Ole wenu CHADEMA!

Ole wenu CHADEMA!

Asha unatisha bibie, laiti wanachadema wengi wangekuwa na moyo na mwamko kama wewe, mbona kazi ya kuing'oa CCM ingekuwa "smuuzi".

Kwenu viongozi wa Chadema:
kuweni na umoja kuliko wakati wowote ule, hivi sasa hili tufani lililokikumba chama chenu si la kupuuzia na kuact "individually", wakishammaliza Mbowe msidhani imekwisha hiyo Watakumalizeni na nyinyi, huu ni wakati wa kumsaidia Mbowe na kuwa naye bega kwa bega.

Asante Gamba la Nyoka.

Ni vizuri viongozi wa CHADEMA wazingatie ushauri wako. Lakini pia kila mmoja ajue kuwa wakimaliza na viongozi wa CHADEMA watahamia kwa kina "Mwanakijiji". Haya ni mapambano kati ya HAKI na UOVU. Kati ya UFISADI na UADILIFU. Ama sivyo basi tuwaachie wakina Mtikila waendelee kutusanii!

Asha
 
"CCM mpya haitakuwa na simile juu ya Mbowe..nakuhakikishia, baada ya miaka minne CHADEMA haitakuwa ile ile, wala Mbowe hatatamba tena," kilisema chanzo kingine.
Yanaelekea kutimia... I see, nimenyoosha mikono!
 
Yanaelekea kutimia... I see, nimenyoosha mikono!

Usijecheza na wale vijana wa mikocheni kwenye mambo ya siasa. Wanaweza wakaachia vingine vyote - mafisadi, loliondo, mikataba ya madini, mabomu ya mbagala, nk. Inapokuja kwenye suala la upinzani hapa Tanzania, hawajahi kulala hata siku moja.
 
From the trend, it seems that after every 5 years, 'they' allow someone to brag to the maximum then destroy him/her completely;
1995 it was Mrema and his NCCR
2000 it was Lipumba and his CUF
2005+ it has been Mbowe and his CHADEMA
2010... watch the trend
 
Yanaelekea kutimia... I see, nimenyoosha mikono!

Mkuu heshima mbele.

CHADEMA mpaka kufikia kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2010 itachekesha sana tena wasipokuwa makini wanaweza kusahaulika kama NCCR Mageuzi,sipendi itokee lakini kuna kila dalili Bwana Mbowe na timu nzima ya uongozi hawajui wanachotakiwa kikifanya.

Mchakato wa uchaguzi CHADEMA umeacha makovu yasiyoweza kutibika kirahisi,pia suala la chama kuchukua sura ya kindugu linaweza kutumiwa na CCM kukiweka mahali pabaya kadri siku zinavyosonga mbele.
 
Chadema ni chama cha siasa bado Hakijafikia kuwa chama mbadala cha CCM.

Kitika vipi ulishahama ccm?if yes kwanini mkuu? rudi nyumbani mkuu. tukutane kwenye PM
 
Chadema ni chama cha siasa bado Hakijafikia kuwa chama mbadala cha CCM.

Kitika vipi ulishahama ccm?if yes kwanini mkuu? rudi nyumbani mkuu. tukutane kwenye PM


Mbona mnasema hivo jama? Sisi huku madongo kuinama tupo mstari wa mbele kuhamasisha walala hoi kujiunga na mbadala! na kazi inaendlea kwa kasi nzuri tu, kwani kulikoni?

Opereshseni Sangara nayo tunaisubiri kwa hamu wakuu!
 
Chadema upo makini chini ya Mbowe na pia hata CCM wanajua hilo juu ya Mambo ya CHADEMa na pia itakuwa makini sana
 
JJ naona upo, vp hali ya CHadema kwa sasa shwari?????

JojiPoji

Mwaka 2009 zilisemwa shari nyingi kuhusu CHADEMA; huu ni mwaka 2010, CHADEMA ipo shwari. Tusonge mbele, mpaka kieleweke. Pamoja Tunaweza

JJ
 
Nilikuwa naipitia thread hii ya JF mwaka 2006, nimekubali watu walikuwa kweli wanazama deep, kwa sisi tuliojiunga majuzi juzi, tumemkuta championi ni Mzee Mwanakijiji na wachache ndio bado wapo. Mode fanya utaratibu kwa wanachama wanapoamua kupumzika, wawe na ustaarabu wa kuaga na kutoa sababu, kama zina mashiko, zifanyiwe kazi.

