Rais wao nadhani wako chini ya wizara inayohusika na mambo ya utumishi.
Inaitwa GSO

Nakumbuka siku moja kwenye mafunzo wanatuambia Serikali ni dude jeusi linaloishi gizani ukifanya fyoko wanakufyatua kichwa unakwisha taratibu
 
Sasa kivipi madini yameibwa kwa miaka 20? Kivipi Tanzanite inapitishwa chini ya ukuta? Kivipi CCM mafisadi wapo madarakani kama kweli usalama wapo?

Hawana lolote ni kelele tu otherwise hata kifo cha JPM kisingevuja kirahisi vile.
Govt Security Office, hawa ndo wale wazee wa Mihuri Nyekundu... SIRI/CONFIDENTIAL

Usiombe file lako liingie barua yenye hiyo muhuri
 
Kwahiyo zamani kila kinachoandikwa JF mlikuwa mnakikubali tu! Basi sawa.

Lakini zama za sasa za Mtoto wa Shule kama mimi lazima nibishe mpaka nithibitishiwe pasi na shaka kwamba kilichoandikwa ni sahihi. Kama sio, basi hiyo ni chai!
Unakuwa mjinga sasa ndo maana ukajiita mtoto wa shule
 
Back
Top Bottom