Olympic 2024 France: Maonesho ya Ufunguzi yashutumiwa kuonesha viashiria vya ushetani na upinga Kristo

Olympic 2024 France: Maonesho ya Ufunguzi yashutumiwa kuonesha viashiria vya ushetani na upinga Kristo

Mungu mwenyewe atawahukumu kwasababu yeye ndiye anayejua wapi ni watakatifu nawapi wabaya.Mambo ya Mungu uku afrika tunajipa tu umuhimu tusio kua nao.
Mungu habagui bara au taifa, Wote tupo sawa mbele ya Mungu sio wazungu au waafrika pekeyao
 
Inasikitisha sana watu wengi duniani wameshutumu sana sherehe za kufungua michezo ya Olympic za mwaka huu jijini Paris

Ni kama Shetani alishushwa kwenda kutumbuiza

Ungekuwa unajua historia usingetokwa na povu jingi kiasi hiki, Michezo ya Olympics imekuwepo miaka takribani 700 kabla ya Kristo huko katika Ugiriki ya kale na ilikuwa kwa ajili kumuenzi Mungu wa Wagiriki aitwaye Zeus na mtoto wake Heracles, nyie watu wa dini ndio mnajipendekeza na kulazimisha mambo yenu katika Historia na utamaduni wa Ugiriki ya kale.
 
Uwa siamini kuwa wazungu wametuzidi akili waafrika.unaanza kutetea ushoga alafu ukajiita una akili?
Wasingekuwa na akili wasingekutawala kwa zaid ya karne nzima huku wakiwachukua babu zako utumwani kwa karne nyingi tu.
 
Ungekuwa unajua historia usingetokwa na povu jingi kiasi hiki, Michezo ya Olympics imekuwepo miaka takribani 700 kabla ya Kristo huko katika Ugiriki ya kale na ilikuwa kwa ajili kumuenzi Mungu wa Wagiriki aitwaye Zeus na mtoto wake Heracles, nyie watu wa dini ndio mnajipendekeza na kulazimisha mambo yenu katika Historia na utamaduni wa Ugiriki ya kale.
Uko sahihi kabisa Mkuu
 
Wajukuu wa waliokuletea dini unayoing'ang'ania ndiyo wana-mock hayo maujinga ya babu zao.
Wewe muafrika fuata tamaduni za kwenu.
Acha kujifanya mzungu kuliko wazungu wenyewe.
Unajifanya mkristu kuliko waliokuletea ukristo.
Ndiyo kila siku tunawaambia achaneni na ukoloni mamboleo wa dini.
 
Ulaya walishaachana na Ukristo miaka mingi iliyopita na sasa wanauza Majengo ya Makanisa kwa Waislamu!
Ufaransa siyo siku nyingi litakuwa Taifa la kiislamu!
Sio waliachana na dini, ila mamlaka ya shetani ndyo imefanya juhudi kusambaratisha dini huko ulaya, na bado juhudi zinaendelea kutimiza lengo hilo duniani kote
 
Wajukuu wa waliokuletea dini unayoing'ang'ania ndiyo wana-mock hayo maujinga ya babu zao.
Wewe muafrika fuata tamaduni za kwenu.
Acha kujifanya mzungu kuliko wazungu wenyewe.
Unajifanya mkristu kuliko waliokuletea ukristo.
Ndiyo kila siku tunawaambia achaneni na ukoloni mamboleo wa dini.
Najifanya mkristo? Wapi nimesema mimi ni mkristo?

Pia ni afadhali kuamini katika dini kuliko kutambika makaburini
 
Najifanya mkristo? Wapi nimesema mimi ni mkristo?

Pia ni afadhali kuamini katika dini kuliko kutambika makaburini
Kutambika makaburini ni mojawapo ya dini za asili, hata dini kubwa mbili huwa wanafanya ibada za makaburini.
 
Badala ya kupambana kutokomeza umaskini, uhujumu uchumi, wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma uliokithiri barani kote Afrika,

Mnahangaika na maisha ya wazungu ambayo hayawasaidii na haisaidii kubadilisha chochote kile nchini kwenu.
Huu uzi hausiani na umasikini wa bara la Afrika. Tunachangia kulingana na mada husika iliyo kwenye thread.
 
Ni zipi ibada za kuomba wafu makaburini zinafanywa na watu wa dini?

Watu wa dini tena wakristo wakatoliki, Hufanya ibada kwenye maiti za wafu na hata makaburini.

Wakristo wakatoliki Hufanya ibada za wafu wakiabudu maiti za kina Padri Pio, Rita wa kashia na wafu wengine wakidai kwamba ni watakatifu!!!

Kila ikifika November 2, wakristo wakatoliki Hufanya ibada za wafu tena wengine makaburini kabisa wakiwasha mishumaa.

Kwa hivyo hata dini unayo jaribu kuitetea kwamba hawaabudu wafu, Ni uongo.

You haven't done enough research.
 
Ungekuwa unajua historia usingetokwa na povu jingi kiasi hiki, Michezo ya Olympics imekuwepo miaka takribani 700 kabla ya Kristo huko katika Ugiriki ya kale na ilikuwa kwa ajili kumuenzi Mungu wa Wagiriki aitwaye Zeus na mtoto wake Heracles, nyie watu wa dini ndio mnajipendekeza na kulazimisha mambo yenu katika Historia na utamaduni wa Ugiriki ya kale.
Inajulikana hilo hii mchezo ilianzia jiji la Athene, Ugiriki na hapo ndipo ilikuwa stadium ya kwanza ya Olympic games.

Hakuna mtu yeyote anayejipendekeza kinachozungumziwa na watu ni maadili.

Kumbuka huu ufunguzi umetazamwa na watu zaidi ya 1.2 billion worldwide kutia ndani watoto.

Je, huoni kuwa mahudhui yake yanabomoa maadili? Je, waandaaji walikuwa sahihi kufanya yale maonyesho waziwazi kwenye jamii?
 
Huu uzi hausiani na umasikini wa bara la Afrika. Tunachangia kulingana na mada husika iliyo kwenye thread.
Haya thibitisha huyo shetani yupo?

Kisha thibitisha hiyo michezo ya olimpiki ni ya kishetani.

Sio unaleta mihemko yenu ya kidini na kuipachika kwenye tamaduni, michezo na burudani za watu.
 
Back
Top Bottom