16. Mzee Es, narudia tena. Matokeo ya uchaguzi hayawezi kunifanya niingie CCM. Kwa nini sikuingia in a first place. I differ in its leadership principles and policies!. Sijaingia kwenye siasa kwa ajili ya Mkate na Jibini. There is a vision and mission I am pursuing. Sorry for using strong language but as Shaban Robert puts it, Msema kweli hukimbiwa na marafiki zake nikipatwa na ajali kama hiyo sitawaonea wivu wale wanaodumu na marafiki zao siku zote. Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo na kujinyima ushirika wa milele unaotarajiwa kutokea baada ya kushindwa kwa uongo
Nafikiri hii paragraph ni jibu tosha kwa
Mzee ES asifikiri watu wote wana tabia ya kutotosheka, kuna watu wanaridhika na kidogo walichonacho, vision zao haziyumbishwi.
Anaposema kwenye uchaguzi Mbowe alikuwa strong Candidate na Kikwete alionekana weak na matokeo Mbowe alipata kura chache, hawezi jiuliza kwanini ilitokea kuwa hivyo kama mwenyewe anakiri Mbowe alikuwa strong, kwanza sijasikia kama Chadema kuna siku walipinga matokeo wao Chadema wanasema hawakuridhishwa nayo.
Kuna sababu nyingi za Chadema kushindwa kwenye uchaguzi uliopita, kwanza Umri na uwezo(kipesa si isera) wa Chadema ukilinganishwa na ule wa CCM, pili kwa wakati huo Chadema ilikuwa haijajiimalisha zaidi hasa vijijini, tatu jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa ulikuwa si wa haki, polisi,serikali, Tume ya uchaguzi vyote vilikuwa biased, nne wizi ingawa hii ni vigumu kuithibitisha, mwisho hata utangazaji wenyewe wa matokeo haukuzingatia haki mfano matokeo kutangazwa bila kujumlisha
vituo vyote 'ubabeubabe', na mambo kama hayo.
Nafurahi kuwa Mzee ES amekili Mbowe alikuwa strong candidate na hata wananchi wengi hawakuamini yale matokeo.
Kwanini Mbowe anapigwa vita zaidi sasa na si wengine: Mzee ES anashindwa kuelewa kuwa mti wenye matunda ndio hutupiwa mawe, kabla ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 nafikiri Mzee ES ulikuwepo na ulishuhudia, kama nakumbuka vizuri nilikuwa sisikii sana Jina la Mbowe na magazeti mengi yalikuwa hayaandiki sana habari za Chadema zaidi ya NCCR na Mrema, hata wewe Mzee ES sijui kama una makala yeyote inayomhusu Mbowe au Chadema kabla ya 1995,
kwanini.
Wakati huo chama kilikuwepo ingawa kilikuwa hakisikiki baada ya Mbowe kugombea uraisi wa 2000 wengi ndio wakaanza kukijua chama vizuri na kikajinadi kwa sera ya majimbo ' nitoke vipi' kikawa na sera tofauti kabisa na vyama vingine kama si vyote hadi hii leo kinajulikana nchi nzima na nje ya nchi. Si kwamba hii ilikuja automatically ni kutokana na mipango thabiti ya chama kinachoongozwa na mwenyekiti wake Mbowe. Hata matumizi ya helkopta watu tuliona ni matumizi mabaya ya pesa za chanma lakini inalipa. Kwa hiyo huwezi kusema chama kinakuwa ila mwenyekiti wake ndio tatizo haiingii akilini, inawezekana ndiyo mikakati yake watu wajue ndivyo sivyo na wewe uliye nje utaona anakibomoa.
10 + 5 = 15 vilevile
20 - 5 = 15 majibu yote ni 15, mjinga hawezi jiuliza kuwa kuna wakati unaweza kujumlisha na kutoa ukapata majibu sawa, mwenye busara atajiuliza inategemea umetumia namba zipi, mpumbavu hatajua kabisa atasema haiwezekani.