Hawa watu ni balaa,, yupo kaka yetu Huwa ni mkimya na anasauti ya kipole sana, hua mara nyingi anatabasamu, aliwahi kufanya matukio mpka kesho nikiona mtu anamfanyia mazoea namtahadharisha 'kaka yangu ni kichaa atakuua'
1.jamaa hua ni mchezaji mzuri wa mpira, beki mzuri tuu, Kuna siku kulikua na mechi za wafanyakazi ofisini kwao, jamaa akaomba acheze striker, kisa Kuna beki wa upande WA pili alimwita jamaa mchele mcehele Hana maajabu, bro alisumbua sana mbele mabeki akiwepo jamaa aliemdharau, eh jamaa akaona hizi sifa Sasa, akamchezea rafu mbaya sana brother... Akapewa penati, goli!! Sasa Cha ajabu mpira ukaenda kati brother akaanza kuukokokota sio kulifuata goli anamfuata jamaa, kufika kwake akafanya kama kumpasia hivi, jamaa Ile anaupokea alichotwa mtama akapaa hewani akatua kwa taya aisee jamaa alililia kama mtoto, mkono ulivunjika, taya zimepinda, aliuguzwa karibu miezi sita.
2.kuna Mzee mmoja mtaani alimjibu vibaya mama yetu, akamtishia vibaya na hatimaye kumpiga kibao, visa tuu vya kibiashara, brother hakuwepo, alivyofika Mzee yupo upande WA pili jamaa anahadithiwa tuu anajibu kwa upole na uso WA tabasamu, kidogo jamaa akaingia jikoni akachukua panga, akatoka nje kawaida tuu, akafika mlangoni kwa huyo Mzee sijui ikawaje Kuna msumari ulimshika shati jamaa akajivuta kwa speed ya ajabu shati likagawanyika, Mzee alisikia akatoka ghafla kama mshale aisee lilirushwa panga hewani... Lilimkosa yule Mzee hajakaa sawa panga lipo angani jamaa yupo speed anamfuata, Mzee alichotwa mtama, ametua sijui panga lilifuatwa mda gani tayari kashaliweka shingoni kwa Mzee,, aisee kina mama sio vilio, kilichosaidia ni vijana mtaani na bibi yetu alikua analia na kutoa machozi... Jamaa akanyanyuka akaenda chumbani kwake kulala, aliamka usiku, kula!!