Ogopa binadamu unaongea naye hakujibu bali anatabasamu

Ogopa binadamu unaongea naye hakujibu bali anatabasamu

Ni kweli kabisa kuna jamaa alikuwa wa hivyo Sasa Mimi nikawa nimezoea nikikutana naye na wakiwepo watu wengine naanza kumtania watu wanamcheka Ila yeye hajibu anatabasamu tu .

Siku moja nikamtania tena mbele ya watu wakacheka sana yeye akasmile Sasa wakati wa kutawanyika nikampa lift kwenye Corolla yangu tulikuwa wawili tu ,jamaa alinikwida vibaya ovyo ,akanibana Koo alafu ndiyo akawa anasema unapenda sana kunidhalilisha ,nililia sana kwa kile kibano omba msamaha wapi ,mwamba anatembeza makonde tu alafu kanibana kwenye Sterling nikaona Cha kufia nini nikawa napiga makelele ndiyo watu kuja kutuamulia toka siku hiyo jamaa namheshimu sana na simletei utani kabisa.

Hivyo hata job nikiletaga tafrani utasikia boss anasema au tumuite fulani lengo niogope
Wewe ni wa kike au wa kiume ?
 
Nilikuja kugundua mtu anaetabasamu mara nyingi hata katika mambo magumu na mabaya anakuwa na maisha marefu yenye furaha na amani na uso wake una nuru wakati wote,
Mfano mh Kikwete .
kikwete ana nuru na maisha marefu sabu ana uhakika wa maisha yale ya kifalme, (daraja la juu zaidi) hoja yako haina uhalisia mkuu.
 
Ni kweli kabisa kuna jamaa alikuwa wa hivyo Sasa Mimi nikawa nimezoea nikikutana naye na wakiwepo watu wengine naanza kumtania watu wanamcheka Ila yeye hajibu anatabasamu tu .

Siku moja nikamtania tena mbele ya watu wakacheka sana yeye akasmile Sasa wakati wa kutawanyika nikampa lift kwenye Corolla yangu tulikuwa wawili tu ,jamaa alinikwida vibaya ovyo ,akanibana Koo alafu ndiyo akawa anasema unapenda sana kunidhalilisha ,nililia sana kwa kile kibano omba msamaha wapi ,mwamba anatembeza makonde tu alafu kanibana kwenye Sterling nikaona Cha kufia nini nikawa napiga makelele ndiyo watu kuja kutuamulia toka siku hiyo jamaa namheshimu sana na simletei utani kabisa.

Hivyo hata job nikiletaga tafrani utasikia boss anasema au tumuite fulani lengo niogope
Juzi Basi la BM limedondoka Lugalo kwa abiria kumzaba kumzaba kibao dereva! Ni hatari
 
Hawa watu ni balaa,, yupo kaka yetu Huwa ni mkimya na anasauti ya kipole sana, hua mara nyingi anatabasamu, aliwahi kufanya matukio mpka kesho nikiona mtu anamfanyia mazoea namtahadharisha 'kaka yangu ni kichaa atakuua'

1.jamaa hua ni mchezaji mzuri wa mpira, beki mzuri tuu, Kuna siku kulikua na mechi za wafanyakazi ofisini kwao, jamaa akaomba acheze striker, kisa Kuna beki wa upande WA pili alimwita jamaa mchele mcehele Hana maajabu, bro alisumbua sana mbele mabeki akiwepo jamaa aliemdharau, eh jamaa akaona hizi sifa Sasa, akamchezea rafu mbaya sana brother... Akapewa penati, goli!! Sasa Cha ajabu mpira ukaenda kati brother akaanza kuukokokota sio kulifuata goli anamfuata jamaa, kufika kwake akafanya kama kumpasia hivi, jamaa Ile anaupokea alichotwa mtama akapaa hewani akatua kwa taya aisee jamaa alililia kama mtoto, mkono ulivunjika, taya zimepinda, aliuguzwa karibu miezi sita.

2.kuna Mzee mmoja mtaani alimjibu vibaya mama yetu, akamtishia vibaya na hatimaye kumpiga kibao, visa tuu vya kibiashara, brother hakuwepo, alivyofika Mzee yupo upande WA pili jamaa anahadithiwa tuu anajibu kwa upole na uso WA tabasamu, kidogo jamaa akaingia jikoni akachukua panga, akatoka nje kawaida tuu, akafika mlangoni kwa huyo Mzee sijui ikawaje Kuna msumari ulimshika shati jamaa akajivuta kwa speed ya ajabu shati likagawanyika, Mzee alisikia akatoka ghafla kama mshale aisee lilirushwa panga hewani... Lilimkosa yule Mzee hajakaa sawa panga lipo angani jamaa yupo speed anamfuata, Mzee alichotwa mtama, ametua sijui panga lilifuatwa mda gani tayari kashaliweka shingoni kwa Mzee,, aisee kina mama sio vilio, kilichosaidia ni vijana mtaani na bibi yetu alikua analia na kutoa machozi... Jamaa akanyanyuka akaenda chumbani kwake kulala, aliamka usiku, kula!!
 
Nimekaa na kuishi na watu kadhaa unamtendea sivyo ila yeye ana smile tu. Hasemi kitu. Yeye pamoja na mabaya yanayofanywa na watu wanaoona wako sawa na wabishi yeye kazi yake ni kuongea kidogo baadae mnapojadili yeye kimya, na kuendelea ku smile 😃 tu. Kuna maamuzi atachukua na utashangaa tu ameshakipa, mwingine wala hakukimbii anakuacha tu.
Kuna kijiji fulani nyanda za juu kusini wakazi wake wako hivyo, unaweza kujikuta asubuhi unapiga mswaki ziwani
 
Back
Top Bottom