Hakika hawa machawa wa mama Kizimkazi wanatuona Watanzania bado ni wajinga sana!
Omary Mjenga ni mwanadiplomasia Mwandamizi na Mtendaji Mkuu wa National Defense College leo ametetea Rais Samia kutumia ndege ya ATC aina ya Boeing Dreamliner yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 100 kibiashara kwa hoja kuwa angetumia ndege ya Rais aina ya Gulfstream gharama ingekuwa mara 7 zaidi!
Amesema hayo wakati akihojiwa na Farhia Middle kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV. Bw. Omary amejenga hoja kuwa Rais anasafiri na ujumbe wa watu wengi wakiwemo walinzi na wasaidizi kadhaa mbali na wataalam! Ameongeza kusema angesafiri kwa Gulfstream ingelazimu wajumbe wengine kusafiri kwa ndege za kibiashara.
Bw. Omary anatakiwa atueleze je kuna umuhimu wa Rais kusafiri na watu zaidi ya 100 katika ziara zake nchi za nje? Uzoefu wetu unaonyesha huwa anasafiri na machawa wake wakiwemo wasanii ambao hawana mchango wo wote katika mazungumzo ya kiserikali na wafanyabiashara ambao wanatumika kuhujumu na kufisadi mali za umma!
Bw. Omary atueleze ni hasara kiasi gani ATC inapata kwa ndege kutofanya biashara kipindi chote cha ziara za Rais?
Bw. Omary atueleze ni faida gani tutapata kutokana na mwaliko wa Rais kuhudhuria mkutano wa G20 akiambatana na watu zaidi ya 100 na kitu gani tungekosa kama angesafiri na watu wachache?
Maswali ni mengi lakini kwa kweli Watanzania tumepigwa!