Bila shaka wewe ni mkwewe au ulikuwa unanufaika nae kwa namna moja ama nyingine. Wacha vyombo husika vifanye kazi yake, kama yuko safi mbona haonewei mtu hapa....... naamini nae ana wanasheria, kila kitu kitakwenda sawa, acha kuwaza kitoto Tajiri Tanzanitevip!
Binafsi nimekuwa mtanzamaji na msomaji sana katika hili swala la Ole Sabaya. Baada ya kuona mashambulizi yanakuwa makubwa..nikaona nilifanyie utafiti na kujiuliza maswali ya msingi.
Ni kweli kuna maneno mengi sana yameongelea kuhusiana na Sabaya ila katika hizi tuhuma tuziangalie kwa mapana na kujiuliza maswali ya msingi.
Binafsi nimeshaona clips nyingi Ole Sabaya akiwasaka wafanyabiashara wanaibia serikali serikali na kwa kukwepa kodi..mkwepa kodi ni sawa na mwizi kama mwizi mwingine..katika nchi za ulaya ni anapewa adhabu kubwa sana.
Pia nilishaona clips mbalimbali akitatua migogoro ya ardhi jambo ambalo limeleta suluhu kwa wananchi walionyima haki yao kwa muda mrefu...nimeona clip nyingi sana...sasa swali la msingi la kijiuliza... kati ya Sabaya na hao wafanya biashara wanaokwepa kodi na Jambazi?
Ninachokiona hapa kuna hoja za chuki dhidi ya huyu bwana zenye elements za kisiasa na ukabila.
Ukirejea clips ya Lema na Sabaya kuna kitu cha kujifunza wakati Lema anasema community ya kichagga..kwenye hiyo sentence kuna vitu vya kujifunza.
Harakati ambazo zilikuwa zikiendelea mitandao dhidi ya Sabaya ni harakati za kumuondoa hai kwasababu amekuwa mwanga na mtu jasiri dhidi watu wachache wenye nguvu katika ile jamiii walikuwa mungu watu dhidi ya watu wanyonge.
Lakini pia embu tujaribu kuchukua sample ya watu wanaorusha sana tuhuma dhidi ya Sabaya utakuta ni watu wenye idiology moja kisiasa au utakuta ni kabila moja.
Hata hao wanaorusha tuhuma sio wasafi sana katika uongozi wao ni watu waajanja wajanja.
Namshauri mama na Rais wangu Samia aangalie hili swala kwa mapana yake. Kuna kikundi cha watu wenye interest naona wanafanikiwa kummanipulate mama kwa interest za kikabila na za kisiasa.
Pia naamini Sabaya hakuwa msafi katika uongozi wake ila naona exaggeration kwenye tuhuma zake.
Naomba Melo kama wewe ni mkurugenzi wa hili jukwaa uwe makini sana kwasabsbu kuna madmin wanaukabila na usiasa na wakishaona thread isiyoendana na matakwa yao wanaunganisha ili mradi wavuruge maana husika ya thread kwa maslahi yao..NB Melo kunawatu waanza kuleta ukabila wa kishamba mpaka jf...au kama umesha muuzia m#shi niache kuandika thread kuanzia leo.