DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Miongoni mwa ofisi zinazotoa huduma zilizopo kwenye kituo hicho kilichopo Posta Jijini Dar es salaam ni pamoja na ofisi za TRA, PSSSF, NSSF, Uhamiaji,NIDA, RITA,, BRELA, Polisi, na NHIF.
Licha ya kituo hicho kuwa na umuhimu kwa wananchi na wadau mbalimbali katika kuharakisha huduma upatikanaji wa huduma lakini kumekuwepo na changamoto ambayo inashangaza kuona mamlaka zinachelewa kuiona na kuitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuondoa usumbufu na kuongeza maana halisi ya kituo hicho, ambacho sifa yake kuu inaonekana ni kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Kwa mara kadha nimefika eneo hilo, jambo nililobaini kama changamoto ni kwamba inapotokea umeme umekatik ofisi hizo zinaacha kufanya kazi na Watumishi wanaondoka kabisa kwenye ofisi hizo huku wananchi wakikaa muda mrefu kungojea huduma mpaka umeme unaporejea ndipo huduma zinaendelea.
Katika mazingira ya aina hiyo inafanya wananchi kukaa muda mrefu eneo hilo jambo ambalo linafifisha mantiki halisi ya kituo hicho, mfano kuna siku nyingine tumewai kukaa masaa zaidi ya matatu umeme ukiwa umekatika, hii imekuwa kero karibia kila siku.
Katika kuzingatia umuhimu wa kituo hicho ambacho kimekuwa msaada , natoa wito kwa mamlaka kukiwezesha kituo hicho kuwa na miundombinu mbadala ya umeme (jenereta) ili umeme unapokatika huduma zisikwame, lakini pia kuwezesha uwepo wa vifaa vya kisasa hususani kompyuta ambazo zinaweza kuendelea kutumika kwa muda hata umeme unapokatika.