Uchaguzi 2020 Ole Sabaya anategemewa na CCM kumng'oa Mbowe jimbo la Hai

Mkuu Mushi, umetoa maelezo marefu lakini nadhani ama sio mkazi wa Hai wa kila siku au umeambiwa kwa ushabiki.

Nijuavyo mimi ambae nina shuguli zangu hapa na siwezi kukosa kuwepo Hai kwa uchache siku 8 kila mwezi na nina wafanyakazi zaidi ya 35 ambao wako Wilaya ya Hai, huu ufuatao ndio ukweli; CCM hawana mtu mzuri wa kumuondoa Mbowe kwa sasa hivi lakini Mbowe Hai wamemchoka, na hana mvuto tena.

Katika kata zifuatazo hii ndio muono wangu na Wamachame wengi, na sio kweli unavyosema kuwa hawajali. Wamachame idadi kubwa wameanza kuamini Mbowe ndio anasababisha dhiki walizo nazo na ukosefu wa kazi japo kuwa sio kweli.

Ila Wamachame wamechoka kabisa kuendelea kubaki upinzani na hasa Wakazi wa kudumu wa Wilaya ya Hai. Na Mbowe anaheshimika na kupendwa zaidi nje ya kilimanjaro , kuliko Kilimanjaro kwenyewe.

Uchambuzi wangu kata kwa kata za Wilaya ya Hai upo kama ifuatavyo.

1) Barangata --- Hapa Mbowe hapati kitu.
2) Boma la Ngombe -- Hapa Mbowe hapati kitu.
3) Bondeni Boloti -- Hapa Mbowe hapati kitu.
4) Engare Nairobi -- Hpa Mbowe hapati kitu.
5) Kibohehe -- Anaweza kuwapindua, japo pagumu sana.
6) Kibongoto --- Hapa atafanikiwa.
7) Kibosho --- nusu kwa nusu.
8) Kware ---- anaweza kuwapindua.
9) Lemira ---- anaweza kuwapindua.
10) Lyamungu----- pagumu sana kwake.
11) Mabire --- anaweza kuwapindua.
12) Machame --- pagumu sana kwake.
13) Masama ---- anaweza kuwapindua.
14) Sanya Juu --- anaweza kuwapindua.
15) Shiri -- ana kazi kubwa,
16) Uru -- anakazi kubwa.
17) Uswaa ---- anaweza kuwapindua japo wamemchoka.
18) Weru Weru ----- anaweza kuwapindua.

Pamoja na unavyo sema kuhusu makanisa, lakini naamini Hai ni jimbo lina waislamu wa kutosha ingawa Wakristo ndio wengi zaidi.
Wilaya ya Hai inafanana kidogo sana na Jimbo la Mwanga kwa hali ya kidini, kwa Mkoa wetu wa Kilimanjaro.
Ajitayarishe kwa mapambano hali ni tete sana kwa Mbowe.
Q
Kibongoto na Sanya juu ziko jimbo la Siha.
 
Sabaya hana lolote zaidi ya kiburi na roho mbaya kama mfuasi wa Ibilisi.

Yaani kati ya watu wanaoinajisi taasisi ya urais iliyomteua, basi ni Sabaya.

Kuna maisha baada ya uongozi, naamini iko siku tutakuwa naye street.

Mimi CCM ila nachukia sana viongozi wanaofanya siasa za kukomoana na visasi na ulaghai

👆 Kwa taarifa tu na erufi kubwa...

AJIFUNZE KWA YALIYOMKUTA MTIA NIA MAKONDA.... tupo nae street.

CHEO NI DHAMANA MTU HAZIKWI NACHO..
 
Hapo kwenye udhaifu wa Mbowe unaposema hakuna jambo kubwa ambalo amelifanya kwake ningependa uelezee ulitaka afanye jambo gani?

Nahisi umeshindwa kuelezea zaidi hiyo pointi kwasababu siamini kama mbunge anaweza peleka maendeleo jimboni yeye binafsi bila kuungwa mkono na serikali, tena serikali hii inayomchukia Mbowe bila sababu.

Sabaya hawezi kumtoa Mbowe Hai, labda amuondoe Mbowe kwa kumvurumishia mawe kama anavyofanya na hao wahuni wake.
 
Hapo kwenye udhaifu wa Mbowe unaposema hakuna jambo kubwa ambalo amelifanya kwake ningependa uelezee ulitaka afanye jambo gani?

