Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Tatizo la kutokuzingatia job discription linaweza kutusumbua kwa muda mrefu.
 
Mbona hamna la ubakaji?
Nadhani ushahidi wake ni mgumu kuupata labda kama kamera zingerekodi.
Hayo yanamtosha kama ni mtu wa kujifunza..
Miaka 34 ,bado kijana sana ,ana muda wa kujipanga.
 
🤔😥😣😇🤗😏🙄😶☺😑😐😐
Rise And Fall Of The Kingdom!!

Ahadi Ya Mwana Tanu
Cheo Ni Dhamana,Rushwa Ni Adui Wa Haki
 
Lazima muanze kujiandaa kisaikolojia mjue kbs mmepanga kufanya Nini endapo huyu mnayemuona Ni mtesi wenu hatafungwa..tatizo lenu Ni Moja tu hamuwajui watu wa Kanda ya kaskazini tabia zao..ukitaka kuwajua tabia zao angalia maisha ya mbowe,sumaye,lowasa n.k angalieni walichowafanyia..kwanza Mimi nashangaa eti mnaona ajabu kwa aliyekuwa kiongozi kupelekwa vyombo vya dola mnasahau hata Kuna mawaziri wa awamu ya tatu na mabilionea fulani washapelekwa rumande na wengine kufungwa kabisa.Sasa sijui mtaandamana au mtafanyaje?.

Kwanini msishupalie na vitu vyingine mfano watoto wenu kupatiwa ajira maana Ni haki Yao na pesa zipo nyie mnakomalia ishu zisizo na maana kivile.Simtetei sabaya lakini najua Kama kijana mwingine yoyote mihemko Ni Jambo la kawaida huenda alipokuwa DC alikuwa kweli akilewa na kutongoza wasichana wa watu ndo maana akajengewa chuki lakini Hilo sio tatizo kisheria.ila hili la kusema eti ameonea wafanyabiashara Hili hapana Bali alikuwa akitimiza majukumu yake na hakuwa peke yake walikuwa wanaenda sehemu na kamati yote ya ulinzi ya wilaya kwa hivyo Hapo poleni mtaangukia pua mapema sana.
Kaa kwa kutulia bwana wako zama zake zimekwisha.
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Na hili la kuvamia hoteli usiku wa manane na akitumia magari yenye plate namba za UN vipi?
IMG_20210605_110756.JPG

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Haya halafu mseme Magufuri alikuwa mzalendo,tuliibiwa sana kipindi cha Magufuri,Tulidhulumiwa sana kipindi chake na kunyanyaswa sana utafikiri Tanzania siyo nchi yetu kwa kukumbatia vibaka kama Ole Sabaya na Makonda.
Kwaiyo unaamini jamaa(Sabaya na Hayati? Wameiba simu ya tochi na elfu 35?

Ndio hujue hata kama jamaa wana makosa sio kwa kuiba simu ya kitochi,waendesha mashtaka wa kitanzania wanateleza sana.
 
Do you think JPM sent him to do those criminal things???
-Na 'ujinga wako' kama jinalo,
Tusichoshane kwa 'Kinge' wengine hadi tulewe.

Nipe jibu;
Unadhani huyo uliemtaja hakuwa akipata angalau tetesi za matendo ya wateule wake?
kama ndivyo itakuwa maajabu ya Dunia.

Wakati mwingine inahitaji akili ndogo tu kuelewa nani anabariki nini wala usitumie 'karoli' nyingi kufikiri.

Tafakari.
 
Wapo wapi wanaharakati wa haki za wanawake, kuongelea mabinti na wanawake waliobakwa na huyu jamaa. Mbona wanakuwa kimya katika mambo ya msingi ila kazi kupiga kelele mbunge wa kike kutolewa nje sababu ya kuvaa suruali.

Hebu wajitokeze waje kupambana na huyu jamaa.....
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
aaanh...MAKONDA JEEH?
 
-Na 'ujinga wako' kama jinalo,
Tusichoshane kwa 'Kinge' wengine hadi tulewe.

Nipe jibu;
Unadhani huyo uliemtaja hakuwa akipata angalau tetesi za matendo ya wateule wake?
kama ndivyo itakuwa maajabu ya Dunia.

Wakati mwingine inahitaji akili ndogo tu kuelewa nani anabariki nini wala usitumie 'karoli' nyingi kufikiri.

Tafakari.
Umenikumbusha mbali hapo kwenye karoli
 
Back
Top Bottom