Huu ni mwaka wa uchaguzi, we need hivi vichwa JF more than ever.

Wajameni nyie vichwa wa JF iliokuwa likizo, rudini kazini, hiki ndio kipindi cha kutumia vichwa vyenu kuleta ukombozi wa kweli wa Mtanzania.

Ni ombi tuu.
 
Mzee JJ,

Kwanza heshima yako, halafu nafikiri unakumbuka nilikwambia nini kule BCs, Keenja na Sumaye watakuibia kura halafu bado ndugu yangu ninakukumbusha kuwa njoo una great skills politically, ila tu uko kwenye chama kibovu rudi nyumbani CCM tuanze kazi mpya bro!


15 I know thy works, that thou art neither cold nor hot: I would thou wert cold or hot.
16 So then because thou art lukewarm, and neither cold nor hot, I will spue thee out of my mouth
 
Mode fanya utaratibu kwa wanachama wanapoamua kupumzika, wawe na ustaarabu wa kuaga na kutoa sababu, kama zina mashiko, zifanyiwe kazi.
Mkuu Pasco, Senior members (hasa tulioanza nao 2006) huwa wakiwa na issue ambayo wanajua ni sensitive na wanajua ni muhimu kwa uhai wa jukwaa huwa wananitumia PM na hawalalamiki kwenye topic tu, nikitumiwa PM (Private Message) huwa naambatanishiwa na link ya eneo lenye tatizo na huwa linafanyiwa kazi kwa karibu kabisa...

Tukifahamishana kwa njia hii inapendeza sana kuliko mtu kulalamika kwenye posts ndani maana si rahisi kujua wapi watu wamelalamika au wamekosea, si rahisi kusoma kila sehemu, mods hawaoni kila post, nyingine zinapita... Ndo maana unaona leo nipo, x-mas nilikuwepo, hakuna leave kwangu lakino mods wengine ruksa kupumzika!

Nafurahi umeweza kusoma na kujua tulikotoka, endelea kusoma na kupata mengi zaidi!
 
16. Mzee Es, narudia tena. Matokeo ya uchaguzi hayawezi kunifanya niingie CCM. Kwa nini sikuingia in a first place. I differ in its leadership principles and policies!. Sijaingia kwenye siasa kwa ajili ya “Mkate na Jibini”. There is a vision and mission I am pursuing. Sorry for using strong language but as Shaban Robert puts it, ‘’ ‘’Msema kweli hukimbiwa na marafiki zake nikipatwa na ajali kama hiyo sitawaonea wivu wale wanaodumu na marafiki zao siku zote. Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo na kujinyima ushirika wa milele unaotarajiwa kutokea baada ya kushindwa kwa uongo”

