Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Salaam Wakuu,

Rais Samia katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, amesema kuna umuhimu Mkubwa wa kuangalia Usafiri wa Majini akimanisha Meli yenye Uwezo wa kusafirisha Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman.

Watu hapa wasifikilie Wanyama Pori tu, Bali ni Habari njema kwa Wafugaji wa Tanzania kwani sasa Wataanza Kusafirisha Ng'ombe, Sungura, Kitimoto, Mbuzi, Swala, Twiga nk hasa kwa wawindaji wenye Vitaru.

Pia kazungumzia kuhusu meli za Kuvua samaki Bahari Kuu.

Amewataka Oman waje kuwekeza Tanzania ardhi ipo ya kutosha.

Watanzania Kaeni Mkao wa kula.

............................................................................

Rais Samia akiwa kwenye kongamano Kiuchumi nchini Oman, amesema kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman kutaboresha biashara kati ya pande hizo mbili

Pia amegusia japokuwa tuna makubwa ya kuvua, kwa sasa hamna uvuvi wenye tija kwa taifa, amesema “kuna nchi zinakuja Tanzania kuvua na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa, hivyo wanavua na kuondoka, hili ni eneo lingine ambalo tunaweza kushirikiana kwa pamoja”

Amesema kuwa kongamano la mwaka huu limekusudia kuangazia namna Tanzania itashirikiana na Oman katika sekta za utalii, kilimo, Uzalishaji (viwanda) mifugo na uvuvi na usafirishaji wa majini.
Serikari imeweza kununua madege, itshindwa kununua mtumbwi wa kubeba mbuzi alfu, au anaomba Oman wasaidie?
 
Mama aliposema tu usafirishaji wa wanyama hai WAARABU WAKAPIGA MAKOFI! Ukiona hivyo ujue tumeliwa. Tumetangaza mbuga zet kuwa shamba la bibi! Sina uhakika kama ndivyo alivyokuwa amepanga kusema au hilo la kusafirisha wanyama hai (live animals) amelifikiri hapo hapo. Ninasema hivyo kwa sababu hotuba yake lazima iwe imeandikwa na wataalamu na kupitiwa na wataalamu kabla ya kuidhinishwa. Ina maana wataalamu wetu ndio wamemwandikia mama hivyo?
 
Ni lini mtauza finished products? Wakiuzwa ng'ombe walio hai viwanda vya nyama vitawauzia nani?
Hapa ndipo utakapo gundua kama nchi, hatuna viongozi makini na wenye maono!
Yaani viongozi wa ccm wanaona fahari kuuza nchi kwa vipande 30 vya fedha!

Hawajawahi kuwa na uchungu na maliasili zetu. Badala ya kuwauzia hao Waarab nyama iliyochakatwa kwenye viwanda vyetu vya ndani! Eti unawauzia wanyama walio hai!
 
Salaam Wakuu,

Rais Samia katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, amesema kuna umuhimu Mkubwa wa kuangalia Usafiri wa Majini akimanisha Meli yenye Uwezo wa kusafirisha Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman.

Watu hapa wasifikilie Wanyama Pori tu, Bali ni Habari njema kwa Wafugaji wa Tanzania kwani sasa Wataanza Kusafirisha Ng'ombe, Sungura, Kitimoto, Mbuzi, Swala, Twiga nk hasa kwa wawindaji wenye Vitaru.

Pia kazungumzia kuhusu meli za Kuvua samaki Bahari Kuu.

Amewataka Oman waje kuwekeza Tanzania ardhi ipo ya kutosha.

Watanzania Kaeni Mkao wa kula.

............................................................................

Rais Samia akiwa kwenye kongamano Kiuchumi nchini Oman, amesema kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman kutaboresha biashara kati ya pande hizo mbili

Pia amegusia japokuwa tuna makubwa ya kuvua, kwa sasa hamna uvuvi wenye tija kwa taifa, amesema “kuna nchi zinakuja Tanzania kuvua na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa, hivyo wanavua na kuondoka, hili ni eneo lingine ambalo tunaweza kushirikiana kwa pamoja”

Amesema kuwa kongamano la mwaka huu limekusudia kuangazia namna Tanzania itashirikiana na Oman katika sekta za utalii, kilimo, Uzalishaji (viwanda) mifugo na uvuvi na usafirishaji wa majini.
Hapo kwenye kitimoto umechapia mkuu...
 
Mchakato mzima wa biashara ya wanyama hai unahusisha idara nyingi mfano wafugaji wenyewe, mabwana mifugo, afya ya mifugo, kunenepesha mifugo, usafiri rafiki mpaka bandarini na kisha kupakiwa ktk meli . Ni zoezi linalotakiwa wadau wengi kujiweka ktk utayari kufanikisha azma hiyo ya biashara ya wanyama hai kufanyika.

Sasa kwetu kinacholengwa hapa ni wanyama pori kama twiga, pundamilia, vifaru na kadhalika. Lete mfano wa nchi moja tu duniani ambayo husafirisha mali asili kama wanyama kwa wingi kiasi cha kutengenezewa meli yao. Hata hivyo hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa huo mfano wa kondoo huko australia walikuwa wanasafirishwa nje ya australia, maana usafiri wa meli huko kati ya mji na mji ni kawaida maana ni kisiwa hicho, Ni kama kusafirisha mifugo toka mwanza kwenda bukoba kwa meli.
 
