Olengurumwa: Uhaini waliopewa akina Dkt. Slaa unatia doa taifa na taswira ya Rais

Olengurumwa: Uhaini waliopewa akina Dkt. Slaa unatia doa taifa na taswira ya Rais

nchi haiwezi kutulia kwa mtindo huo. Hakuna anayetaka kuipindua serikali. ambacho hakitakiwi ni mkataba mbovu wa bandari. kufunga watu sio suluhisho. inatujengea chuki zaidi baina yetu, tunajichafua kimataifa. wanaomshauri Rais wanampoteza. majitu machumia tumbo ndio yanayoiharibu hii nchi.

Mkataba na DPW uvunjwe, watu waachiwe huru, maisha yaendelee! VINGINEVYO.
Kauli za uchochezi, za chuki, za kibaguzi na kwamba tutaiondoa serikali hii kabla ya 2025 ina uhusiano gani na mkataba wa bandari? Rwanda mambo yalianza hivi hivi mpaka kanisani chuki zilienezwa wakaishia kwenye mauaji ya halaiki. Navipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri. Funga wajinga hao, pumbavu kabisa.
 
Jamaa ni wapuuzi sana ,uhaini mpaka kuwe na NIA OVU ambayo ipo confirmed kabisa kwamba walitaka kupindua serikali either kwa kupanga mikakati ya kumuua rais au kuorganise vita na huwa ni siri kwa wanaofanya ,sasa cha kushangaza eti wanamkamata mtu kwa uhaini kisa ametamka waziwazi kwenye TV(Yaani hakuna Siri kabisa).

Wangejua Mapinduzi waliyofanya kina Mu7 na Kabila wasingepoteza muda kutumia resorces/kodi za walalahoi kuendesha cases za kijinga.

Wangetamka kwa siri tungejua serikali imewaonea kumbe hata wew umeskia kauli zao.mtu akikutishia kwa maneno tuh anataka kukuua kuna sheria na kanuni za kumshtaki kwa kutishia maisha yako.sio hadi aje na kisu kukukimbiza uponee chupuchupu ndio ukashtaki
 
Hatuna IGP mweledi. Kingai siyo mweledi
Pale anapaswa kutenguliwa apishe wenye uwezo wa kazi.

JEshi la.polisi linahitaji maboresho makubwa kimfumo na kiutendaji.
we unaona unafit nafasi yake, nyie kima utafikiri mnajua kila kitu
 
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema.

Pamoja na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kupongezwa na wadau mbali mbali wa haki za binadamu katika maeneo mengi ikiwemo kutoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni uhuru, sakata la kukamatwa wakosoaji wakubwa wa mkataba wa bandari Balozi Mstaafu Dkt. Willbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali kunaweza kutia dosari mazuri hayo pamoja na kuchafua taswira ya Rais Samia kimataifa endapo akikubali watuhumiwa hao kuwa na kesi ya uhaini.

Amesema, itakuwa ni historia katika awamu hii ya sita na pia itakuwa ni kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kupata watu wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

"Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake, katiba imetulinda, Wakili Mwabukusi, Mdude na Balozi Dkt. Slaa walikuwa wanafanya kwa mujibu wa katiba na kama kuna mahali popote waliteleza kwa maneno ya hapa na pale isiwe ni sababu ya kuwafungulia kesi kubwa kama hii na kuwazuia wao na Watanzania wengine wasikosoe" alisema Wakili Olengurumwa na kuongeza

"Kuanza kuwakamata wote wanaopinga mkataba wa bandari kuanzia kwa Wakili Madeleka sasa Slaa na wenzake litatutia doa kama Taifa, tunawashauri viongozi wetu kabla ya kufika mbali katika hatua hii ,hawa watu wasifunguliwe jalada la uhaini.”
Mbona mlikaa kimyaa wakati wao wanatoa maneno ya uhaini?
 
kauli za uchochezi, za chuki, za kibaguzi na kwamba tutaiondoa serikali hii kabla ya 2025 ina uhusiano gani na mkataba wa bandari? Rwanda mambo yalianza hivi hivi mpaka kanisani chuki zilienezwa wakaishia kwenye mauaji ya halaiki. Navipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri. Funga wajinga hao, pumbavu kabisa.

Wanaowatetea utaskia ooh wako watatu kwa hio waachwe mpka wawe wengi ndio washughulikiwe au
Yaani watz cjui tukoje
 
Kwa kauli hii yaonesha hata mahakamn ujawai simama.usipojua sheria utaona mahakama inakuonea maana wew utaleta ushahidi wa hisia wenzako wanakuja na hoja na vifungu vya sheria
Msubirini kibatala aje kuwagalagaza mahakamani.
 
Wapi Dr Slaa ametishia? Umeisikiliza ile clip vizuri? kauli aliyoitoa siyo uhaini ,alikuwa anajibu swali la mtangazaji inaamisha kwamba asingeulizwa asingejibu.

Madaraka yanatoka kwa watu na ndiyo wenye mamlaka ya kupindua serikali(iwe field au sanduku la kura) ,hakusema mimi nitaorganise na wananchi tuipindue serikali na hata kama akisema bado si uhaini mpaka kuwe na nia OVU(Mikakati ya kutekeleza ambayo imegundulika).....Wanasiasa siku zote huwa wanasema maamuzi mnayo nyinyi wananchi wa kuiondoa Serikali madarakani.
Ndio maana ya kupelekwa mahakamani ili ukweli ujidhihiri.
 
Enzi za utawala wa Mwinyi Mtikila aliwahi kumwambia Rais Mwinyi arudi mwenyewe Zanzibar kabla hajarudishwa kwenye jeneza, hakufunguliwa kesi yeyote kutokana na matamshi hayo, ingekuwa leo enzi za Samia angenyongwa kabisa. Sheria na Busara ni mapacha.
Hiyo kauli Ina tatizo gani?
 
Unajuaje kama Polisi hawana? Kwa Tanzania, Sheria zetu zinasema,"Innocent until proven guilty"! Wacha waende mahakamani kitajulikana huko kuliko kuleta ushabiki humu JF!

ok tu-assume wanavyo ndiyo maana wamepelekwa na upelelezi ushakamilika.
 
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema.

Pamoja na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kupongezwa na wadau mbali mbali wa haki za binadamu katika maeneo mengi ikiwemo kutoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni uhuru, sakata la kukamatwa wakosoaji wakubwa wa mkataba wa bandari Balozi Mstaafu Dkt. Willbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali kunaweza kutia dosari mazuri hayo pamoja na kuchafua taswira ya Rais Samia kimataifa endapo akikubali watuhumiwa hao kuwa na kesi ya uhaini.

Amesema, itakuwa ni historia katika awamu hii ya sita na pia itakuwa ni kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kupata watu wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

"Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake, katiba imetulinda, Wakili Mwabukusi, Mdude na Balozi Dkt. Slaa walikuwa wanafanya kwa mujibu wa katiba na kama kuna mahali popote waliteleza kwa maneno ya hapa na pale isiwe ni sababu ya kuwafungulia kesi kubwa kama hii na kuwazuia wao na Watanzania wengine wasikosoe" alisema Wakili Olengurumwa na kuongeza

"Kuanza kuwakamata wote wanaopinga mkataba wa bandari kuanzia kwa Wakili Madeleka sasa Slaa na wenzake litatutia doa kama Taifa, tunawashauri viongozi wetu kabla ya kufika mbali katika hatua hii ,hawa watu wasifunguliwe jalada la uhaini.”
Ndo huyo anataka kusuluhisha kinya!!
 
Back
Top Bottom