Olengurumwa : Kukosekana kwa familia imara inaweza kuwa sababu ya kuchochea uharifu na kuporomoka kwa maadili

Olengurumwa : Kukosekana kwa familia imara inaweza kuwa sababu ya kuchochea uharifu na kuporomoka kwa maadili

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
"Faida za kuwa na familia imara yenye amani, mshikamano na upendo kwa watoto ni kubwa sana, kwanza watoto watakuwa salama, sio rahisi watoto kufanyiwa ukatili, watoto watakuwa na maadili mazuri lakini utaona hata idadi ya watoto wa mitaani inapungua"
IMG-20240515-WA0004.jpg

Mratibu THRDC, Wakili, Onesmo Olengurumwa

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya familia ambayo uadhimishwa siku kama ya leo Mei 5, kila mwaka, ambapo ametoa wito kwa Serikali kupitia Sheria, na miongozo yake kuendelea kuiboresha zaidi na kuisimamia ili kulinda familia.

Amesema jamii yenye kuzingatia umuhimu wa familia inaweza kuwa katika hali nzuri ya kuepuka changamoto mbalimbali ikiwemo matukio ya uharifu, kuporomoka kwa maadili, matukio ya ukatili kwa watoto, matumizi ya madawa ya kulevya...

Olengurumwa anasema kuwa kwa siku za hivi karibuni familia zimekuwa hatarini, amedai kati ya kinaishiria ni taarifa za uwepo la wimbi kubwa la 'single mother", hali ambayo amedai kuwa imekuwa ikipelekea watoto kukosa malezi stahiki huku wengine wakiishia kuwa 'watoto wa mitaani'.

Pia amedai kuwa watoto ambao utokana na familia bora ni chachu ya familia bora kwa siku za mbeleni, lakini amedai kwa watoto wengi ambao hawatokani na familia bora wengi wao ni vigumu kuwa na familia bora huko mbeleni.

Ametoa wito kwa Serikali kuipa umuhimu zaidi siku ya familia kwa lengo la kuchochea watu wengi kutambua umuhimu wa familia.

Alipoulizwa juu ya kauli ya 50/50 baina ya Mwanaume na Mwanamke kudaiwa kupelekea changamoto ambazo zinaweza kuchangia kuvunjika au vijana wengi kuacha kuingia kwenye familia, amesema kumekuwepo na madai hayo licha ya kutokupo kwa tafiti rasmi.

Lakini amesema mapokeo au namna uwasilishaji wa ajenda hiyo unavyoratibiwa unaweza kuwa sababu ya kupelekea kuwepo na mtazamo huo. Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia kuendelea kuzingatiwa ili kuwa na jamii yenye haki kwa wote.
 
Ndo ukweli ila kwa kizazi hiki watakaoshinda mtihani ni wachache sana
 
Back
Top Bottom