Ogopa Teknolojia: Nimeweka mkataba wa bandari kwenye Chat-GPT, Imejibu kwamba bandari zitakuwa za DP World Milele!

Ogopa Teknolojia: Nimeweka mkataba wa bandari kwenye Chat-GPT, Imejibu kwamba bandari zitakuwa za DP World Milele!

Sana tena, mtu nishalenga dili zangu la kuwapangisha nyumba DP World kwa Dirham.

Nishaanza na kuwanoa wajukuu Kiarabu chao, Mungu akiwajaalia wanaweza kupata wachumba wa Dubai huko, halafu wajinga wajinga wanataka kuleta kauzibe.
Aiseee


Kila nikisoma koment zako najikuta nazid kukupenda
 
Kwa wale ambao hamuijui Chat GPT, hii ni teknolojia ya Artificial Intelligence (Akili Bandia),

Kumekuwa na vuta nikuvute ya huu mkataba, wapo wanaosema mkataba huu ni halali wakiongozwa na spika wa bunge Tulia Ackson na msemaji Gerson Msigwa... Upande wa pili ndio hawa wanaofanya ishu itrend kila kona ya nchi kwamba mkataba huu unapiga nchi mnada.

Nikaona nipandishe mkataba huu kwenye mtambo wa chat gpt.

Nikaiuliza swali - makubalioano haya yanaweza kuzipora bandari za Tanzania milele.

Jibu ndilo hilo kama lilivyo kwenye picha,

Huu mkataba unamwezesha mwarabu kuichukua bandari milele, Tukitaka kuuvunja hatuwezi upande moja, DP World akiamua anaweza kuiendesha bandari milele!!

View attachment 2680572

Nikaiuliza, kuna kifungu kinavunja mkataba 23(1) kukiwa na "permanent cessation" hii ina maana gani, ikanijibu kwamba ni mpaka pale DP world atakapoamua kuacha shughuli zake, Ni mpaka yeye atakapoamua.

Nikauliza kama inaweza kuwa baada ya miaka elf 1, ikajibu kwamba inaweza kuwa milele "indefinetely"


View attachment 2680573

Inasikitisha sana kuona mpaka robots wanaukataa huu mkataba ulivyo wa hovyo, lakini ajabu viongozi wetu baadhi maprofesa wanajiaibisha kwamba kila kitu kiko sawa, Aibu tupu!

Ushauri wangu: mkataba uwe na kikomo cha muda, Mfano majirani wetu Zanzibar bandari yao hivi karibuni wamesaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya "The Africa Global Logistics - AGL", Sisi huku kwetu Tanzania Bara kwanini mkataba wetu hauna kikomo cha muda ? nachopendekeza mkataba uwe na muda wa kikomo, kwa sasa hao hao DP world wanaweza kuonekana waaminifu lakini hakuna aijuae kesho, wanaweza kuja kutukomoa huko mbele na hatuna cha kuwafanya, hii sio sawa kwa watoto na wajukuu zetu kuja kuumia kwenye jambo ambalo linaweza kurekebishwa ndani ya siku 1 tu bungeni.

kampuni iliyopita ya TICTS iliyosimamia bandari kwa miaka 22 ilikuwa na uwezo mdogo na madudu mengi haifai hata kidogo, suluhisho imebidi ije kampuni yenye ufanisi zaidi lakini hakuna sababu hata moja ya kujishusha kiasi hiki, Ni sawa na kwenda kwa mganga ukiwa na hali ya kawaida kiuchumi unataka pesa zaidi unapuuzia masharti lakini ukipata pesa unaanza kuona masharti ni magumu, unatamani kurudi hali ya zamani uwe huru lakini ndio hivyo tena huwezi.
It is common sense,kama wameonyesha kutokuwa na waaminifu tangia mwanzo,kwa nini tuendelee nao.Tenda hii itangazwe upya makampuni yanayotaka kuiendesha Bandari yashindanishwe kwa uwazi.Utapeli uliofanywa na akina Mbarawa haukubaliki.Ingekuwa China akina Mbarawa wangekuwa Hayati leo,bahati yao.
 
Mawakili wenu?!So wewe ni mmoja wa wanaouza nchi yetu eti?Ndio maana ulifurahi ndugu yako alipo olewa na familia ya Eugenicist Billy Gates,ni zuzu kweli kweli.
Hivyo unavyo wewe tu, hata mawakili wenu Mbeya hawajavitaja.
 
Huo sio mkataba ni makubaliano kati ya tz na dubai mikataba itakuwa kati ya TPA na dpw kumbuka kwenye chat gpt hujaweka ushahidi wa sheria ya ardhi ya 1999 hairuhusu mwekezaji kumiliki ardhi Tanzania. Haiwezekani dubai kujimilikisha kitu Nchi ina sheria zake
 
Itakuwa kichekesho.Wana moral authority gani ya kumpeleka mtu mahakamani.Halafuu,mbona hajataja mtu?
 
Back
Top Bottom