Nafikiri hii paragraph ni jibu tosha kwa Mzee ES asifikiri watu wote wana tabia ya kutotosheka, kuna watu wanaridhika na kidogo walichonacho, vision zao haziyumbishwi.
Anaposema kwenye uchaguzi Mbowe alikuwa strong Candidate na Kikwete alionekana weak na matokeo Mbowe alipata kura chache, hawezi jiuliza kwanini ilitokea kuwa hivyo kama mwenyewe anakiri Mbowe alikuwa strong, kwanza sijasikia kama Chadema kuna siku walipinga matokeo wao Chadema wanasema hawakuridhishwa nayo.
Kuna sababu nyingi za Chadema kushindwa kwenye uchaguzi uliopita, kwanza Umri na uwezo(kipesa si isera) wa Chadema ukilinganishwa na ule wa CCM, pili kwa wakati huo Chadema ilikuwa haijajiimalisha zaidi hasa vijijini, tatu jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa ulikuwa si wa haki, polisi,serikali, Tume ya uchaguzi vyote vilikuwa biased, nne wizi ingawa hii ni vigumu kuithibitisha, mwisho hata utangazaji wenyewe wa matokeo haukuzingatia haki mfano matokeo kutangazwa bila kujumlisha vituo vyote 'ubabeubabe', na mambo kama hayo.
Nafurahi kuwa Mzee ES amekili Mbowe alikuwa strong candidate na hata wananchi wengi hawakuamini yale matokeo.
Kwanini Mbowe anapigwa vita zaidi sasa na si wengine: Mzee ES anashindwa kuelewa kuwa mti wenye matunda ndio hutupiwa mawe, kabla ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 nafikiri Mzee ES ulikuwepo na ulishuhudia, kama nakumbuka vizuri nilikuwa sisikii sana Jina la Mbowe na magazeti mengi yalikuwa hayaandiki sana habari za Chadema zaidi ya NCCR na Mrema, hata wewe Mzee ES sijui kama una makala yeyote inayomhusu Mbowe au Chadema kabla ya 1995, kwanini.
Wakati huo chama kilikuwepo ingawa kilikuwa hakisikiki baada ya Mbowe kugombea uraisi wa 2000 wengi ndio wakaanza kukijua chama vizuri na kikajinadi kwa sera ya majimbo ' nitoke vipi' kikawa na sera tofauti kabisa na vyama vingine kama si vyote hadi hii leo kinajulikana nchi nzima na nje ya nchi. Si kwamba hii ilikuja automatically ni kutokana na mipango thabiti ya chama kinachoongozwa na mwenyekiti wake Mbowe. Hata matumizi ya helkopta watu tuliona ni matumizi mabaya ya pesa za chanma lakini inalipa. Kwa hiyo huwezi kusema chama kinakuwa ila mwenyekiti wake ndio tatizo haiingii akilini, inawezekana ndiyo mikakati yake watu wajue ndivyo sivyo na wewe uliye nje utaona anakibomoa.

10 + 5 = 15 vilevile 20 - 5 = 15 majibu yote ni 15, mjinga hawezi jiuliza kuwa kuna wakati unaweza kujumlisha na kutoa ukapata majibu sawa, mwenye busara atajiuliza inategemea umetumia namba zipi, mpumbavu hatajua kabisa atasema haiwezekani.
 
Duh, leo nimepitia mada hii na kujisemea mwenyewe kumbe hekima haina darasa wala hainunuliwi sokoni kweli. Yaani haya mambo tuliyazungumza mwaka 2006, leo hii yanajitokeza kama sinema vile. Nimerudia kumsoma Kitila Mkumbo alonivuta Chadema na sasa aaah mwenyewe angeweza kula matapishi yake ingekuwaje sijui!
 
Dah.. Hakika JF kilikuwa kisima ya Elimu.. Yaliyosemwa mwaka 2006 tunayashuhudia 2014..
 
Mkandara wewe ni mmoja wa waanzilishi wachache niliowahi kukutana nao uso kwa uso.

Mie kinachonifanya niwe msomaji zaidi ya uchangiaji ni wingi wa waandishi wa kutumwa. Unaona wazi mtu hana hoja ila ana kazania hoja yake na kejeli juu. Taarabu sasa zinaimbwa humu bila kukoma.

Anyway hata mwalimu JKN aliongoza na kuachia wengine. Jukwaa lipo vyema bado akina Pasco wanaendeleza tulioanzisha.

Well done guys
 
Last edited by a moderator:

Mkuu heshima mbele.

CHADEMA mpaka kufikia kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2010 itachekesha sana tena wasipokuwa makini wanaweza kusahaulika kama NCCR Mageuzi,sipendi itokee lakini kuna kila dalili Bwana Mbowe na timu nzima ya uongozi hawajui wanachotakiwa kikifanya.

Mchakato wa uchaguzi CHADEMA umeacha makovu yasiyoweza kutibika kirahisi,pia suala la chama kuchukua sura ya kindugu linaweza kutumiwa na CCM kukiweka mahali pabaya kadri siku zinavyosonga mbele.

Sipati picha leo 2014 unapoisoma hii comment yako. A tragedy of miscalculation.
 
Kun post moja Mkandara amesema mwaka 2006 kua Mbowe hawezi kuachia madaraka hata iweje. Na ni mtu anayependa kusujudiwa (hawezi kujishusha) nimeisoma leo nikacheka sana.

Bob umetishaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom