Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Kuna kamchezo hapo....ile kwanza anaweza akapigwa fine au kifungo....zilizobakia zote ni fine pia....analipa zote huyu alikitoa mhanga anewekeza 3bil kwa wafanya biashara Arusha na Nairobi.....alikuwa anajua anafanya nini
Kapiga sn rushwa
 
Ni vema ukafanyika uchunguzi yakinifu kabla ya kupeleka kesi Mahakamani,kuepuka masuala ya uchunguzi haujakamilika au kubadili mashitaka mara kwa Mara.
Weledi upewe nafasi yake.
 
Kuna kamchezo hapo....ile kwanza anaweza akapigwa fine au kifungo....zilizobakia zote ni fine pia....analipa zote huyu alikitoa mhanga anewekeza 3bil kwa wafanya biashara Arusha na Nairobi.....alikuwa anajua anafanya nini
Nani kakwambia kesi ya Unyang'anyi kwa Tanzania adhabu yake ni faini

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye hizi case zote mbona Nandi apeleki ya kwake?

Kama Nandi ulimsamehe sabaya Tuambie
 
Kuna kamchezo hapo....ile kwanza anaweza akapigwa fine au kifungo....zilizobakia zote ni fine pia....analipa zote huyu alikitoa mhanga anewekeza 3bil kwa wafanya biashara Arusha na Nairobi.....alikuwa anajua anafanya nini
Sijui kifungu gani cha sheria kitatumika kumpiga faini mnyang'anyi wa kutumia silaha labda useme mahakama haitomtia hatiani.
 
Bado mengine ya mkoa wa kilimanjaro yanamsubiria,arusha kwa wahindi kawapiga sana huyu mchambia rungu
Yote yanaivua nguo serikali kama kweli yalitendwa. Usalama wa nchi unashikiliwa na usalama wa taifa, idara iliyo chini ya rais. Haiwezi kuwa kweli taarifa hizi zilikuwa hazimfikii rais. Na kuacha kuchukua hatua kunaashiria alifaidika nayo. Usalama wa taifa ulichukua hatua gani?
 
Sijui kifungu gani cha sheria kitatumika kumpiga faini mnyang'anyi wa kutumia silaha labda useme mahakama haitomtia hatiani.
Mipango yao tu.....usishangae kwa lolote yule jambazi kabisa basi tu tusubiri Oct 1
 
Mwandishi rekebisha uandishi huu kwa sababu unaweza kuleta taharuki. DPP si sehemu ya mahakama, ni mlalamikaji - jamhuri. Sio sahihi kusema anaweza kuipa mamlaka mahakama ya chini kusikiliza keshi!

Kilichotokea ni kuwa DDP aliomba kesi hii isikilizwe Arusha na Mahakama yenye mamlaka ikatoa kibali cha kusikilizwa kwa kesi. Jamhuri imesoma mashtaka hayo na kueleza ruhusa hiyo ili ku-preempt challenge ya mshitakiwa kuwa mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hii!!

Iwe wazi kuwa DPP ni mshitaki na kwa mahakama za chini huwakilishwa na polisi wakaoitwa PP (public prosecutor).
 
16 September 2021
Arusha, Tanzania

SABAYA MAHAKAMANI "ALISIMAMA NJE YA BENKI MROSO AKATOA MIL. 90"




KESI YA UHUJUMU UCHUMI NAMBA 27 / 2021
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai lengai ole Sabaya pamoja na wenzake sita wanaoshtakiwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi waameanza kusomewa maelezo ya awali huku jamhuri ikitarajia kuleta mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16...
....
Source : Millard Ayo

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imeelezwa kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita walimkamata na kumpeleka mfanyabiashara, Fransis Mrosso, katika Benki ya CRDB tawi la Murombo na kumshinikiza awape Sh90 milioni baada ya kumtuhumu kufanya biashara bila kutoa risiti na kuingiza vipuri vya magari bila kufuata taratibu.

Akisoma maelezo ya mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili Sabaya na wenzake leo Alhamisi Septemba 16, 2021, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia amesema Sabaya na wenzake waligawana fedha hizo baada ya kuzichukua benki. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda.

Amesema siku ya tukio Januari 22, watuhumiwa wote wakiongozwa na Sabaya walienda katika gereji inayomilikiwa na Mrosso eneo la Mbauda jijini Arusha na walipomkuta walimwambia yeye ni mkwepa Kodi.

Wakili Kwetukia alidai Sabaya na wenzake walimtuhumu Mrosso kwa kuingiza vifaa vya magari kutoka Dubai na Nairobi kupitia Zanzibar bila kufuata utaratibu wa kulipa kodi.

“Kufuatia kumpatia tuhuma hizi, mtuhumiwa wa kwanza (Sabaya), ulimtishia Mrosso kwamba asipofanya kitu mtampatia kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Kufuatia kumtishia huko na bila kufahamu nini afanye, Mrosso alimuuliza Sabaya ni kitu gani anatakiwa kufanya,”alidai.

“Sabaya alimwelekeza atoe Sh 90 milioni kwa washitakiwa wenzake ili awe huru kutokana na tuhuma ambazo wamempatia. Pale mwanzo Mrosso alikataa hilo lakini kutokana na vitisho na pasipokujua kuwa ni matokeo gani yatafuata alikuja kukubali kulipa kiasi hicho,” alidai wakili huyo wa Serikali.

Wakili Kwetukia aliendelea kuieleza mahakama kuwa watuhumiwa hao wakiwa na Mrosso walikwenda benki ya CRDB, tawi la Kwa Morombo ambapo mhanga huyo alitoa kasi hicho cha fedha katika mazingira ya kulazimishwa akiwa katika usimamizi wa karibu wa watuhumiwa wenzake na Sabaya.

Mbali na Sabaya, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka huu, ni Enock Mnken (41), Watson Mwahomange (27) na John Aweyo, wote wakazi wa Arusha.
Wengine ni Sylvester Nyegu (26), mkazi wa Bomang’ombe, wilayani Hai, Jackson Macha (29), mkazi wa Moshi na Nathan Msuya (31) mkazi wa Msangara Kilimanjaro. Wote wanatetewa na Mawakili Mosses Mahuna,Charles Adiel,Sylvester Kahunduka na Fridolin Gwemelo
 
Hii ni kesi nyingine tena?
Nilijua ni unafiki wake kumbe sio Lile chozi ni halali alie vile ile siku pale Chato
Inapendeza kuvuna ulichopanda!
 
Back
Top Bottom