Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ndiyo Taarifa ya uvunguni ambayo imevuja , kwamba yule kijana katili aliyetesa watu na kupora pesa za wafanyabiashara wa Hai anapanga kukimbia nchi hii baada uchunguzi dhidi yake kumkalia vibaya .
Lengo la kuleta Taarifa hii nyeti ni kuvitaarifu vyombo vinavyomchunguza kuhakikisha wanamuweka kwenye Zero distance ili asiwaache solemba na kukimbilia Nairobi ambako Sheria za Kenya zaweza kumlinda na asiletwe Tanzania kujibu mashitaka yake , Tafadhalini sana vyombo vya dola msije mkathubutu kumsaidia Sabaya kutoroka , hatutawaelewa na huenda mkasababisha machafuko , mwacheni afikishwe Mahakamani akajibu tuhuma zake na akawataje wote alioshirikiana nao .
Mara nyingi sana humu JF kupitia jukwaa hili hili , mimi binafsi na waungwana wengine wengi sana tumesisitiza sana vijana wanaopata bahati ya kuteuliwa kwenye uongozi kutumia uongozi wanaopewa kwa kutenda haki , wahakikishe wanafanya kazi zao kwa mujibu wa katiba ya nchi , wasithubutu kutekeleza unyama hata kama wametumwa na mkubwa , Biblia ilishaonya tangu enzi kumtegemea mwanadamu (YEREMIA 17:5) , Kila aliyetenda kinyume cha Katiba tumwache avune alichopanda .