Ole Sendeka: Waziri Pindi Chana anataka Simanjiro, Ngorongoro na Longido kuwa Mapori ya akiba. Wamasai hatutakubali kamwe!

Hayo masilahi mapana ni yepi sasa, kwa upande wa Ngorongoro? Impact kubwa ni ccm, waziri na rais wa nchi? Au una maanisha, wanyama?! Kwamba nchi inapata kipato kupitia utalii?! Alafu hicho kipato kinafabyia nini taifa? Na taifa lisonge mbele kwa gharama za maisha ya wachache? Kama nchi ni yetu sote, ijengwe na sisi sote, siyo kwa damu za maasai wachache!
 
Masilahi ya nchi au ya Wazungu? Kuna masilahi ya nchi pale?
 
Hao Wamasai wapo kila kona ya nchi, mnasahau kwamba nao wananufaika na uhuru wa kila Mtanzania ana haki ya kuishi popote ali mradi asivunje sheria?.

Wao wenyewe wameshaona ni ngumu kubaki sehemu moja wakati wote.
 
..hatuna utamaduni wa kusikiliza hoja mpaka mwisho bila kumkatisha-katisha mchangiaji.

..mimi nimeona kuna kitu alichokuwa nacho Ole Sendeka lakini kwasababu ya kusakamwa na Spika ameshindwa kuchangia na hoja yake kueleweka.
Alikuwa anapotosha na akinukuu vifungu ambavyo havifahamu na anaweka tafsiri zake
 
Wamasai wanataka kujifanya ardhi ya nchi hii hasa Arusha ni ya kwao...KAmwe hii haitakubalika
 
Alikuwa anapotosha na akinukuu vifungu ambavyo havifahamu na anaweka tafsiri zake

..hili suala sio la kisheria peke yake, ni la kijamii, na kiuchumi vilevile.

..huu mgogoro umekuwa ukiibuka na kutulia ktk kila awamu ya Uraisi wa Tanzania.

..Kwanini hatujaweza kupata suluhisho la kudumu?
 
Wanaondolewa kimabavu na sio kuhamishwa maana hawataki.
Tafautisha kuhama na kuhamishwa. Kuhama ni kwa hiari, kuhamishwa ni kuondolewa kwenye eneo fulani, uwe unapenda au hupendi.

Ni mara nyingi haya yametokea kwa wwtu wengi,wa maene9 mengi na makabila mengi. Siyo ajabu jambo hilo kutokea kwa wamasai.
 
Wabena walihamishwa kutoka Njombe au walihamia wenyewe kwa hiari?
 
Alikuwa anapotosha na akinukuu vifungu ambavyo havifahamu na anaweka tafsiri zake

..waziri anafahamu vifungu vya sheria lakini halijui eneo la Ngorongoro na watu wake.

..mbunge hajui vifungu vya sheria lakini anawalijua eneo lake na watu wake.

..mkiona mpaka wabunge wa Ccm ambao kazi yao ni kusifia kila kitu wanawagomea jambo la serikali mjue kuna tatizo.
 
Yaani wilaya nne zigeuzwe mapori ili waarabu wawinde na kusafirisha wanyama wetu bila bughudha!! Na watu wanakuja na justification!!! Kweli rushwa inapofusha macho, hata hao waarabu wanatuna sisi manyani kweli
 
Maslahi gani hayo?
 
Serikali imeweka azima ya Wamasai kuondoka na inatakiwa hivyo..

Hoja ya msingi ni kwamba sheria ya kuchukua maeneo ya Vijijini iligutwa kwa mujibu wa Sendeka jambo ambalo ni uongo..

Ugumu wa Masai kuhama unatoka wapi ikiwa wananchi wa maeneo mengine wamehamishwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…