Uchaguzi 2020 Oktoba 2020, Tunachagua kati ya Utu wa Mtu na Maendeleo ya Vitu

Uchaguzi 2020 Oktoba 2020, Tunachagua kati ya Utu wa Mtu na Maendeleo ya Vitu

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Wagombea prominent mwaka huu ni watatu Magufuli, Lissu na Membe, lkn wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda ni wawili Magufuli na Lissu.

Wagombea hawa wawili tayari wameshajipambanua wazi nini vipaumbele vyao 'first priorities'.

Wakati anachukua fomu ya NEC mgombea wa CCM Rais Magufuli alisema tumuongeze miaka 5 ili amalizie miradi yake aliyoianzisha, madaraja, barabara, ndege, meli, reli, mabwawa nk. miradi ambayo anadhani bila yeye hakuna wa kuiendeleza, akaongeza kusema wakiwapa upinzani watayavunja madaraja aliyoyajenga.

Mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu mara nyingi amekuwa akisema akichaguliwa kitu cha kwanza ni kujenga MIFUMO, mifumo bora ya utawala wa sheria unaozingatia haki za binadamu na utawala bora, mfumo bora wa kodi, mfumo bora wa jeshi la polisi, mfumo bora wa mahakama nk., yaani ni mifumo inayogusa maisha ya mtanzania moja kwa moja.

Kiufupi (summary), nionavyo mimi, uchaguzi wa mwaka huu tunachagua kati ya Utu na Vitu.

Nini kipaumbele chako, maendeleo ya watu au maendeleo ya vitu
 
Naenda kuchagua anayejali UTU wa binadamu,wanadamu wote ni SAWA na watendewe kwa HAKI.Tunakataa mtawala anayejali vitu dhidi ya UTU wetu.
 
TANZANIA BADO INAITAJI MTU WA NAMNA YA MAGUFURI ATA KWA MIAKA KUMI IVI KWA MAANA ANGALAU ILA UYO MWENGINE HAPANA HANA SIFA HATA ...
 
Watu wakiheshimiwa na wakashirikishwa, watawezesha maendeleo yao wenyewe kwa furaha zaidi kuliko serikali ya MTU mmoja.
Wagombea prominent mwaka huu ni watatu Magufuli, Lissu na Membe, lkn wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda ni wawili Magufuli na Lissu.

Wagombea hawa wawili tayari wameshajipambanua wazi nini vipaumbele vyao 'first priorities'.

Wakati anachukua fomu ya NEC mgombea wa CCM Rais Magufuli alisema tumuongeze miaka 5 ili amalizie miradi yake, madaraja, barabara, meli, reli, mabwawa nk. miradi ambayo anadhani bila yeye hakuna wa kuiendeleza.

Mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu mara nyingi amekuwa akisema akichaguliwa kitu cha kwanza ni kujenga mifumo bora ya utawala wa sheria unaozingatia haki za binadamu na utawala bora.

Kiufupi (summary), nionavyo mimi, uchaguzi wa mwaka huu tunachagua kati ya Utu na Vitu.

Nini kipaumbele chako.
 
Unajua kuna namna nyingi ya kuhitaji

Ili uweze kuwa huru unaweza kumhitaji lissu

Ili uweze kusogea mbele kimaendeleo utamwitaji magufuli

Hawa watu wawili sio wanafiki na hawajui kuficha maneno kama ilivyo kwa wanasisa wengine
 
SUSTAINABLE DEVELOPMENT MATTERS.

Sioni haya maswala ya kuambiwa eti mnafunga mkanda kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
TANZANIA BADO INAITAJI MTU WA NAMNA YA MAGUFURI ATA KWA MIAKA KUMI IVI KWA MAANA ANGALAU ILA UYO MWENGINE HAPANA HANA SIFA HATA ...
Ndiyo kusema utawala wa sheria usubiri tumalizie bwawa la stieglas gorge kwanza.
 
Haumhitaji wewe sio watanzania tunaopenda maendeleo.

Maendeleo yalianzishwa na wakoloni, sasa hivi ni muendelezo wa yoyote atakayekuwa madarakani.
 
Maendeleo yalianzishwa na wakoloni, sasa hivi ni muendelezo wa yoyote atakayekuwa madarakani.
Maendeleo tulianza sisi kabla hata ya ujio wa wakoloni.
 
Back
Top Bottom