G
guest-1788671453
Guest
- Thread starter
-
- #21
hapo utasema waafrika tuko sawa kweli?Afisa wa serikali anakupa miadi ya kushughulikia tatizo lako. Ikifika siku ya ahadi anakuuliza ni kuhusu nini vile?
Ni kwamba hawako tayari kufanya kazi zao pasi na ushawishi wa rushwa. Wala hawaoni shida kukuzungusha hata miaka.
Hili jambo huwa linanisikitisha Sana, Choo ni kama jalala au Banda la Ng'ombe huko Wilaya ya KibakweUkitaka kujua akili ya mwafrika nenda kwenye choo chake hata huko maofisini
uzengeHili ni tatizo kubwa. Brela wao wameweka landline (TTCL-na wanajua si watu wote wamezoea code 07 au 06) na kuna wakati utasubirishwa kwa kipindi kirefu.
Taasisi nyingine utapiga simu (landline) lakini itajibiwa line imezuiwa. Email ndiyo usithubutu.
Changamoto nyingine; Taasisi wanaandika kuwa masuala yote hasa usajili yanafanyika online, lakini mwisho wa siku lazima jambo fulani lifanyike manual. Kwa mfano TAMISEMI kupitia mfumo wa TAUSI, unafanya taratibu zote kupata leseni ila ukitaka leseni kwa niaba ya taasisi yako inabidi upeleke barua manually ya kumtambulisha 'caretaker'. Yaani kama Kampuni ipo Bunju, unapaswa kupeleka barua Manispaa Kinondoni.
Wizara ya afya unasajili hospitali kwenye mfumo ila cheti kinafuatwa manually!!