Ofisi ya Waendesha Mashtaka kugeuka kuwa ofisi ya wafuta mashtaka kunatia doa mfumo wa haki nchini

Ofisi ya Waendesha Mashtaka kugeuka kuwa ofisi ya wafuta mashtaka kunatia doa mfumo wa haki nchini

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Ofisi ya DPP imegeuka kuwa ofisi ya wafuta mashtaka badala ya ofisi ya waendesha mashtaka. Haya madaraka mapya yakufuta mashtaka wameyatoa wapi?

Kwanini imeacha jukumu la Msingi la kuanzishwa kwake? Kama wamebaini walikosea, hao waliokosea kifungua mashtaka wanasubiri nini kushtakiwa?
 
Binafsi napingana na wewe,tungekuwa tunaweza kusimamia haki kwa mujibu wa Sheria na taratibu,Bila kubambikia watu kesi,Bila kuonea Bila kudhulumu,Bila kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukanda na ukabila ningeunga mkono malalamiko yako,ila kwa njia tuliyokuwa tumeichagua tunapoteza uhalali hata wa kulalamikia yanayotokea leo.
 
Laana inayolitesa bara la afrika chanzo chake ni uonevu uliopo katika mifumo ya utoaji haki.

Kesi 147 za takukuru za uonevu zinapofutwa inabidi tuangalie kwa kina na kujadili ni wangapi wameteseka ambao maisha yao yanawategemea wote waliobambikiwa kesi.
 
aliesema taasisi ya urais ni mhimili uliojichimbia chini zaidi alikua yuko sahihi ni upofu wetu tu kutokuchambua mambo kwa kina badala yake tumejikita kudandia hoja za kisiasa kwa juu. Ni dhahiri sasa yanayo tendeka yote saivi yanazingatia matakwa ya ikulu
 
Hapa DPP anaenda kutengeneza bomu ambalo litaiathiri serikali yote kwa ujumla
Kwani hujui MAMLAKA YA DPP kwamba ni pamoja na uwezo wa kufuta kesi bila kutoa sababu! Mkiambiwa Katiba Mpya na sheria njema zinahitajika mnaruka ruka kama kuku wa mdondo!

Acha DPP atumie mamlaka yake kisheria, nendeni mahakamani mkapinge sheria husika!

Watu walihoji uwepo wa sheria TATA ya UHUJUMU UCHUMI na baadhi ya sheria zenye kueleza makosa ya kutokuwa na DAHAMANA, mkanengua kuwapinga, kaa kwa kutulia utakata shanga zako.
 
Back
Top Bottom