Ole Sabaya: Doa jeusi kwa utawala wa Hayati Magufuli

Mkuu mtaje tu huyo Sabaya clone.
Linalohitajika ni mtu kulalamika rasmi tu.
 
Tatizo yeye mwenyewe kakili kosa Sasa hapo ni ngumu kushinda hata kama anaenda kukataa lufaa.Hii hukumu tayali imeshakua ngumu sana kwake Maana kama hukumu isingetoka kama ilivotoka basi ingehalalisha Serikali ilikua ndo yenye kutoa hizo oda za kuumiza watu Sasa basi kwa hii hukumu Serikali imekwepa Hilo doa.Nampa pole nyingi lakini ukishakubali kutumika Namna hiyo basi mwisho wa siku Dola hukutelekeza ili isichafuke ,Sabaya kavuna alichopnda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waanze kukamatwa usalama wa taifa pia maana ndio waliofanya vetting
 
Many of you writes pro or otherwise on the function of governments. For your information : all governments in the world's are criminal enterprises, that's why all heads' seek protection of the law while discharging it's duties.

There is no government enterprise that is people centered, all projects are implemented to serve the best interests of those in power, unless you are lucky that your interests accidentally converge with theirs. ..
 
 

Nuremberg trials iliweka precedence kwamba kutumwa na mamlaka za Juu kufanya makosa hakimuondolei aliyetenda hilo kosa hukumu.
Nuremberg trials ni mashtaka maalumu kwa wale wote waliohusika na mauaji ya waisrael uliofanywa na wajerumani chini ya uongozi wa Adolf Hitler.
katika hukumu hizo majenerali wa jeshi la ujerumani walioshiriki mauaji hayo walijitetea kwamba walikuwa wanatekeleza maagizo kutoka kwa Adolf Hitler na hayakuwa matakwa yao.
Wote walifungwa utetezi wao huo haukukubalika.
Hao mawakili wa sabaya sijui walikuwa hawafahamu kuhusu hizo kesi study za Nuremberg.
 
Ifike mahali wana ccm wajue kwamba kinachopiganiwa na chadema yaani katiba mpyaa ni muhimu sana kuliko wanavodhani ….Sabaya kaingia matatizo kwa kutumika tu kama chambo ,kutii maagizo kutoka juu..vijana wa ccm still now bado mnatumiwa direct au indirect ifike mahali mkubali katiba mpya inatakiwa mjue katiba mpya ni salama kwenu na itakua kinga kwenu muache kutumika…aliekua anamtumia sabaya hayupo leo familia ya sabaya inatokwa na machozi kwa matunda waloyafaidi kwa muda mfupi…katiba mpya ni sasa.
 
Yule wakili wake hajitambui, jana anahojiwa anasema hukumu iliyotoka ni nzuri na yeye ameipenda, sasa kama hukumu ni nzuri unakata rufaa ya nini?
 
Hafungwi mtu hapa. We all know that... Wanapoteza pesa ya serikali bure tu.
 
It is pity kwamba Makonda hajachunguzwa. arrogance aliyokuwa nayo wakati ule, inawezekana yapo maovu alitenda
 
Crap. Worth for the fools.

You are one of them. You know why? Because even kwa Yale maswali ambayo hujaulizwa una Majibu. Kwenye kichwa chako. Jina Mbowe Liko Programmed kwenye mambo matamu tu.
 
Mwisho wa Ubaya AIBU! Hata wanaojipirikicha kumuinua Mwendazake wanatia kinyaa! Yule alikuwa wakala wa shetani kwisha!
 
Bado ameomba kukata rufaa atajisafisha tu.

Hapa kazi tu.
Rufaa atachomokaje na ameshakiri aliyoyafanya.. kwamba ni amri kutoka juu, j kuna kifungu cha kuhalisha uovu kwa kigezonhicho?
 
Ni bora anayepanga kuliko anayeharibu amani ya nchi tena live kabisa na kupata baraka kutoka kwa magufuli.
 
Hapana wote wanahusika ama kwa kuruhusu, kwa kutokuchukua hatua au kutoachia madaraka kupinga vitendo hivyo. Kwa mantiki unayoisemea hiyo basi hizo jinai zinazofanana na aliyofanya Sabaya hazitakoma. Zinatakiwa zikome kama tunataka Tanzania iwe sehemu ya jamii ya ulimwengu unaoendeshwa kwa mujibu wa utawala wa sheria. Heshima ya Tanzania tuliyokuwa nayo ndiyo inaporomoshwa na uongozi unaotafuta sababu za kukwepa kuwajibika ipasavyo. Mbona Mwenyekiti wetu wa CCM mstaafu, Mzee Mwiny,i amekuwa wazi kwenye kitabu chake jinsi alivyowajibika kwenye vifo vya mahabusu wa Shinyanga wakati yeye hakuhusika moja kwa moja. Cha kushangaza hayo madoa meusi ya Hayati Magufuli yanayoharibu mengine mazuri aliyotufanyia Watanzania bado yanaendelezwa na uongozi wa sasa hata wakati aliyeanzisha hayupo! Simwelewi mtu ye yote mwenye akili ya wastani na ana uwezo wa kusoma historia anaweza kuyaendeleza akawa anakwenda Kanisani au Msikitini au Umoja wa Mataifa kutoa hotuba! Anakwenda kufanya nini!? Mwenyezi Mungu apishe mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…