Mwaka 2020 mwishoni nilikopa Pesa CRDB ml.36 ambapo dhamana ilikuwa Mshahara wangu ofisini(ilikuwa nilipe kwa miaka 5).Baada ya miezi 11 tangu nikope nikiwa nakatwa rejesho kutoka kwenye Mshahara wangu,Kampuni ikanipunguza kazi mimi pamoja na wenzangu kama 200. CRDB wakaanza kunipigia kuuliza rejesho nikawa nawatukana mpaka wakakoma,wakatafuta Kampuni ya kukusanya madeni,nao wamenipigia kama mara tatu nawaporomoshea matusi naona wameona maji marefu wameacha kunipigia sitakagi ujinga. Maana niliwauliza wakati nakopa niliweka nyumba yangu au kiwanja au gari langu kama dhamana jibu wakaniambia HAPANA,wakasema dhamana yako ilikuwa Mshahara wako,nikawajibu sasa kama dhamana yangu ilikuwa Mshahara wafuateni ofisini waulizeni kwa nini walinidhamini nikope halafu baada ya miezi 9 wakanipunguza kazini,wanategemea nilipe deni kwa matako??mpaka leo wapo kimya, Kadi ya Bank ya CRDB nikishaichoma na moto