Olengurumwa: Uhaini waliopewa akina Dkt. Slaa unatia doa taifa na taswira ya Rais

Wewe kwa ufahamu wako ili mtu ashitakiwe kwa kesi ya Uhaini afanye mambo gani ili uwe uhaini?
 
Wewe kwa ufahamu wako ili mtu ashitakiwe kwa kesi ya Uhaini afanye mambo gani ili uwe uhaini?

Mbona mifano ipo mingi sana humu JF ya watu waliofanya uhaini kweli,Katiba imesema wazi uhaini ni nini.

Soma kuhusu Nyerere kutaka kupinduliwa ,utajua maana halisi ya uhaini halafu linganisha na "Uhaini" wa Dr Slaa,Mdude na mwabukusi.
 
Mambo ya mkataba wa bandari yako Mahakama ya Rufaa. Hao wameshikwa kwa kauli zao za kuchochea maandamano ya kupindua nchi.
 
Soma kesi ya Uhaini ya mwaka 1985. Kuna waliokuwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na wasiokuwemo kwenye hivyo vyombo na hata serikalini ambao walikutwa na hatia.
Sasa unajipatia jibu wewe mwenyewe!
Kulikuwa mpaka makomandoo kina marehemu Mohamed Tamim na Yassin memba kaka yake na Mussa memba....

Sasa haya ya wakili mmojana Dk slaa mwanasiasa mstaafu mmoja na whistle-blower mmoja ndio uhaini?
 
Na hichi ndio kiini cha tatizo watu wameshakula hela za muarabu matumbo joto wapo tayari hata kuua ili mkataba upite
 
Waliowakama Dk Slaa, Mwabhukusi na Mdude ndio walioanza kuwatumia meseji za kutaka kuwaua kwa hiyo wakamataji ni majambazi dhidi ya binadamu (crime against person).
Watu watatu wanampindua nani kwa nyenzo gani?

Wamemchochea nani na akafanya kitendo gani dhidi ya yule anayedaiwa kutendewa kosa?

Mwanajeshi gani, usalama wa taifa gani au kiongozi mwandamizi wa serikali ambaye amekula njma na hao watu watatu kumpindua rais na nia hiyo ingetekelezwa na wapi?
 

Kwann hamkulalamika wakat hao waliokamatwa walipokua wanatumia huo uhuru vibaya
Afu kukosoa bandari hakujawafanya wakamatwe acheni upotoshaji wote tumeyasikia maneno yao jukwaani .msilete siasa za chuki kwa kila jambo,hao wamepata waliostahil kwa matamshi yao ya kijinga ya kutishia usalama na kueka chuki wala c kauli za bandari
 

Ukweli mtupu mkuu.na wamefanya kusudi ili kumtoa rais kwenye reli aonekane ananyima uhuru
Ila hakuna uhuru usio na mipaka
 

Utafanyaje vinginevo? Aya kawatoe au na ww endeleza walichoanza
 
Eti mhaini anajitangaza
 

Wanaelewa ila wanaeka emotion mbele hapo ndio wanajikuta kutumika vibaya na wanasiasa
 

Uelewa wako ukoje mkuu..kauli za mtu mmoja mwenye ushawishi zinaeza pindua serikali
Kama wakiachwa waendelee na izo kauli wazani nn kitatokea?
 
huyo masai mchumia tumbo akae kimya, hao ni vibaraka wa maadui zetu ndivyo wanavyopata kula yao, hawana uzalendo zaidi ya matumbo yao.wapuuzwe hao washenzi
 
Kwa hili hata Mimi sioni sababu ya kupoteza Fedha kwa kesi Hii. Tutadharaulika saaana kimataifa. Polisi Hasa IGP atumie hekima kwa Hili. Hata wananchi hawatawaamini, ni vizuri kuaminika
we ndio unadharaulika kwa huo ujinga wako
 

Kwa kauli hii yaonesha hata mahakamn ujawai simama.usipojua sheria utaona mahakama inakuonea maana wew utaleta ushahidi wa hisia wenzako wanakuja na hoja na vifungu vya sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…