Hili ni tatizo kubwa. Brela wao wameweka landline (TTCL-na wanajua si watu wote wamezoea code 07 au 06) na kuna wakati utasubirishwa kwa kipindi kirefu.
Taasisi nyingine utapiga simu (landline) lakini itajibiwa line imezuiwa. Email ndiyo usithubutu.
Changamoto nyingine; Taasisi wanaandika kuwa masuala yote hasa usajili yanafanyika online, lakini mwisho wa siku lazima jambo fulani lifanyike manual. Kwa mfano TAMISEMI kupitia mfumo wa TAUSI, unafanya taratibu zote kupata leseni ila ukitaka leseni kwa niaba ya taasisi yako inabidi upeleke barua manually ya kumtambulisha 'caretaker'. Yaani kama Kampuni ipo Bunju, unapaswa kupeleka barua Manispaa Kinondoni.
Wizara ya afya unasajili hospitali kwenye mfumo ila cheti kinafuatwa manually!!