Nahisi umeshindwa kuelezea zaidi hiyo pointi kwasababu siamini kama mbunge anaweza peleka maendeleo jimboni yeye binafsi bila kuungwa mkono na serikali, tena serikali hii inayomchukia Mbowe bila sababu.
Sabaya ameharibu mashamba ya Mbowe, JPM amemvunjia billcanas na kufanya pawe parking, sasa Mbowe hata kutoa gari la wagonjwa CCM Hai wapo radhi wamama wafe nyumbani kuliko gari lipokelewe, na ikawa hivyo , na bado walionyweshwa mataptap wanashangilia hawajui ndugu zao ndio wanakufa, hii nchi ilishalogwa
 
Mwaka huu mwanzoni kabisa niliwaambia kuwa Jimbo la Hai ni mojawapo ya Jimbo ambalo litavuta hisia za Siasa za Tanzania, hapa hakuna kulala, ni mwendo wa mahuburi, ngumi na jino kwa jino. Hii Ni kutokana na umuhimu wa Jimbo hili kwa Upinzani na kwa CCM. Kwa Upinzani ndipo anapotokea Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Yaani hawatokubali inyeshe mvua liwake jua kupoteza eneo hili kwani itakuwa aibu ya mwaka. Kwa CCM hapa wanataka kumpiga mchungaji na Kondoo watawanyike, wanajua kabisa ukitaka kumuua nyoka gonga kichwani....

NGUVU YA CCM.

Mipango ya Ushindi wa CCM unaanzia Kichwani kwa Ole Lengai Sabaya, yaani CCM kwa ujumla wanategemea Ole Sabaya awasaidie kumngoa Mbowe pale Hai. Sabaya ndiye DC anayeongoza eneo gumu kuliko yote kati ya maDC wote nchini yaani kupewa jukumu la kuongoza eneo ambalo anatokea Kiongozi mkuu wa Upinzani sio kazi ndogo.

Jukumu la pili alilopewa au alilojipa Ni la kuhakikisha Mbowe hashindi Hai jukumu ambalo Ni zito ambalo hata Bashiru Ally Kakurwa hawezi kulibeba.

Sabaya anapambana kweli matokeo yake anaweza kuumia au akaishinda hii vita, lazima impact itakuwa aidha aumie au ashinde. Niliwahi kusema Kama hatopata usaidizi huyu kwa Jasusi Mbowe ataonekana hafai hata U DC. Pale CCM nani anaweza kuja kuwaongoza watu wanaomuita Mbowe kaka na akaeleweka? Mbowe Hai sio Mbunge tu Bali Ni kaka yao Kama wanavyomuita.

Nguvu ya Pili ya CCM Ni kuwa Sabaya anajitahidi Sana kufanya Siasa na watu wa Tambarare. Siasa maendeleo, siku za karibuni tunaona barabara zikichongwa, hospital ikijengwa nk. Sabaya anajitoa sana kuhakikisha image ya Serikali na Chama inaelewaka Hai. Aidha kwa kutumia mbinu nzuri au mipango Michafu lakini anapambana sana.

UDHAIFU WA CCM

Udhaifu CCM ni kwamba imejisahau, wanamtegemea Mkuu wa Wilaya afanye Kila kitu. Haitawezekana peke yake awaletee Ushindi halafu pia Ni kinyume cha Sheria mkuu wa Wilaya kufanya Siasa za wazi. Ndio maana hata waosema ni yeye ametuma watu wamshambulie Lisu hawana ushahidi wa moja kwa moja.

Udhaifu wa pili Ni kwamba CCM Haina network ambayo Mbowe anayo. Nitaelezea hapa chini nitakapokuwa naelezea nguvu za Mbowe.

Udhaifu wa tatu ambao hauonekani Ni Kifo cha Mzee Mengi. At least Mengi alikuwa Ni mmojawapo ya watu ambao walikuwa wanaweza kuwaambia Viongozi wa Dini Jambo wakalisikia, au hata jamii yake (Wachaga) jambo na wakamsikia.

Udhaifu wa nne Mkoa wa Kilimanjaro Ni Mkoa ambao hauna Agenda ya kuombea kura. Yaani hakuna Jimbo ambalo utapata kura kwa kuahidi hospital, Au umeme, au maji au barabara. Hivi Ni vitu ambavyo vipo toka uhuru. CCM Mara nyingi imekuwa ikitumia agenda hizi kuombea kura kwenye majimbo ya Kilimanjaro hizi sio agenda.

