MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Binafsi kama mdau mkubwa wa sana ya muziki, hasahasa ule wa Afrika. Hizi siku mbili nimesikiliza album mpya ya msanii kutoka Nigeria, Omah Lay. Niseme tu, mimi kama shabiki mkubwa wa huyu msanii kinda sijaangushwa kabisa. Album yake inaitwa BOY ALONE na imetoka leo hii.
Nilichofurahishwa sana na Omah Lay ni kiwango chake cha ubunifu kilichotumika kwenye nyimbo za humu ndani. Ukisikiliza vizuri utatambua kwamba ameimba Modern RnB, Soul na Pop lakini ile radha ya muziki wa Afrika Magharibi (High-Life) haijabadilika. Vyombo vya asili kama ngoma vinasikika vizuri, lakini hata upigaji wake umekaa kiasili. Kuna sehemu nyingine utasikia mahadhi ya muziki wa Jazz, sehemu nyingine utakutana na uimbaji kama ule wa ISICATHAMIYA kama ambao huimbwa na BLACK MAMBAZO. Sema huku ndani wametumia ISICATHAMIYA kama Back Vocals.
Kiukweli nimefurahishwa sana, hasa ukizingatia kwamba umri wake ni mdogo, lakini pia kwenye nyimbo nyingi amesimama mwenyewe bila kushirikisha wasanii wakubwa kama ambavyo wengine wemefanya. Kiufupi ameimba Afro-Fusion muziki ambao Burna Boy anaimba. Amethibitisha ukomavu mkubwa sana maana genre ya Afro-Fusion siyo rahisi kuimba. Wasanii wachache wa Nigeria kama ASA, Burna Boy na Timi Dakolo ndiyo wameweza kuimba vizuri genre inayochanganya miziki ya Afrika na Marekekani.
Pia watengenezaji wa hii Album (Voice Engineers) wamefanya kazi kubwa hasa kwenye MIXING, kila nyimbo inasikika vizuri. Naamini kama watamnadi vizuri, kuna nyimbo zake zinaweza zikafanya vizuri sana sokoni mwaka huu.
Sijapeleka mbele wimbo hata mmoja, lakini kuna nyimbo ambazo zimefanya vizuri tofauti na Understanding na Attention ambazo zilitoka mapema.
1. I'm Mess
2. Soso
3. How to luv
4. Never Forget