Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Serikari imeweza kununua madege, itshindwa kununua mtumbwi wa kubeba mbuzi alfu, au anaomba Oman wasaidie?
 
Mama aliposema tu usafirishaji wa wanyama hai WAARABU WAKAPIGA MAKOFI! Ukiona hivyo ujue tumeliwa. Tumetangaza mbuga zet kuwa shamba la bibi! Sina uhakika kama ndivyo alivyokuwa amepanga kusema au hilo la kusafirisha wanyama hai (live animals) amelifikiri hapo hapo. Ninasema hivyo kwa sababu hotuba yake lazima iwe imeandikwa na wataalamu na kupitiwa na wataalamu kabla ya kuidhinishwa. Ina maana wataalamu wetu ndio wamemwandikia mama hivyo?
 
Ni lini mtauza finished products? Wakiuzwa ng'ombe walio hai viwanda vya nyama vitawauzia nani?
Hapa ndipo utakapo gundua kama nchi, hatuna viongozi makini na wenye maono!
Yaani viongozi wa ccm wanaona fahari kuuza nchi kwa vipande 30 vya fedha!

Hawajawahi kuwa na uchungu na maliasili zetu. Badala ya kuwauzia hao Waarab nyama iliyochakatwa kwenye viwanda vyetu vya ndani! Eti unawauzia wanyama walio hai!
 
Hapo kwenye kitimoto umechapia mkuu...
 
Sasa kwetu kinacholengwa hapa ni wanyama pori kama twiga, pundamilia, vifaru na kadhalika. Lete mfano wa nchi moja tu duniani ambayo husafirisha mali asili kama wanyama kwa wingi kiasi cha kutengenezewa meli yao. Hata hivyo hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa huo mfano wa kondoo huko australia walikuwa wanasafirishwa nje ya australia, maana usafiri wa meli huko kati ya mji na mji ni kawaida maana ni kisiwa hicho, Ni kama kusafirisha mifugo toka mwanza kwenda bukoba kwa meli.
 
Haya ndio mawazo ya mtanzania wa kawaida, kudhani kila siku anaibiwa yeye tu!. Unaweza kuweka ushahidi wa wizi utakavyokuwa?.
 
Hizi ni hisia zako tu mkuu.
 
Maliasili zetu ni kama mapambo tu kama hatuzitumii na zikatuzalishia pesa. Ni akili ya kimaskini kujisifu kuwa tumejaliwa mali nyingi halafu hakuna mkakati wa kuzigeuza kuwa pesa.

Ni uoga pia kuendelea kuahirisha matumizi ya rasilimali hizi huku miaka ikiwa inakwenda kwa kasi.
 
Somalia sio nchi ya kufananisha na chochote. Somalia ni failed state, Hakuna serikali

Una uhakika Hakuna serikali Mbona juzi wamefanya uchaguzi

Sisi tuna kila kitu kuwazidi ila bado tunaomba
Tusibishane kwa failed state or not hapa tunaongelea biashara Mkuu
Kuna watu wanapeleka bidhaa sana huko na hata Oman wanafanya sana biashara huko
 
Kusafirisha wanyama hai hata wa porini si kitu kigeni. Kilicho kigeni sasa ni kule kutengenezwa meli kabisa ili kuvuna kabisa na kufilisi kabla ya 2030 na tuachiwe mbuga tupu! Si ajabu wakahamishiwa zenj wengine, na watalii wakawa wanaishia zenj.
 
Watanzania tuna shida vichwani. Si bure, tupimwe.
 
Matumizi ya mali asili siyo kuihamishia kwa waarabu halafu kizazi kijacho kikose chochote!! Matumizi sahihi ya maliasili kwenye mbuga zetu ni utalii endelevu!! Wawekezaji wajenge mahoteli mazuri ya kitalii na watumishi waajiriwe watanzania, kuboresha miundombinu na kuboresha mazingira ya wanyamapori!
 
I don't think timing ya safari na pia hayo anayoongelea is best ...
 
Hii ni fursa nzuri sana kwa mauzo ya Mbuzi, Kondoo na Ng'ombe ila ni vizuri serikali "isiwatafute" watakaorusha mtandaoni picha za Twiga na Pundamilia wakiwa kwenye meli tayari kuelekea Oman! maana hakuna siri siku hizi!! teknolojia iko juu!!

Iwapo watasafirisha wild animals kwenda Oman tutakuwa na Rais mbaya mno kuwahi kutokea na sidhani kama katiba itabaki salama akimaliza muda wake tutaichanachana na kufuta uongozi wa kinamama milele!!

Hivi ulaya hawapokei wakimbizi wasiopenda kuongozwa na mwanamke nchini mwao? wengine hatumuelewi Bimkubwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…