NGUVU YA CHADEMA.

Mbowe karelax kabisa sidhani hata Kama anawaza Sana kuhusu Ushindi wake. Nguvu kubwa waliyoanayo Chadema Ni aina ya mgombea waliyenaye. Mbowe kwa Sasa ndiye mhimili wa Siasa za Upinzani nchini.

Uimara wa Pili wa Chadema Hai Ni network ambayo Mbowe anayo. Mbowe anaungwa mkono na taasisi za Kidini lipo chini ya capert na ndio wanaompa nguvu sana, Mbowe anaungwa mkono na wafanyabiashara wengi toka Hai, Mbowe anaungwa mkono na hata baadhi ya wanaccm waliopo Hai.

Uimara wa tatu ni desturi na Mila za Kabila la wachaga. Kabila hili likishamuamini mtu sio rahisi kuwabadili. Hawaogopi kujilipua kwa kitu wanachokipenda. Mbowe anapendwa Sana na jamii yake. Hawa ndio wanaomuitaga Kaka si rahisi kuwabadilisha mtizamo, watakuchekea usoni lakini kwenye Sanduku la kura watakuadhibu tu. Ndio maana Kabila hili linaongoza katika kuendesha Siasa za Upinzani. Ndio Kabila linalotoa Viongozi wengi wa vyama vya Upinzani nchini. Hii Ni hulka yao kwa maana hiyo ukitaka kuwawin lazima Kwanza wakupende na wakuamini.

Uimara wa nne wa Mbowe Ni kulitawala jukwaa kwa Hoja. Ukimruhusu huyu mtu akupige kwa Hoja atakuua kabisa.

UDHAIFU WA MBOWE.

Udhaifu mkubwa wa brother Mbowe hakuna Jambo kubwa ambalo amelifanya kwenye Jimbo lake.

Pili eneo analotokea si rafiki Sana kwa Siasa za sasa. Mbowe anatokea eneo la milimani, Kuna tetesi kuwa eneo la tambarare ambalo Lina watu wengi nao wameanza kuwaza kutoa mtu wao kuwa Mbunge. Hii Ni kwa sababu eneo hili halijaendelea kwa Sana Kama eneo la Milimani hivyo Wana hasira.

Udhaifu wa Tatu Mbowe amejikita zaidi kwenye siasa za kitaifa na kusahau watu wake. Huu ni udhaifu kwa wabunge wengi wa Upinzani.

Swali ninalojiuliza Sabaya atauweza huu Mbuyu ambao umeshindikana Miaka na Miaka?

Ukitaka kumshinda Mbowe kirahisi tenganisha urafiki wake na Kanisa, tenganisha urafiki wake na wafanyabiashara wa Hai. Mwisho kabisa CCM ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa wakitaka kushinda Hai wamsaidie Sabaya, peke yake hatoweza.

Ole Mushi
0712702602.
Asante kwa ushauri mkuu .. chadema hai tutahakikisha mbowe anarudi tena bungeni na majimbo yote nchi nzima
 
Sabaya atang'oka yeye.
 
Hiyo ni ndoto yako, hat sie tuliemueka hapo tunajua, Ile sio size ya Mbowe, bali tuliamua kumuweka chakaramu Mmoja asiye na haya hapo hai, ili amsumbue na kumvunjia heshima Mbowe, na anatimiza kazi aliyotumwa.
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.

MITANO YA MKONO WA CHUMA, INATOSHA...
 
Attachments

  • Makonda ajitangaza mla raha namba moja duniani..mp4
    857.8 KB
Sabaya ameharibu mashamba ya Mbowe, JPM amemvunjia billcanas na kufanya pawe parking, sasa Mbowe hata kutoa gari la wagonjwa CCM Hai wapo radhi wamama wafe nyumbani kuliko gari lipokelewe, na ikawa hivyo , na bado walionyweshwa mataptap wanashangilia hawajui ndugu zao ndio wanakufa, hii nchi ilishalogwa

Nilipenda sana nichangie kuelimisha lakini naona hapa unajenga uwongo zaidi, nadhani unatengeneza propaganda tuu. Wana Hai wengi ambao ni walala hoi tuu wanataka mabadiliko, na wao mabadiliko ni kuingiza CCM Jimbo la Hai.