Mama anazingua sana Sasa hivi.

Anatuuza mchana kweupe, Hapo ametumia Tu lugha ya staha Ila kinacholengwa ni wild animals.

Now, nimeelewa sasa kwanini ilisemwa mwanamke ni kiumbe dhaifu even if amesoma Ila Bado haiondoi udhaifu wake wa kiasili.

Pamoja na mazuri yake Ila kwa haya yanayoendelea mama anatuangusha sana.

Namuombea kwa Mungu apate kuamshwa kwenye usingizi wa fikra.
Haya ndio mawazo ya mtanzania wa kawaida, kudhani kila siku anaibiwa yeye tu!. Unaweza kuweka ushahidi wa wizi utakavyokuwa?.
 
Hakuna mfumo dume wala nini! hapa! mtu ukiwa na integrity ndogo ni ndogo tu!
Hivi mnajua huyu ni binti yake yule aliyeingia mkataba wa loliondo yule ruksa aliyeruhusu kuuza loliondo na mwandishi mmoja stan katabalo akalogwa akafa kwa kufuatilia!?
Hivi mnajua huyu amezaa mtoto na yule rais aliyeifundisha tanzania ufisadi na hasa kusafirisha wanyama pori hai kupeleka arabuni? Amemzaa Rit1 mwanae ambaye sasa amempa uwaziri wa ardhi yetu? Twafwaaa!

Fikiria sasa- Samia mwanae Mwinyi, Samia mamaye Ritz1, Ritz1 wa jakaya----Tutapona???

Serious hakuna uchama hapa ila ndugai na uzuzu wake alituamsha kidogo tukamzodoa akapigwa na kitu kizito.
Hizi ni hisia zako tu mkuu.
 
Hapa ndipo utakapo gundua kama nchi, hatuna viongozi makini na wenye maono!
Yaani viongozi wa ccm wanaona fahari kuuza nchi kwa vipande 30 vya fedha!

Hawajawahi kuwa na uchungu na maliasili zetu. Badala ya kuwauzia hao Waarab nyama iliyochakatwa kwenye viwanda vyetu vya ndani! Eti unawauzia wanyama walio hai!
Maliasili zetu ni kama mapambo tu kama hatuzitumii na zikatuzalishia pesa. Ni akili ya kimaskini kujisifu kuwa tumejaliwa mali nyingi halafu hakuna mkakati wa kuzigeuza kuwa pesa.

Ni uoga pia kuendelea kuahirisha matumizi ya rasilimali hizi huku miaka ikiwa inakwenda kwa kasi.
 
Somalia sio nchi ya kufananisha na chochote. Somalia ni failed state, Hakuna serikali

Una uhakika Hakuna serikali Mbona juzi wamefanya uchaguzi

Sisi tuna kila kitu kuwazidi ila bado tunaomba
Tusibishane kwa failed state or not hapa tunaongelea biashara Mkuu
Kuna watu wanapeleka bidhaa sana huko na hata Oman wanafanya sana biashara huko
 
Kusafirisha wanyama hai hata wa porini si kitu kigeni. Kilicho kigeni sasa ni kule kutengenezwa meli kabisa ili kuvuna kabisa na kufilisi kabla ya 2030 na tuachiwe mbuga tupu! Si ajabu wakahamishiwa zenj wengine, na watalii wakawa wanaishia zenj.
 
Watanzania tuna shida vichwani. Si bure, tupimwe.
 
Maliasili zetu ni kama mapambo tu kama hatuzitumii na zikatuzalishia pesa. Ni akili ya kimaskini kujisifu kuwa tumejaliwa mali nyingi halafu hakuna mkakati wa kuzigeuza kuwa pesa.

Ni uoga pia kuendelea kuahirisha matumizi ya rasilimali hizi huku miaka ikiwa inakwenda kwa kasi.
Matumizi ya mali asili siyo kuihamishia kwa waarabu halafu kizazi kijacho kikose chochote!! Matumizi sahihi ya maliasili kwenye mbuga zetu ni utalii endelevu!! Wawekezaji wajenge mahoteli mazuri ya kitalii na watumishi waajiriwe watanzania, kuboresha miundombinu na kuboresha mazingira ya wanyamapori!
 
I don't think timing ya safari na pia hayo anayoongelea is best ...
 
Hii ni fursa nzuri sana kwa mauzo ya Mbuzi, Kondoo na Ng'ombe ila ni vizuri serikali "isiwatafute" watakaorusha mtandaoni picha za Twiga na Pundamilia wakiwa kwenye meli tayari kuelekea Oman! maana hakuna siri siku hizi!! teknolojia iko juu!!

Iwapo watasafirisha wild animals kwenda Oman tutakuwa na Rais mbaya mno kuwahi kutokea na sidhani kama katiba itabaki salama akimaliza muda wake tutaichanachana na kufuta uongozi wa kinamama milele!!

Hivi ulaya hawapokei wakimbizi wasiopenda kuongozwa na mwanamke nchini mwao? wengine hatumuelewi Bimkubwa!!
 
Back
Top Bottom