Oliver N’goma: Mmoja kati ya wanamuziki bora zaidi wa kiume wa miondoko ya Zuku

Mzee Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
9,968
Reaction score
16,680
Huyu ni mmoja ya kati ya wanamuziki bora zaidi wa kiume wa miondoko ya Zuku kuwahi kutokea katika hii dunia.
Embu tujikumbushe kidogo na hii ngoma yake Inaitwa Ng’e. Btw wale watoto wa bongo flavor sikilizeni hii ngoma alafu mlinganishe na muziki wa sasa wa wavaa suruali chini ya makalio.


 
Huyu jamaa ni habari nyingine uwa nikisikilza nyimbo zake zinanipeleka mbali sana pia kuna na nyimbo za miria bele
 
Jamaa anaimba mpaka unajisikia burudani, japo simwelewi ila ni mpenzi sana wa nyimbo zake
 
Producer wake mkuu alikua Manu Lima ambaye ni mpiga kinanda hodari sana. Katika baadhi ya nyimbo zake akiwashirikisha wakali wa magitaa akina.Dally Ndala Kimoko-Solo na Denis Khasia a.k.a Lokassa Ya Mbongo-Rhythm. Nyimbo kama Lusa na.Mayumba mipini hio ya gitaa imesikika vema na katika wimbo Alfoncine kinanda cha Manu Lima kimetamalaki sawia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwanini wasanii wetu hawajifunzi kwa waliofanikiwa kama hawa, unajua kuimba ila kutunga huwezi tafuta watunzi mahili wakuandikie mashairi, wapiga vyombo wapangilie mziki wako ili mwisho wa siku utoke na kitu murua kabisa na sio hii miziki yeboyebo inayovuma siku 2 tu, siku ya 3 inachuja.
 
Naisikia sauti ya Massoud Massoud hapa kwny comment...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…