Walicho fanikiwa sana ni wao kusimama katika upande wa wananchi wa kawaida wa Hai na sio sisi wafanya biashara Wenye makampuni ya kupandisha watu milimani na wenye mashamba ya kibiashara.

Kwa kuwa zile kero zilizo kuwa zikiwasumbua sana, zote zimeondolewa. Sabaya anachukiwa sana na wenye uwezo lakini wanahai wengi wa kawaida wanamuona sabaya kama muokozi wao, anapendwa sana na watu wa kawaida.

Amehakikisha malalamiko ya Waislamu na mali zao, ugomvi wa Misikiti na shule, mashamba na mali zao imesimamia kikamilifu na ameimaliza . Ila siasa kuna uwongo mwingi tukubali hilo.

Japo wengi wenu mmefungwa macho, Mh Mbowe sio tajiri hivyo kama watu wa sehemu zingine mbali ya Wanahai wanavyo aminishwa. Watu wa Hai tunafahamu vizuri, ila siasa ni pamoja na uwongo.
 
Mbona hueleweki unataka kusema nini? Be specific
 
Yaani tambarare(boma ngombe)kuna watu wengi kuliko Nkuu, Makeresho, Lyamungo Sind, Ndoo, Kati, Narum na Kilanya ?
Acha zako
Asante...kwanza Mbowe hajatokea milimani, kwao ni Lambo jirani kabisa na Machine Tools(Njiapanda ya Machame)all in all hakuna Ccm itakuja kutawala Hai mpaka dunia inaisha..
 
Halafu kasema hajafanya kitu Hai huku anasema huwezi pata kura kwa hoja za umeme, maji,barabara na mahospitali maana zipo toka uhuru...Sasa hicho kitu ambacho hajafanya ni kipi??
Hapo kwenye udhaifu wa Mbowe unaposema hakuna jambo kubwa ambalo amelifanya kwake ningependa uelezee ulitaka afanye jambo gani?

Nahisi umeshindwa kuelezea zaidi hiyo pointi kwasababu siamini kama mbunge anaweza peleka maendeleo jimboni yeye binafsi bila kuungwa mkono na serikali, tena serikali hii inayomchukia Mbowe bila sababu.
 
Hapo kwenye udhaifu wa Mbowe unaposema hakuna jambo kubwa ambalo amelifanya kwake ningependa uelezee ulitaka afanye jambo gani?

Nahisi umeshindwa kuelezea zaidi hiyo pointi kwasababu siamini kama mbunge anaweza peleka maendeleo jimboni yeye binafsi bila kuungwa mkono na serikali, tena serikali hii inayomchukia Mbowe bila sababu.
Lkn anakiri kuwa, mkuu wa wilaya anajenga barabara na hospitali.
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.

MITANO YA MKONO WA CHUMA, INATOSHA...

Samahani,Nyerere alikuwa mwanademokrasia?
 
Mleta mada Hai inakuwaje wilaya ngumu kuliko zote Tanzania??
Vigezo vipi umetumia??
Ina ukame, ni jangwa, milima haifikiki, hakuna barabara, hakuna umeme, hakuna shule wala zahanati, hakuna huduma za maji???
Fafanua ugumu wa hiyo wilaya!

Uwepo wa Mbowe kama mbunge hakuifanyi hiyo wilaya iwe ngumu kuliko zote.

Ila naona uneducated kuacha namba za simu, hope watakutafuta wahusika!

Everyday is Saturday..........................😎
 
Wachaga siyo wapumbavu wamsikilize masai mtu wa kupita wamuache Mbowe mtoto wa nyumbani ambaye amewasaidia mambo mengi. Uchagani kuna elimu pia wanathamini mtu wa nyumbani kuliko mpita njia.
 
Sabaya hana lolote zaidi ya kiburi na roho mbaya kama mfuasi wa Ibilisi.

Yaani kati ya watu wanaoinajisi taasisi ya urais iliyomteua, basi ni Sabaya.

Kuna maisha baada ya uongozi, naamini iko siku tutakuwa naye street.

Mimi CCM ila nachukia sana viongozi wanaofanya siasa za kukomoana na visasi na ulaghai
Unachuki binafsi
 
Back
Top Bottom