Ogopa sana Marafiki. Heri akuwinde mtu baki kuliko rafiki yako ambaye huwezi kumdhania

Ogopa sana Marafiki. Heri akuwinde mtu baki kuliko rafiki yako ambaye huwezi kumdhania

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,812
Reaction score
82,328
Kumeibuka week hii story yakusikitisha ya mwanamke Roselyn Asanti Mchuna almaarufu Chunna. Ambae inasadikiwa alilishwa sumu na mmoja ya rafiki zake huko nchini Kenya.
1000247445.jpg
1000247448.jpg


Mwanadada huyo mwenyeji wa Mombasa alikuwa influencer na mfanyabiashara mkubwa wa nyumba za kupanga maarufu kama Air BnB katika miji mbalimbali nchini Kenya ikiwemo Nairobi.

Inadaiwa kuwa siku ya Valentine's February 14, 2026 ambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa ya mwanadada huyo aliamua kufanya sherehe kwaajili ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
1000247433.jpg


Hivyo alialika marafiki na familia yake lakini alianguka wakati sherehe hiyo ikiendelea ambapo alikimbizwa hospitali na baada ya uchunguzu uliofanywa na wataalamu ilionekana alikula sumu (kwenye chakula au kinywaji).

Hali hiyo ilimpelekea ubongo wake kuathirika (kufa) kwa zaidi ya asilimia 50 hali iliyopelekea mwili kushindwa kufanya kazi vizuri. Hawezi kula, kuona, kuongea wala kutembea.

Familia inasema Roselyn amekuwa ICU kwa miezi kadhaa na sasa analelewa na mama yake nyumbani. Pia wanasema waliripoti tukio hilo polisi lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliehojiwa.
1000247449.jpg
1000247442.jpg
1000247439.jpg


Tuchunge sana watu tunaowaamini ndio wabaya zaidi kwakuwa unakuwa hauna mashaka nao.
 
Food poisoning haina maana chukula kimetiwa sumu.chakula au kinywaji kilichochafuliwa na bakteria, virusi, vimelea, au sumu zinazozalishwa na vijidudu hivyo.
Thanks. Ila inasemekana aliwekewa sumu either kwenye kinywaji au chakula.
 
kama Mama yako mzazi bado yupo hai mpende sana akiii, nimewaza tu kwa sauti kwenye wale ‘waliokuwa watu wake wa karibu’ nani bado yupo naye karibu mpaka sasa..!??

Hii dunia..!🙌🏾💔💔
Most of them huwezi kuwapata. Tena wengine yawezekana na biashara zake wameshamuibia.
 
Back
Top Bottom