Oliver N’Goma: Muziki Burudani na Elimu (Ujumbe)

Oliver N’Goma: Muziki Burudani na Elimu (Ujumbe)

Tonydigital

Senior Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
186
Reaction score
245
Habari za muda huu wadau?

Siku ya leo ya mapumziko (Muungano) nimeamua kupitia na kusikiliza baadhi ya nyimbo za nguli wa muziki Oliver N’Goma ( sasa marehemu) moja ya nyimbo zake nazozipenda ni hii “Bane” iliyoachiwa rasmi mwaka 1990 na inapatikana kwenye album yake ya kwanza yenye jina hilo hilo.
Nimevutiwa zaidi na contents za wimbo huu.
Nyimbo: Bane
Maana: Watoto (children)
Album: Bane
Kutolewa: 1990
Mwandishi: Oliver N’Goma
Mwandaaji: Manu Lima

-Katika kibao hiki Oliver anakiasa kizazi kipya (watoto) kuhusu umuhimu wa elimu katika maisha yao. Anasisitiza kuwa maisha yamebadilika sana hivyo wawe makini, imara na kusikiliza ujumbe wake. Wajiandae wawe watu wenye msaada kwa jamii baadae kwa kujikomboa kupitia elimu, mali za wazazi sio zao na zinaweza kuwaingiza kwenye matatizo endapo ndugu wenye nia mbaya waingiliapo.

Hivyo wajishugulishe kutafuta vitu na mali zao binafsi na sio kutegemea urithi / wazazi. Oliver N’Goma anaitaja shule “Icole” katika dakika ya (3:57) kama moja ya nyenzo ya kubadilisha maisha na kuwa watu bora katika jamii, hivyo watoto (kizazi kipya) wafanye bidii katika elimu kwani ndo ukombozi halisi.MWISHO.

Mzee wetu Lowassa pia aliwahi kusisitiza “Elimu Elimu Elimu”😀


8F5FCD89-81D4-4A80-A178-4D9798081CFF.jpeg
 
Mimi nikiskia mtu anamfananisha ngoma na takataka hasa yule Monique seka naua huyo
kwako Massoud Massoud
manu lima anaonekana alikuwa fundi sana
 
Mimi nikiskia mtu anamfananisha ngoma na takataka hasa yule Monique seka naua huyo
kwako massoud massoud
manu lima anaonekana alikuwa fundi sana
😂😂😂 Manu alimjulia sana Oliver ndo maana hata ukisikia Ile album ya 3 (Seva) utaona utofauti mkubwa (ndo album pekee ambayo Lima hakuandaa)

Comparison ya Oliver vs Monique Seka binafsi naona ni humuliation kwa Monie..alinganishwe na kina “Tshala Muana” & etc.
 
Back
Top Bottom